Uongozi wa timu ya Barcelona umepinga vikali maamuzi ya chama cha mpira nchini humo kumfutia adhabu kocha wa timu pinzani ya Real Madrid coach Jose Mourinho.
Mourinho alipewa adhabu hiyo mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kumsukumiza kwa kidole jichoni kocha msaidizi wa Barcelona ambaye ndiye kocha mkuu kwasasa Tito Vilanova.
Mzungumzaji wa Barca amesema kitendo alichofanya Mourinho kina picha mbaya kwa mpira wa Hispania na kufutiwa adhabu yake ni sawa na kuruhusu vitendo kama hivyo.