Hakutaja majina lakini Rihanna ameonesha kuzungumzia mahaba mazito aliyokuwa nayo kwa Chris Brown kwenye jarida la Harper’s Bazaar litakalotoka mwezi August.
“Nilipokuwa nimependa, nilipenda hasa. I was really, really, really in love,” Rihanna, 24, aliliambia jarida hilo.
“The way it made me feel was priceless. And in a blink of an eye my whole life changed. Everything that I knew was different.”
Ingawa Rihanna na Brown, 23, waliachana rasmi February 2009 baada ya ugomvi uliomwacha Rihanna na majeraha usoni, wameendelea kuwasialiana na miezi kadhaa iliyopita walishirikishana kwenye nyimbo zao.
Pia mtandao wa Us Weekly, umesema wapenzi hao wa zamani wamekuwa wakionana kisirisiri.
Akizungumzia mahaba hayo bila kumtaja mhusika, Rihanna Ameliambia jarida la Harper’s Bazaar kuwa anasita kupenda tena: “I never thought I’d feel that pain in my life. I’m afraid of feeling that again.”
Mwanadada huyo na muigizaji wa filamu ya Battleship pia amesema anashangazwa na jinsi anavyoendelea kukonda kila siku.
“Sijui kama kuna kitu kinaendelea kwenye mwili wangu sasa hivi, lakini nakula kitu katika maisha yangu, anasema Rihanna. “I miss my ass. It just went away! I need a butt. I have an idea of one, but it’s not living up to its full potential right now.”

source:bongo5.