Mchezaji wa mpira wa kikapu cha kulipwa katika ligi ya NBA ya Marekani, mtanzania Hasheem Thabeet kesho Jumatano, anatarajiwa kusaini mkabata rasmi wa miaka miwili kukipiga na timu ya Oklahoma City Thunder.
Kama akisaini kesho anaweza kucheza kwenye mechi tatu za mwisho akiwa na timu yake mpya kwenye Orlando Pro Summer League.
Thabeet hawezi kusaini rasmi mkataba wake mpya na Thunder hadi kesho pindi msitisho rasmi wa free agent huyo ukitolewa. Kabla ya hayo kufanyika, bado sio mchezaji wa kimkataba na timu ya Thunder.
Hata hiyo haimkatazi Thabeet kucheza kwakuwa wachezaji kumi kati ya 14 wa OKC kwenye roster ya summer league hawana mkataba na Thunder.
Lakini wachezaji hao kumi hawana siku moja tu zilizosalia ili kusaini mkataba unaohusisha malipo kama Thabeet.
Wachambuzi wa masuala ya mchezo huo nchini Marekani wanasema kuwa Thabeet anaweza kusaini mkataba huo kesho asubuhi kwa saa za Marekani na kuingia uwanjani rasmi.
Thabeet anatarajiwa kujiunga na timu yake wiki hii mjini Orlando na anaweza kushiriki kwenye mazoezi wiki hii yote na kama kesho akisaini mkataba hakutakuwa na chochote tena cha kumzuia kucheza.
Ni wachezaji wachache wanaohitaji muda wa kucheza kumzidi Thabeet, na ndo maana ni lazima acheze wiki hii.
Kwa misimu miwili iliyopita Thabeet amecheza kwa dakika 512 tu.