Zlatan Ibrahimovic anaweza kuja kuwa ndio mchezaji ghali kihistoria baada ya Paris Saint-Germain kutoa fedha hizo kwa AC Milan ili kuweza mpata mchezaji huyo.
Timu hiyo ya Ufaransa inayoongozwa na Carlo Ancelotti inasemekana imetoa paundi mil 51 kwa ajili ya kumpata Ibrahimovic na Thiago Silva.
Inasemekana Silva amekataa kuihama Milan lakini paundi mil 32 zilizobakia kwa ajili ya kumpata Ibra zinaweza zikakubalika. Kama uhamisho huo ukifanyika basi Ibrah atakuwa amefikisha mjumuisho wa kiasi cha paundi mil 150 katika bei zake ambazo ametolewa kwa ajili ya uhamisho katika klabu zake zote alizowahi cheza za Ajax, Juventus, Inter Milan, Barcelona na AC Milan.

source:dailymail