Msanifu maarufu wa utengenezaji wa magari ikiwemo miundo ya Ferrari na Fiat Sergio Pininfarina (pichani) wa nchini Italia amefariki dunia nyumbani kwake katika mji wa Turin baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Pininfarina alisanifu miundo maarufu ya magari ikiwa ni pamoja na Ferrari, Fiat na Maseratis na pia magari aina ya Peugeot na Mitsubishi.
Sergio Pininfarina pia alikuwa mbunge wa bunge la Ulaya hadi mwaka wa 1988 na baadaye kukiongoza Chama cha Wafanyabiashara wa Italia.
Waziri Mkuu wa Italia Mario Monti amesema kuwa Pininfarina alizaliwa na kipaji cha kuleta pamoja uzuri na ubora katika kazi yake.
Sergio Pininfarina alizaliwa katika mji wa viwanda wa Turin Kaskazini mwa Italia na amefariki akiwa na umri wa miaka 85.