Siku zikiwa zinahesabika ili msanii Mfalme wa Rymes Afande selle kutangaza chama atakachogombea nacho Ubunge 2015 Morogoro Mjini, mkongwe huyu amekubali kuwataja wanasiasa ambao ndio wanamvutia, wanampa hamu na ushawishi wa hiyo kazi kutokana na wanayoyafanya.

Afande anaesema anayajua machungu ya wanamoro amekiri kwamba wanaomvutia kwenye siasa ni wengi lakini wachache wao sana sana ni Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Halima Mdee wa Kawe na Burhani wa Lindi.

Amesema “mtu kama Zitto Kabwe ni mtu ambae ananipigia simu mara nyingi nikiwa na masahibu yangu ananishauri, namuheshimu sana na nafasi hii naitumia kumshukuru, yuko dada Halima Mdee wananionyesha kitu flani ambacho ninaweza kukifanya vilevile, kuna wabunge vijana kama Baruani kutoka Lindi japo ni Albino lakini ameonyesha kwamba Albino anaweza kuwa kiongozi mzuri kuliko hata watu wasio na ulemavu, wako wengi wananivutia hasa kutoka vyama vya upinzani”

Kwenye interview yake ya May 2012 na AMPLIFAYA, Afande alisema kuna vyama saba vya kisiasa vilivyomuita ajiunge navyo kugombea Ubunge lakini viwili ndio vyenye nafasi kubwa, kimoja kati ya CHADEMA au C.U.F

Alisema “kimsingi ndio vyama ambavyo hata namna ya kuvionganisha ningetamani siku moja viwe na sera moja na kuungana kuipigania nchi hii kwa sababu siamini kama kimoja bila kingine kati ya hivyo viwili kinaweza kuliangusha hili dudu kubwa ambalo lipo madarakani”

source:millardayo