Baada ya Nigeria kufululiza miaka mitatu kwa kutoa mshindi wa Big Brother Africa, hatimaye jana utemi huo umefikia tamati baada ya mshiriki pekee wa Nigeria aliyekuwa amesalia kutoka.
Goldie ambaye kwa mshangao wa watu wengi alikuwa amepewa nafasi kubwa ya kushinda kutoka na umaarufu wake, alitolewa jana.
Wiki iliyopita washiriki waliokuwa wamewekwa kwenye kikaango ni Lady May, Kyle, Prezzo na Goldie ambao kwa pamoja walikuwa wamepewa jina la PreGo. Lady May na Kyle waliokolewa na wapiga kura wa Africa.
Baada ya Goldie kutangazwa kuwa ameyaaga mashindano hayo, aliondoka kwenye jumba hilo kimya baada ya kumkumbatia kinyonge mpenzi wake Prezzo ambaye amebaki kuendelea kuwania kitita cha dola laki tatu.
Kuondoka kwa Goldie kwa mara nyingine tena kunaongeza nafasi ya ushindi kwa ‘Masai Warrior’ Prezzo ambaye Kenya na Tanzania zimeendelea kupiga kura kwa wingi kuhakikisha anaendelea kubaki mjengoni.
Hivi ndivyo Africa ilivyopiga kura wiki (15 July 2012)
Angola: Prezzo
Botswana: Lady May
Ghana: Kyle
Kenya: Prezzo
Liberia: Prezzo
Malawi: Kyle
Namibia: Lady May
Nigeria: Goldie
South Africa: Kyle
Sierra Leone: Kyle
Tanzania: Prezzo
Uganda: Kyle
Zambia: Kyle
Zimbabwe: Lady May
Rest of Africa: Goldie

source:bongo5