Home

WAJANJA WA BUSH WAMLIZA TIMBULO DOLA 800

Leave a comment


Nyota wa muziki wa kizazi kipya Bongo, ALLY Timbulo ‘Timbulo’ amepatwa na tukio la aina yake baada ya wajanja wa Bush kumliza kamera kubwa aina ya sonny wakati wa paty maalumu aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita kijijini kwao Riuwa, Wilayani Mbalali jijini Mbeya.

Akizunguma na Teentz mapema leo Timbulo amesema kuwa aligundua kupotea ghafla kwa kamera yake hiyo mara baada ya kumalizika kwa paty hiyo iliyokuwa imechangamka kupita kiasi huku vijana wengi aliokuwa wamefurika wakiwa hoi kwa mitungi.
“Nilipomaliza kuimba nikawa nimechili sehemu napumzika, lakini baada ya party kuisha nianza kukusanya vitu vyangu na baadae nikagundua kuwa kamera yangu haipo, kwa kweli nilichanganyikiwa kwa kuwa bado ni mpya kabisa na niliinunua kiasi cha dola 800 za Marekani” alisema Timbulo
Akiendelea zaidi timbulo amesema kuwa juhudi za kumsaka mtu aliyesepa na kamera hiyo ya kisa bado zinaendelea kwa kuwa sehemu kubwa ya watu waliofika siku hiyo wanafahamiana hivyo anaamini ndani ya siku chache zijazo atakuwa ameipata.
katika shoo hiyo Timbulo amerifu kuwa jukwaa alilokuwa analitumia kuwaburudisha mashabiki wake lilishindwa kuhimili vishondo na kuvunjika kufuatia watu kushindwa kuvumilia na kupanda juu alipokuwa yeye na hatimaye jukwaa hilo likasalimu amri.
“Hakika ilikuwa siku mbaya kwani kuna mambo mengi yalijitokeza ikiwamo shughuli yangu kucheleweshwa baada ya mchana na kuwa ucku kutokana na mtendaji wa kata kuzuia mpaka diwani alipoingilia kati na kuniruhusu” alimaliza

source:teentz

Wolper: Kuna binti ananichokonoa

Leave a comment


Jack Wolper

MWIGIZAJI nyota katika tasnia ya filamu za Swahiliwood, Jacqueline Wolper, amedai kuna mtangazaji mmoja wa Bongo anayemchafua makusudi kwa kumzushia kashfa mbalimbali.

Alisema kuwa mtangazaji huyo wa kike, pia anajaribu kumtengenezea mazingira ya yeye kuingia katika ugomvi na wasanii wenzake wa kike.

Jack amesema hayo baada ya kuenea kwa uvumi kuwa amenyang’anywa gari aina BMW X 6 aliyopewa na mpenzi wake na amezuiwa kukata mitaa.

Anaeneza habari za uzushi ikiwa na kuhakikisha kuwa mimi ninakosa na wasanii wenzangu, kama hivi karibuni nikiwa kwenye sehemu za kupigia picha na rafiki zangu walinipigia simu wakinijulisha kuna habari zinatangazwa eti nimenyang’anywa gari,” alisema.

“Hizi ni habari za uongo mtupu. Si kweli, kwani gari lipo ndani nyumbani kwangu.”

Msanii huyo amedai kuwa anamiliki gari zaidi ya moja kwa hiyo hakuna mtu wa kumpangia atembelee gari gani, kwani katika taarifa hizo ilisemekana kuwa kuwa alikuwa akitembelea gari aina ya Noah.

source:mwanaspoti

Gari la Khadija Kopa la patikana

Leave a comment


Malkia Khadija Kopa

May 22 mwaka huu mwimbaji staa wa Taarab Khadija Kopa alitoa taarifa kwenye kipindi AMPLIFAYA kuwa gari lake aina ya Noah lililokua limelazwa sehemu ya kulaza magari kwa kulipia Mwananyamala Dar es salaam kuwa limeibiwa .

Wezi waliohusika hawakuliwasha wakati wa kuiba, waliliburuza hadi mbali kidogo ndio wakaliwasha hilo na magari mengine mawili likiwemo la msanii wa bongo fleva Dogo Hamidu ambae alilipata lake maeneo ya Mlimani City Dars es salaam zaidi ya wiki moja baadae.

Alichoniambia Khadija Kopa jana usiku ni kwamba gari lake limepatikana jana mchana, limekutwa moshi lilikua limeuzwa kwa mtu ambae nae baadae aliliweka rehani kwa mtu mwingine tu likawa limehifadhiwa.

Mpaka limepatikana tayari limetolewa rim zote na zimeuzwa kwa mtu mwingine, Jambazi anaedaiwa kuhusika na wizi wa magari yote kwa mujibu wa Khadija Kopa anaitwa Rinko alikamatwa juzi na magari yote yaliyoibwa matatu yalikua chini yake.

Kwenye sentensi nyingine Khadija kopa amekanusha stori zilizotangazwa mwanzoni mwa wiki iliyopita kwamba amemtungia wimbo mwizi huyo wa gari lake.

WATU 10 KATIKA AJALI IGAWILO MCHANA WA LEO

1 CommentAbiria mwingine wa basi amefariki dunia mara tu alipofikishwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya hivyo kufikisha idadi ya watu 10 ambapo wanaume ni 7 na wanawake 3. Gari la Abiria aina ya Coaster T188 AWE lililokuwa likitokea Mbeya Mjini kuelekea Kyela liliparamiwa na Lori aina ya Fuso T 658 ASN lililokuwa likitokea nchini Malawi, kufuatia mfumo wa breki za Lori hilo kushindwa kufanya kazi.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema Lori hilo lilikuwa likitokea njia ya Malawi kuja mjini Mbeya lilianza kuyumbayumba na kushindwa na wakati huo huo basi la Abiria lilikuwa likipandisha kwenda Kyela. Dereva wa basi la Abiria amefariki dunia papo hapo huku Kondakta wake akijeruhiwa. Majeruhi wamekimbizwa Hospitali ya Rufaa huku wawili hali zao zikiwa mbaya.

Maafisa wa Jeshi la Polisi wamethibitisha kutokea kwatukio hilo la kutisha

sourcejaizmelaleo.blogspot

%d bloggers like this: