Upendo wa Beyonce Knowles kwa Michelle Obama unaendelea kuimarika zaidi na sasa anataka kuona kuwa first lady huyo anarudi tena ikulu kwa huhakikisha Barack Obama anashinda uchaguzi.
Mwezi uliopita alipost barua ya shukrani kwenye website yake kumueleza ni kwa namna gani anavutiwa naye kwakuwa mama, mke na first lady bora.
Ili kuonesha kuwa Beyonce ni ‘TeamObama’ na kumpa support rais huyo aweze kuchaguliwa tena, ametengeneza video ambayo inamwonesha akiongelea kuhusu barua aliyomwaandikia Michelle.
Kwenye video hiyo Beyonce anaelezea:
“Niliandika barua kwa First Lady kwasababu nilitaka ajue kwamba ninamshukuru sana kwa kila kitu anachokifanya kwaajili ya nchi yetu na wanawake duniani.”
Kwa kuongezea zaidi tofauti na maelezo aliyoyaandika kwenye barua yake, Beyonce alisema, namheshimu sana Michelle Obama. Kila muda nikimuona, huvutia, hunipa nguvu ya kuishi maisha yenye afya na kusaidia wazee.”