Sony Music Entertainment imemsainisha mtoto mwenye kipaji cha hali ya juu aitwaye Kamsee aliye na miaka 12 kwenye roster ya wasanii wake.
Kamsee anaungana na wasanii wakubwa kwenye kampuni hii ya muziki ya pili kwa ukubwa duniani ikiwa na wasanii kama Beyonce,Usher, Britney Spears, Celine Deon, Chris Brown, Jordin Sparks, John Legend, Madonna, R.Kelly na wengine kibao.
Staa huyo mtoto atakuwa chini ya uangalizi na utayarishaji wa timu ya utayarishaji wa muziki ya Afrika Kusini iliyowahi kushinda tuzo za SAMA Jax Panik, ambao watatengeneza nyimbo zilizotungwa na Kamsee zitakazotoka mwaka huu.
Umaarufu wa Kamsee Ekpenyong, mwanafunzi wa Trinity International College, ya Ofada, Nigeria, ulianza baada ya kuonekana kwenye mtandao kwa nyimbo zake ‘Friends’ na Father In Heaven’ zilizoonesha kipaji chake.
Mkataba huu wa kufanya albam kadhaa na Sony Music Entertainment, pamoja na kuhudumiwa kila kitu na Sony Music pamoja na ROCKSTAR4000, ni wa kwanza kwa msanii mwenye umri kama wake katika nchi yoyote barani Afrika.
Paul Thackwray, Meneja mkuu wa Columbia / Epic upande wa Sony Music Africa,alisema: “Tunafurahi kumuunganisha Kamsee kwenye line-up ya wasanii wenye vipaji vya hali ya juu na tunategemea kuiendeleza career yake.”
Mpaka sasa mtoto huyo ambaye alianza kupiga piano akiwa na miaka mitano, ameshafanya show na wasanii wakubwa kama Wizkid, 2face Idibia na Stella Damasus

source:bongo5.