Mwanamuziki wa Uganda Maurice Kirya huenda akafanya kazi na mwanadada wa Kenya aishie nchini Norway, Stella Mwangi aka STL.
Mazungumzo ya mastaa hao wawili yalianzia pale ambapo Mauric Kirya alipomuomba STL kuangalia utaratibu wa kwenda kufanya show nchini Uganda ambako ana mashabiki wengi.
“Would be nice for you to do a gig here in UG! wacha think?” Maurice Kirya alimueleza STL.
Stella Mwangi ambaye kwa sasa yupo nchini Kenya baada ya kurudi mwezi uliopita na kufanya video kadhaa, alijibu,”Sounds like a good idea.”
Maurice hakusita kuelezea hamu yake ya kufanya ngoma na rapper huyo ambaye kwa sasa anatamba na kibao ‘Bad As I Wanna BE’ kwa kumwambia,”Perhaps we could rock a track together!”
“Fo sho! Lets make it happen #BadAsIwannaBe,” alijibu STL.
Mwezi uliopita Maurice Kirya alipata fursa ya kutumbuiza nyimbo zake “Misubbaawa” and “Dont Wanna Fight” kwenye stage ya Big Brother Africa.

source:bongo5