Baada ya movie yake ya Crazy Tenant iliyoigizwa na Wema Sepetu na Peter Msechu kuwa filamu iliyouza zaidi mwezi May hadi June mwaka huu nchini, super director Selles Mapunda anakuja tena na Best Losers.
Katika Best Losers Mapunda amewashirikisha Aunt Ezekiel na Stephen Mapunda na pia kwa mara ya kwanza amewatambulisha kwenye Bongo Movies akina dada ndugu wa kundi la muziki wa injili J-Sisters, Juliet,Judith,Jesse na Josephine.
SYNOPSIS:
Ndoto ya kila msichana jijini Dar es Salaam ni kuhamia Ulaya na kuishi maisha mazuri. Janet (Aunty Ezekiel), Juliet, Judith, Jesse & Josephine (J-Sisters). Akinana hawa wanapoteza miaka mingi kwa maisha yaliyofeli. Lakini ghafla wanagundua mgodi wa dhahabu “pesa zilizoibwa zikiibwa” EPA.
Tofauti na matarajio yao wanakutana na mambo wasiyoyajua kutoka kwa Jackson (Rado) mtu aliyekuwa karibu na marehemu Mapunda (aliyekuwa mbunge) katika mishimishe yao ya kuwa mabilionnare na Jackson hawezi kukubali waharibu ndoto yake.