Mwanahip hop mashuhuri nchini Tanzania, Fareed Kubanda aka Fid Q leo usiku anatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha la filamu la kimatafa la Zanziba, ZIFF.
Fid Q ataipeleka hip hop kwenye level nyingine kabisa kwakuwa amesafiri na bendi yake iitwayo ‘Fid and The Band’.
Miongoni mwa wataokampa support kwenye show ya leo ni pamoja na mwanamuziki wa Sweden aishie nchini, Saraha Msanii na mshiriki wa Tusker Project Fame mwaka huu, Damian.
“Jumanne usiku napiga show pamoja na Fid Q na band yake @ Zanzibar International Film Festival! Karibuni!” aliandika Saraha jumapili hii.
Wasanii wengine wa Tanzania waliopo kwenye orodha ya kuperform mwaka huu ni Diamond, Linah, Barnaba, Roma, Shetta, Nakaya, Carola Kinasha,Charlotte O’neal, Tazneem,Shilole, Swahili Vibes,Black Roots, Synerg, Sultan King na wengine.
Pamoja na burudani leo filamu tatu zitaoneshwa Ngome Kongwe ambazo ni FANTASY, PAPANZENU na 35 and TICKING.
Tamasha hilo litaendelea hadi jumapili ya tarehe 15, July.