Miaka miwili iliyopita,kocha wa klabu ya Real Madrid,Jose Mourinho alizuru nchini Kenya na alisema amenununua kidani kwa msichana sonara ambaye alimtumia aliporudi Hispania.
Na sasa gazeti la The Star la Kenya limesema msichana huyo aitwaye Lelesit Silvana, anatarajiwa kusafiri hadi nchini Poland mwezi September mwaka huu kukutana na Mourinho.
Msichana huyo mwenye miaka ishirini na kitu amesema amekuwa akiwasiliana na kocha huyo kwa e-mail na ziara yake hiyo itakayolipiwa kila kitu nchini Poland itamfanya akae mwezi mzima na kutembelea majiji mbalimbali.
Hata hivyo Silvana alikuwa wa haraka kukanusha uhusiano wowote wa kimapenzi kati yao kwa kusema kuwa ana mpenzi tayari.
“Nina furaha na hii ilikuwa ni ndoto yangu, lakini nina mpenzi mkenya mwenye asili ya kisomali ambaye tumekuwa wapenzi kwa muda,” Silvana aliliambia The Star.
Wakati wa ziara hiyo ya Kenya mwaka 2010 Jose Mourinho alikaa kwenye hoteli ya kifahari ya pwani nchini Kenya ya Almanara akiwa na mke wake na watoto wao wawili (wa kike na wa kiume) wakiwa chini ulinzi mkali.
Ndio hapo alipokutana na Silvana na kumpa order amtengenezee mkufu wa Tanzanite wenye gharama ya shilingi 500, 000 za Kenya(Milioni 9 za Tanzania).
Kulikuwa na uzushi kuwa katika ziara yake ya siku 12 nchini humo, kocha huyo alikutana na waganga wa kienyeji ili wamfanyie mambo kwakuwa ndo alikuwa anaenda kuanza kazi ya kuinoa Real Madrid.

source:bongo5.