Stiker wa Napoli Edinson Cavani amesema kama Club ya Chelsea inamtaka itabidi imlipe mshahara mkubwa kama wanavyolipwa wachezaji wengine wakubwa ambapo mkali huyu mwenye umri wa miaka 25 anapewa nafasi ya kuchukua namba ya Drogba na atakubali kusain kama Chelsea watakubali kumlipa bilioni 770 za Kitanzania.

Gazeti la Uingereza la Daily Mail, Cavani anataka alipwe mshahara unaofanana na John Terry, Lampard na Torres ambao wote wanachukua zaidi ya pound laki moja na nusu kwa wiki ambayo ni zaidi ya bilioni 3 na nusu kwa noti ya kibongo.

Cavani amekua akihusishwa kuhamia Chelsea for some time, kama haufahamu, nakupa hii kwamba Cavani kwenye msimu uliopita wakati akiichezea Napoli, alifunga magoli 94 ndani ya mechi 66 ndio maana inaaminika kwamba anaweza kuliziba pengo la Drogba vizuri, hiyo hapo chini ni video ya magoli ambayo Edinson amewahi kufunga.