Mama mzazi wa wasanii mapacha wa Nigeria Peter na Paul Okoye wa kundi la Psquare amefariki dunia.
Mrs. Okoye amekuwa akiumwa kwa mrefu ugonjwa ambao bado haujajulikana.
Pamoja na Peter na Paul, watoto wake wengine Jude na Ajeh wana mchango mkubwa kwenye muziki wa Nigeria.
Wakati kila mtu anajiuliza nini chanzo cha kifo cha mama yao, mtandao wa niyitabiti.net umebaini kuwa baada ya kuanza kuumwa alipelekwa kwenye hospitali ya St. Nicholas Hospital, miongoni mwa hospitali ghali zaidi nchini Nigeria.Baadaye alipelekwa nchi za nje kwa matibabu zaidi. Bahati mbaya amefariki wakati akiendelea na matibabu hayo.
Muda mfupi baada ya habari hiyoi kujulikana, marafiki na jamaa walianza kutuma salamu za rambirambi kwa familia ya Psquare.Katika maisha yake, mama huyo anafahamika kwa mchango mkubwa kwa mafanikio ya watoto wake. Leo hii P-square ndo wanamuziki wanaolipwa pesa nyingi zaidi nchini Nigeria na barani Afrika kwa ujumla.