MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania bara Simba na Mabingwa wa michuano ya kombe la Mapinduzi Azam FC kesho watakutana katika mchezo wa fainali wa michuano ya kombe la urafiki utakaopigwa kwenye dimba la Amaan, visiwani Zanzibar. Azam imetinga hatua hiyo baada ya kuikwanyua Super Falcon mabao 2-0 huku Simba ikikata tiketi hiyo baada ya kuifunga All Stars bao 1-0. Mchezo huo wa fainali utakuwa wa pili kuzikutanisha timu hizo katika michuano hiyo ambapo awali zilikutana katika hatua ya makundi na kutoka sare tasa.