Baada ya Madaktari kutoa taarifa kwamba wataandamana, Kamanda wa polisi Kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova amesema “mtu yeyote atakaejaribu iwe ni baraza la habari la kiislamu au hawa MAT (Madaktari) wasijaribu kufanya hayo maandamano kwa sababu hatuwezi kuruhusu makosa yatendeke”Ameamplfy zaidi kwamba “natoa onyo kali wasiandamane kwa sababu maandamano hayo ni batili hayana msingi wowote lakini tunaruhusu wakutane wakae kwenye ukumbi waite waandishi wa habari, kwa kuita waandishi wa habari na kukaa sehemu moja inatosha kabisa ujumbe wao kufika hilo linaruhusiwa lakini swala la maandamano halina sababu kwa sababu ujumbe ni ule ule”

source:millardayo