Aliyekuwa jaji wa shindano la American Idol Steven Tyler ameamua kuitosa show hiyo baada kuwepo kwa misimu miwili.
Hatua hiyo imetangazwa jana (July 12) na kituo cha runinga cha Fox.
“After some long, hard thoughts, I’ve decided it’s time for me to let go of my mistress ‘American Idol’ before she boils my rabbit,” alisema Tyler, ambaye alikuwa jaji wa msimu wa 10 na wa 11 wa shindano hilo.
Mwanzilishi wa “Idol” Simon Fuller amesema show hiyo itammiss Tyler, lakini akasema anaelewa hitaji lake la kurejea katika maisha yake ya muziki kwenye bendi yake, Aerosmith.
Fox bado haijatangaza kuhusu mustakabali wa majaji wengine wa “Idol” Jennifer Lopez na Randy Jackson, ambao wote wanadaiwa kuwa kwenye mazungumzo ya mkataba.
Hata hivyo jana J. Lo alihojiwa kwenye kipindi cha Today cha NBC na kusema bado hajaamua kama ataendelea na msimu wa tatu ama ataitosa pia ingawa ameonesha nia ya kuondoka.
“I’ve just enjoyed it so much. But I am thinking that maybe it’s time for me to go and do other things that I really love to do… but then again, I really love the show!” alisema Jennifer.
“Ujue, Nilisaini na American Idol kuwa jaji kwa mwaka mmoja… Nikajikuta nikifanya miaka miwili. Na sasa ni kama vile, ‘OK, tunaendelea na safari hii?’ Nimeipenda sana. Nainjoy show sana. Lakini nahitaji kusema kwamba kuna mambo mengi mengine ninayofanya na nimeyaacha kwaajili hiyo. Mwisho wa siku, njia yoyote, ni uamuzi wa kuvunja moyo kama nikiondoka.”

source:bongo5