Baada ya stori kuandikwa kwenye magazeti kwamba Staa Diamond Platnums anadaiwa kumtelekeza baba yake na hamjali wala hataki kusikia stori zake, hii ndio kauli ya Diamond kuhusu hiyo ishu.

Amesema “kiukweli ni vitu ambavyo mimi vimenishangaza sana kwa sababu sijui chochote nakuja kukuta tu kwenye magazeti, na nisingependa nisikie swala la mzazi wangu kusema mimi ni mtoto wake sijui nini na nini kwamba mimi nafanya starehe sihusiki na yeye sio kauli nzuri kiukweli, ina maana ananijua kwamba mimi ni mwanae baada ya kuwa DIAMOND”

Kwenye line nyingine Diamond amesema “siku zote kama alijua mimi ni mtoto wake basi angenisomesha na kunipa elimu nzuri lakini siku zote nilihangaika na Mama yangu mzazi akanikuza na kunisomesha kwa shida na tabu zote mpaka leo nimekua hivi, nisingependa kumsikia mtu yeyote anaongea kwamba mimi ni mtoto wake au yeye ni nani kwa sababu siku zote hawakuonekana, wasitake kuonekana kipindi cha Maslahi mtu ndio anajifanya anahusika sana na mimi kama mtoto wake”

“Haya mambo nilianza kuyasema toka natoa single ya binaadam sikujua hata kama leo ningekuja kuwa na Prado, makazi au kuwa na haya mafanikio mengine, baba yangu ataendelea kuwa baba yangu tu ila siwezi kumpa kipaumbele kama ninachompa mama yangu kwa sababu kama angetaka hilo angenijali toka mapema” – DIAMOND.

Kwa kumalizia, Diamond ambae mpaka sasa ametumia zaidi ya milioni 69 kujenga Nyumba yake Tegeta Dar es salaam amesema “mimi nilikua napenda kusoma na nilikua nafanya vizuri kwenye masomo yangu lakini sikua na uwezo wa kifedha kuendelea kusoma, mzazi wangu alikua na pesa ina maana angenijua mimi angenisomesha leo ningekuja kuwa hata mbunge au hata waziri kwa sababu mi najua nina upeo mkubwa sana wa kielimu na vitu vingine, sasa nimesota na muziki alafu leo ndio wanajitokeza, SITAKI WANIACHE NA MAMA YANGU MZAZI”