Rapper The Game amepitia mengi ya hatari kama kupigana mtaani, kufungwa jela, kupigwa risasi na sasa yote hayo yanaweza kuonekana kwenye reality show yake itakayoonesha hadi pale atakapomuoa mpenzi wake wa siku nyingi Tiffany Cambridge.
Reality show hiyo inayotayarishwa na kampuni ya 51 Minds Entertainment itaonesha upande mwingine mpya wa rapper huyo.
Mtandao wa TMZ umesema kuwa katika show hiyo Game ataonekana jinsi anavyoijali familia yake na masuala mengine yahusuyo mipango ya ndoa..
Utayarishaji wa show hiyo ulianza mapema mwezi huu na tayari mazungumzo ya kuirusha show hiyo kwenye vituo vya runinga vya MTV na VH1 yameshafanyika.