Stori kutoka kwenye bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania July 26 2012 ni kuhusu Swali alilouliza Mbunge wa Iringa mjini Mch. Peter Msigwa kwa Waziri mkuu Mizengo Pinda.

Swali la Mchungaji lilitokana na taarifa kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetoa tamko kuwachukulia hatua wananchi watakaoonekana wanakula mchana au kuvaa nguo fupi wakati wa mfungo wa Ramadhani.
Mch Msigwa alimuuliza Waziri mkuu “Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania nimesema haina dini, je ni wakati muafaka kwa Serikali yako kutangaza sasa kwamba upande mmoja wa Muungano una fuata sheria za kidini na upande mwingine wa Muungano hauna dini?

Kauli aliyoitoa Waziri mkuu kumjibu mchungaji Msigwa ni hii…. “Nasema hili kwa maana ya mazingira ya Zanzibar, ukienda Zanzibar tungechukua tu takwimu za jumla jumla unaweza ukaona kabisa karibu asilimia 99 hivi ni Waislamu, sasa ndio maana nasema kwa mazingira ya Zanzibar viko vitu ambavyo vinaweza vikafanyika na mimi nadhani kwa sehemu kubwa atakua alipima vilevile mazingira, usilifanye likawa jambo kuuuubwa, angekua anazungumza kwamba serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ofcourse ingekua tofauti”