Wiki hii aliyekuwa naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa Dr.Asha Rose Migiro amerejea nchini baada ya kuutumikia kwa miaka mitano.
Hata hivyo shirika la habari la Vox Media limebaini sababu za kwanini Dr. Migiro hakuongezewa muda wa kufanya kazi kwenye umoja huo.
Limesema vyanzo vya ndani ya UN vimesnitch kuwa utendaji dhaifu na kushindwa kufit kwenye chombo hicho kigumu ni baadhi ya sababu ya kushindwa kuongezewa mkataba wa kufanya kazi humo.
“Nafasi ya Unaibu katibu mkuu ni ngumu mno; inahitaji mtu mzoefu kuongoza vema Secretariat. Changamoto yake kubwa ilikuwa ni kuelewa siasa katika chombo hicho cha kimataifa na kuunda muungano,” chanzo kimoja kiliiambia Vox Media.
Inadaiwa kuwa Dr. Migiro alizungumza na kundi la waafrika lenye asilimia 28 ya wajumbe wa umoja wa mataifa ili achaguliwe tena lakini walimtosa.
“Hakuwa maarufu miongoni wa wanadiplomasia. Hakuna aliyemsikiliza. Unaweza kukumbuka pia kuwa uteuzi wake ulikosolewa sana,” kilisema chanzo hicho.
Katika hatua nyingine Dr. Migiro alisema hana mpango wa kuwania urais wa Tanzania na huenda akarejea kwenye kazi yake ya zamani ya uhadhiri wa chuo kikuu.