In unconfirmed news tumesikia kwamba Chameleone and his crew’s passports have been detained by Eric Shigongo akimtaka ampe dola 3500 aliyotapeliwa na waganda wasiofahamika.
Kwa mujibu wa Chameleone yeye anasema saga hilo limetokea jana wakati anajiandaa kuondoka nchini mida ya saa nane kasoro ambapo mmoja wa wafanyakazi wa Shigongo alimuomba passport yake na za wenzake wawili aliokuja nao ili watoe photocopy baada ya hapo akaambiwa kuwa Shigongo amechukua passport zao ili alipwe hela aliyotapeliwa mwanzo kiasi cha dola 3500 ambazo alitoa kama deposit ya msanii huyo kuperfom.

Chameleone aliendelea kusema kuwa kwa upande wake hahusiki na utapeli huo kwani watu ambao anamhusisha nao amewasikia kupitia kwa msanii wa kirundi Kidum ambaye ndiye aliyemkconnect na watu hao, Chameleone alisema ‘mimi nilishangaa Kidum aliponipigia simu na kuniuliza kama nakuja tz, nikamuuliza mbona sijui kitu? akasema sii hela umepewa kupitia meneja wako, nikamwambia meneja wangu hajapokea pesa yeyoye! Sasa nilivyofuatilia nikagundua watu ambao walimtapeli walimwalika Shigongo Kampala na kumwambia kuwa ni managers wangu na kitu walichofanya ni kutumia gari kama langu aina ya range rover nyeupe ambayo mimi natumia bila number plate wakamwambia kwamba wanahusika na mimi ndio maana ametuachia gari lake. Kuona hivyo Shigongo akatoa deposit nusu ya pesa ya shoo ambayo ilikuwa iwe dola elfu 7 baada ya hapo jamaa wakakata mawasiliano sasa Shigongo ananihusisha vipi na watu ambao mimi siwajui amwambie Kidum arudishe kwa sababu yeye ndiye aliyempa contact ya huyo meneja feki’.

Mpaka tunaandika habari hii hatujapata uhakika kama Chameleone bado yupo nchini kwani alitakiwa kuondoka mida ya alasiri. Pole sana kaka Shigongo kwa kukumbwa na utapeli huo, kwa kweli wakati umefika wa kuwa na booking agencies zinazoeleweka na kuaminika!

source:bongo5.