Hatimaye jana Hasheem Thabeet amesaini mkataba mnono na timu ya Oklahoma City Thunder.
Mwanzoni Thabeet aliliripotiwa kuchukuliwa na timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili lakini mtandao wa The Oklahoman umebaini kuwa mkataba wake ni ‘partially guaranteed’ na unaweza kumweka Oklahoma City kwa misimu mitatu.
Thabeet amehudhuria mechi za summer league huko Orlando, Florida wiki hii, lakini meneja mkuu wa OKC Sam Presti amesema hatocheza na timu yake mpya na badala yake itabidi afocus kwenye maendeleo yake binafsi kwenye kambi ya mazoezi.
“Akiwa kama mchezaji kijana, mwenye miaka 25, ndo kama ameanza tu. Clearly, we feel like there’s an opportunity to impact Hasheem’s development but that’s going to be a process, alisema Presti.
Kwa mujibu wa makala ya mtandao wa bleacherreport.com iliyopewa jina la “Oklahoma City Thunder: Why Hasheem Thabeet Will Thrive with the Thunder” (Kwanini Hasheem Thabeet atafanikiwa na Thunder) umesema kuwa mchezaji huyo akiwa na timu hiyo anaweza kuwa mchezaji aliyekuwa chuoni ambapo alikuwa akihusika zaidi na kuzuia mipira isiingie golini.
“Look out for Hasheem Thabeet to make a thunderous impact in Oklahoma City, where young players go to become stars.He still has time to redeem himself before fans and analysts make comparisons with him to the likes of Darko Milicic and Kwame Brown,” uliandika mtandao huo.

source:bongo5