Polisi nchini Togo wamelazimika kufyatua mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji wanaoipinga serikali ambao wanajaribu kufanya maandamano ndani ya uwanja wa mpira katika mji mkuu wa Lome.
Majeshi ya usalama yamezuia eneo kubwa la mji huo na kufyatua mabomu ya kutoa machozi dhidi ya watu ambao wamekuwa wanajaribu kuingia katika eneo hilo.
Polisi pia wamefyatua mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya mamia ya wapinzani ambao walikusanyika mbele ya ubalozi wa Ufaransa katika mji mkuu wa Lome.
Nchi ya Togo ambayo ni koloni la zamani la Ufaransa imekuwa ikikumbwa na maandamano yenye ghasia katika kipindi cha wiki tatu zilizopita, ambapo waandamanaji wanataka mabadiliko katika mfumo wa uchaguzi nchini humo.