Hatimaye Chris Brown ameizungumzia ofa iliyotolewa na tajiri wa Marekani Alki David ya kuingia ulingoni kuzichapa na adui yake Drake kwa malipo ya dola milioni 9 kwa mshindi na milioni moja kwa loser.
Pambano hilo litakuwa na raundi tatu zenye dakika moja.
Kwa mujibu wa mtandao wa RumorFix, miongoni mwa wapiga picha wa mtandao huo alionana na Chris Brown jana na kumuuliza kama anaweza kukubali ofa hiyo na yeye kujibu,”Yeah, I would. I would.”
Siku chache zilizopita Chris Brown ametoa wimbo wa kumdiss Drake na hivyo kuchochea zaidi beef lao.Drake amesema hatojibu diss hiyo.
Katika taarifa nyingine, wakati ambapo kila msanii amejaribu kuzungumzia beef inayoendelea kati ya Chris Brown na Drake, wapo ambao wameamua kuchukua upande mmoja.
Ukianzia kwa Gayle King ambaye alisema yupo kwenye timu ya rizzy hadi kwa Big Sean aliyesema Breezy ndio mwana wa ukweli zaidi.
Hata hivyo mwanadada Kelly Rowland amesema yeye anabaki neutral na kukubali kuwa anawazimia wote.
“Oh, huwezi kunifanya nichague. Ukweli ni kwamba nawapenda wote,” nyota huyo aliuambia mtandao wa Bossip.
“Ni wasanii wazuri. Sidhani kwamba mtu yeyote anatakiwa kuchagua kati yao.