kamishna msaidizi wa polisi Ahmed Msangi

Nahitaji ufahamu kwamba hii nafasi nimeitoa rasmi leo kwa sababu ya ishu ambayo imekuzwa na mitandao ya kijamii inayotumiwa sana na watanzania wengi muda mfupi baada ya kamishna msaidizi wa polisi Ahmed Msangi kumtembelea hospitali kiongozi wa Madaktari Dr Ulimboka Steve ambapo mistari kadhaa imesambazwa kwenye mitandao hiyo ikimuhusu Kamanda Msangi.

Mistari ambayo ni maarufu ambayo inadaiwa kutolewa na mtu anaedai alisikia kila kitu ni kwamba Dr Ulimboka alipomuona tu Kamanda Msangi amekwenda kumtembelea hospitalini, alianza kumwambia ampe viatu vyake pamoja na simu yake, ikimaanisha kwamba Ahmed Msangi alikuepo wakati Dr Ulimboka akifanyiwa huo ukatili.

Exclusive na millardayo.com Msangi amesema “hata mimi hizo habari nimezisikia na kuzisoma kwenye mitandao na msg zinazotumwa, kiukweli taarifa hizo zote sio za kweli kuna mtu tu amekaa na kuona atunge kitu labda kwa malengo yake mwenyewe, ni kweli nilikwenda kumtembelea hospitalini na nilipitia kwa mkurugenzi wa Moi na ndio tukaambatana pamoja kwenda wodini kumuona Ulimboka, ananifahamu na mara nyingi tunakutana hata kwenye sehemu za kufurahi hivyo akanihadhia jinsi ilivyokua na nikamuuliza maswali kwa ajili ya upelelezi”

Haijawezekana kumpata dr Ulimboka sasa hivi kwa sababu ya taratibu za hospitali, lakini nitaitumia nafasi kwa saa chache zijazo… mpango ukifanikiwa ripoti utaipata manake neno lake yeye ni muhimu sana kwenye hii ishu.

source:millardayo