NDG WAANDISHI WA HABARI   [MICHEZO]

AWALI YA YOTE NINAPENDA KUTOWA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWENU KWA JINSI AMBAVYO VYOMBO VYENU VYA HABARI VIMEKUWA VIKITUSAIDIA SANA KATIKA KUUKUZA MCHEZO HUU WA NGUMI ZA KULIPWA KWA KUUANDIKA VIZURI SANA NA HATIMAYE KURUDISHA IMANI KUBWA KWA WAPENZI WAKE AMBAO TAYARI WALIKUWA WAMEUKIMBIA KUTOKAN NA SABABU AMBAZO MNAZIFAHAMU FIKA ,NA HATA WADHAMINI KUKAA PEMBENI NA KUUTELEKEZA KABISA.

LKN MIAKA ANGALAU MINNE BAADA YA KUPOTEZA MWELEKEO HATIMAYE MASHABIKI WAMEUPOKEA TENA KWA MIKONO MIWILI ,

HIVI KARIBUNI TAYARI PEPO MBAYA AMEANZA KUJITOKEZA KWA LENGO LA KUUVURUGA TENA MCHEZO HUU AMBAO NI NGUVU KAZI YA VIJANA KTK KUJIPATIA PESA ZA KUJIKIMU KIMAISHA KUPITIA NGUMI ZA KULIPWA.

HIVI KARIBUNI VYOMBO VYENU VYA HABARI VIMEKUWA VIKIRIPOT TAARIFA ZA MVUTANO MKUBWA ULIOJITOKEZA KATI YA BONDIA FRNCIS CHEKA NA WAANDAAJI WA TAMASHA LA USIKU WA MATUMAINI KUHUSU PAMBANO LAKE NA JAPHET KASEBA HUKU CHEKA AKIKANUSHA KWAMBA HAKUSAINI MKATABA WA KUCHEZA NA JAPHET KASEBA NA BADALA YAKE ALISAINISHWA KUPIGANA NA BONDIA KUTOKA MISRI.HAPO TAREHE 07-07-2912 KTK UWANJA WA TAIFA

KIMSINGI TU CHEKA ANAJARIBU KUWAFANYA VIONGOZI WA KAMISHENI YA NGUMI ZA KULIPWA -TPBC HAWAJUWI WAJIBU WAO KWA KUMPA PROMOTA KIBALI CHA KURUHUSU PAMBANO AMBALO NI FEKI WAKATI SIYO KWELI ,

MIMI BANAFSI NILIPATA NAFASI YA KUONGEA NA CHEKA NI KWA NINI ALIPIMA UZITO HALI AKIJUWA HATACHEZA PAMBANO ? NA KWA NINI ALIFIKA UWANJANI HALI AKIJUWA HACHEZI PAMBANO ? ALISHINDWA KUNIJIBU .MAHOJIANO HAQYA TULIYAFANYA SIKU YA PAMBANO NDANI YA UWANJA WA TAIFA.

TPBO INAAMINI KWA DHATI KABISA KWAMBA LENGO LA FRANCIS CHEKA LILIKUWA NI KUJARIBU KUTENGENEZA MAAFA MAKUBWA AMBAYO YANGESABABISHA UVUNJIFU WA AMANI KWA KWA MASHABIKI AMBAO WALIKUJA MAHUSUSI KUANGALIA PAMBANO LILE .

NDG ZANGU WAANDISHI WOTE HEBU JIULIZENI KAMA PAMBANO HILI LINGEKUWA NI LA KAWAIDA NA LIMEPANGWA KUFANYIKA KATIKA UKUMBI WOWOTE ,NA PROMOTA AMESHAWATOZA WATU PESA NA WAMEJAA UKUMBINI ,NA KISHA FRANCIS CHEKA AMEINGIA UKUMBINI NA KISHA KUKATAA KUPIGANA JE MNADHANI MASHABIKI WANGEKUBALI ? NI LAZIMA WANGEFANYA VURUGU KUBWA AMBAYO INGEWEZA HATA KUPTEZA MAISHA YA WATU WENGI SANA NA VYMBO VYENU VYA HABARI VINGEKUWA NA KAZI KUBWA SANA YA KUWAHABARISHA WATANZANIA JUU YA MAAFA HAYO AMBAYO YANGSABABISHWA NA UJINGA WA MTU MMOJA TU FRANCIS CHEKA.

TPBO IMESIKITISHWA SANA NA TUKIO HILI AMBALO LIMEUVUNJIA KABISA HESHIM A MCHEZO HUU ,NA HASA UKUZINGATIA KWAMBA VIKUNDI MBALIMBALI VILISHIRIKI KUCHANGIA UJENZI WA MABWENI A WASICHANA ,NA HATA WAREMBO WALIJITOLEA KUPANDA ULINGONI KWA LENGO LA KUCHANGIA ELIMU.

TPBO INAWAPONGEZA WASANII WOTE WA BONGO MOVIE ,WANAMUZIKI WA AINA ZOTE ,NA WABUNGE WOTE KWA MOYO WAO WA HURUMA WALIOUNYESHA KUFANIKISHA LENGO LA TAMASHA HILO .PIA PONGEZI KWA MABONDIA WOTE WALIOKUBALI KUSHIRIKIKUCHANGIA

BONDIA FRANCIS CHEKA AMESHINDWA KABISA KUWATHAMINI WANAJAMII AMBAO KWA MCHANGO YAO WAMWEZA KUMFANYA AJULIKANE TANZANIA NZIMA ,NA AMEWADHARAU SANA NA AMUVJUNJIA HESHIMA MCHEZO WA NGUMI ZA KULIPWA KWA UJUMLA  WAKE ,NA AMEUDHALILISHA SANA MCHEZO HUU MBELE YA JAMII YA KITANZANIA NA AMEWAFANYA MAADUI WASIOUTAKIA MEMA MCHEZO HUU KWA KUTOKUUDHANINI WAAMINI KWAMBA HUU NI MCHEZO WA WAHUNI NA WAVUTA BANGI .

IMANI ZA TPBO
————-

KUTOKANA NA MAELEZO YOTE NILIYOYATOWA KWENU NI VIZURI PIA MKAJUWA IMANI   ZA TPBO

[1] TPBO INAAMINI KABISA KWAMBA INAAMINIWA NA WATANZANIA WOTE WAPENDAO NGUMI ZA KULIPWA KOTE NCHINI TANZANIA NA INAZINGATIA NIDHAMU NA INAPIGA VITA UTUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA MICHEOZNI ,NA HATA BIASHARA YENYEWE YA MADAWA HAYO. KWA WANAMICHEZO WOTE NCHINI

[2] TPBO INAAMINI KABISA KWAMBA NGUMI ZA KULIPWA NI KAZI KAMA KAZI NYINGINE AMBAZO HUMPATIA BINAADAMU KIPATO CHA HALALI ILI KUJIKIMU KIMAISHA.

[3]TPBO INAAMINI KABISA KWAMBA HAKUNA BONDIA YEYOTE MWENYE AKILI TIMAMU AWEZAYE KIDHARAU JAMII IILYOMZUNGUUKA NA KUFANYA AWEZE KUFANYA MABO AMBAYO YATAIKERA JAMII HIYO .

[4] TPBO INAAMINI KWAMBA KILA BONDIA ANAZO HAKI SAWA ZA KUTETEWA NA KULINDIWA HAKI ZAKE PAKE ZINAPOKUWA HATARINI KUPOTEA.

[5] TPBO INAAMINI KABISA KWAMBA WAKUZAJI [MAPROMOTA] WATAPEWA MSAADA MKUBWA PALE WANAPOANDAA MAPAMBANO YAO NA WANAPATA USHIRIKIANO WA DHATI KUTOKA KWA MABONDIA ,IKWA NI PAMOJA NA KUTANGAZIWA MAPAMBANO YAO KWA USHIRIKIANO MKUBWA NA MABONDIA WAHUSIKA.

[6] TPBO INAAMINI KABISA KWAMBA WAPENZI WA NGUMI ZA KULIPWA WANAZO HAKI ZA KUPATA BURDANI YA MCHEZO HUU IL WAEENDELEE KUUPENDA KWA FAIDA YA MABONDIA WOTE .

[7] TPBO INAAMINI KILA BONDIA ANAPASWA HUHESHIMIWA NA HAKUNA BONDIA ALIYE JUU YA SHERIA NA KANUNI ZA MCHEZO ZIENDESHAZO NGUMI ZA KULIPWA.

NA TPBO INAAMINI KABISA KWAMBA  MWENYE MAMLAKA YA KUBADILISHA MPINZANI WA CHEKA NI PROMOTA NA SIYO BONDIA ,NDIPO CHAMA HUSIKA KINATOWA KIBALI KWA AJILI YA PAMBANO HILO ,NA NDIYO MAANA HATA RAIS WA TPBC KUPITIA VYOMBO VYA HABARI ALIUTANGAZIA UMMA WA WATANZANIA KWAMBA ANAITAMBUWA MKATABA /MIKATABA ALIYOISANI FRANCIS CHEKA KUPAMBANA NA JAPHET KASEBA.

MAAMUZI MAGUMU YA TPBO
—————————

\ KWA KUWA JAMII YA WAPENZI WA NGUMI ZA KULIPWA WAMEFADHAISHWA SANA NA TUKIO LILIOFANYWA NA BONDIA FRANCIS CHEKA NAMI NAUNGANA NAO KTK MFADHAIKO HUO NA KUWAOMBA MSAMAHA KWA TUKIO HILO ,NA ILI KUHAKIKISHA KWAMBA SOTE TUMEFADHAISHWA NA JAMBO HILO-;

TPBO INAMUONDOWA  RASMI BONDIA   FRANCIS CHEKA KATIKA ORODHA YA MABONDIA INAOWATAMBUWA NA HAITAFANYA NAYE KAZI YA IANA YOYOTE KTK ULIMWENGU WA MASUMBWI KTK KIPNDI CHOTE CHA UHAI WA TPBO. NA UHAI WANGU BINAFI.

HII HAINA MAANA KWAMBA ANAKATAZWA KUCHEZA NGUMI ,LA BALI HUU NI MSIMAMO WA TPBO ,NA DAIMA MIMI HUIFANANISHA TPBO NA SIMBA DUME LENYE MENO NA AMBALO HALITAKI KULA MIZOGA , LKN KAMA VIKO VYAMA NINAVYODHANI KWAMBA BILA CHEKA HAVIWEZI KUIMARIKA NA VIMTUMIE SINA PINGAMIZI NAVYO.

TPBO IPO IMARA NA ITAENDELEA KUWA IMARA KWA KUFANYA KAZI NA MABONDIA WENYE NIDHAMU NA KATIKA MAAMUZI YETU HATUMUOGOPI YEYOTE ILI MRADI TUMO NDANI YA SHERIA NA KANUNI ZA MCHEZO

AHSANTENI SANA

NB- KWA TAARIFA HII NINAUFUNGA RASMI MJADALA KUHUSU BONDI FRANCIS CHEKA.

IMEANDIKWA NAMI ;-
YASSIN ABDALLAH -USTAADH