Hatimaye baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kusikika redioni mashabiki wa Fina Mambo wana uhakika wa kuanza kuisikia tena sauti yake tamu.
Mtangazaji huyo wa zamani wa kipindi cha Power BreakFast cha Clouds FM, amehamia Magic Fm.
Akiwa Magic Fm, Fina Mango atakuwa akiendesha kipindi cha kila Jumamosi kuanzia saa 9.00 alasiri – 12 jioni.
Kipindi hicho kiitwacho ‘Makutano’ kitaruka kwa mara ya kwanza tarehe 4 mwezi ujao (August).
“My first radio crush is making a comeback…all the best @Fina_Mango cant wait to hear you again on air,” aliandika shabiki wake wa zamani aitwaye Lijocha.
Apparently, Fina Mango atafanya kipindi hicho kwa makubaliano maalum na sio kuajiriwa kwakuwa tayari ana kampuni lake liitwalo 1Plus Communications.