Mwanafunzi wa darasa la pili (7) katika shule ya msingi Mkombozi amenajisiwa na baba yake wa kambo jana majira ya saa 5:00 usiku huko Shigamba, Mbalizi jijini Mbeya.
Maafisa wa Polisi wamesema mtoto huyo, ambaye jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kiusalama ni mbena na mkazi wa Shigamba amebakwa na Josephat Mtawa (39), Mndali, mkulima na mkazi wa Shigamba ambaye ni baba wa kambo wa mtoto huyo na kumsababishia maumivu makali mwilini mwake.

Maafisa hao wameongeza kusema kitendo hicho cha kinyama kwa mtoto huyo kiligundulika na mama mzazi wa mtoto. Pia mbinu aliyoitumia mtuhumiwa ni kumvizia mtoto alipokuwa amelala sebuleni na kumtoa hadi nje hadi kwenye pagala na kumbaka. Mtuhumiwa yupo mahabusu na taratibu za kumfikisha mahakamani zinaendelea.

Kamishna msaidizi wa Polisi, mkoa wa Mbeya Diwani Athumani ametoa wito kwa jamii kujiepusha na matendo ya udhalilishaji yaliyo nje na kinyume na maadili kwani yeyote atakeye jihusisha nayo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
source:jaizmelaleo