Habari njema kwa warembo wa Tanzania na Afrika kwa ujumla hasa wale ambao wangependa kuvuka border katika masuala ya urembo.
Mwanamitindo mkongwe na maarufu duniani, Naomi Campbell, akishirikiana na kampuni za Oxygen Media na Shine America wanaanzisha shindano liitwalo The Face ambapo watakuwa wakisaka warembo barani Africa.
The Face litakuwa shindano litakalorushwa kwenye TV ambapo warembo hao watakuwa wakipewa changamoto na kufundishwa mambo ya urembo na masupermodel waliofanikiwa zaidi duniani.
Mshindi atakuwa kisura wa brand kubwa.
Shindano hilo linawataka wasichana wanaopenda kujiingiza kwenye masuala ya urembo ama hawana muda mrefu tangu waanze shughuli hizo.
Wanatakiwa wawe na zaidi ya miaka 18 ili kushiriki hasa wakiwa na urefu wa 5’7′ na zaidi.
Kama wewe ni mrembo na ungependa kushiriki, tuma picha saizi ya kichwa (heads shot) na mwili mzima (full body) kwenda kwenye e-mail hii theface@bethmodelafrica.com (Warembo wa Africa tu)na mwisho wa kutuma ni July 12, 2012.

source:bongo5