Tromøy, Arendal (Norway).
Mwanamke mwenye asili ya Tanzania anatafutwa, ametoweka nyumbani baada ya kudai kudundwa na mmewe tangu Jumatatu .

Huyu ndiye dada wa Kitanzania aliyepotea toka Jumatatu hajaonekana mpaka leo. Bado anatafutwa! Polisi wanaomba msaada wa wananchi kwa yeyote anayefahamu lolote kuhusu huyu dada.
Mbwa wa polisi wakisaidia kwenye msako wa kumtafuta mwanamke mwenye asili ya Tanzania aliyepotea Tromøy, Arendal. Picha na Anne Karin Andersen (Agderposten)
Jana saa moja mwanamke mmoja alipiga simu polisi na kusema kuwa amepigwa nyumbani kwake. Baada muda mfupi, akaonekana ametoka nyumbani kwake, maeneo ya Tromøy, Arendal. Ametoweka na hajaonekana tokea jana. Mwanamke huyo ana asili ya Tanzania.
Mumewe alitoa taarifa polisi baada ya kutoonekana kwa muda mrefu. Tokea jana amekuwa akitafutwa na helikopta, boti za polisi, polisi wenye mambwa, jamaa wa msalaba mwekundu na watu wa kujitolea.
Source: watanzaniaoslo