Baadhi ya waombolezaji wakibeba jeneza lililowekwa mwili wa merehemu Kati Kerenge kabla ya mazishi yake yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Jumamosi Julai 7 jijini humo. Marehemu Kati aliyekuwa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Barclays alifariki Julai 1 jijini humo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina akizungumza wakati wa misa.

Mama mzazi wa marehemu Kati Kerenge, Professor Apollonia Kerenge (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya waombolezaji katika misa ya mazishi iliyofanyika katika kanisa la Prebeterian la Mt. Columbus jijini Dar es Salaam Jumamosi Julai 7 jijini Dar es Salaam.

Aliyekuwa Mkuu wa Rasilimali Watu wa Tanga Cement ambaye marehemu alishawahi kufanya kazi, Bi. Jayne Nyimbo akizungumza. Kwa sasa Bi Jayne ni Mkuu wa Rasilimali watu wa kampuni ya Twiga Cement.

Mama mzazi wa marehemu Kati Kerenge, Professor Apollonia Kerenge akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu mwanawe.

Baadhi ya marafiki wa marehemu Kati Kerenge wakiweka mashada ya maua juu ya kaburi alilozikwa, Kinondoni, Dar es Salaam Jumamosi Julai 7 mwaka huu.

source:fatherkidevu