Home

HUYU NDIO MUHUBIRI ALIETABIRI AJALI NYINGINE YA NDEGE.

Leave a comment


Muhubiri TB Joshua wa Nigeria ametabiri tena kwamba kuna ajali nyingine mbaya ya ndege itakayotokea siku za karibuni kwenye nchi hiyo. Amesema kama hiyo ajali ya ndege haitotokea basi wanasiasa tisa mpaka 12 wa Nigeria watapoteza maisha yao kwenye ajali nyingine ya ndege, na hiyo itatokea wakati wakiwa wanarudi kutoka kwenye mkutano. Yani wote watapoteza maisha kwenye ndege itakayokua imewabeba wakiwa kuanzia 9 mpaka 12 kwa sababu shetani ana mipango ya kuwashambulia wote kwenye ndege hiyo moja. Amesema ili kuepuka hiyo ajali ni lazima wanasiasa hao waepuke kupanda ndege moja.
Mtandao wa Naija umeuliza, kama kweli huyu ni mtumishi wa Mungu na anaweza kutabiri mambo mabaya tu kutokea kwenye nchi hiyo, kwa nini asitumie nguvu yake kuomba neema na Nigeria kuepushwa na hayo majanga?

Hii ndio ajali maba ya ndege iliyotokea June 4 mwaka huu na kuua zaidi ya watu 153.

source:millardayo

ALICHOSEMA CHEGE KUHUSU USALAMA WAKE BAADA YA KUPATA AJALI USIKU.

Leave a comment


Inawezekana stori ya msanii CHege wa TMK WANAUME FAMILY kupata ajali umeshaisikia mpaka sasa, lakini na uhakika haujasikia kingine alichozungumza exclusive na AMPLIFAYA, nilifanya nae interview jana usiku saa tano na dakika 17 akiwa hospitali ya Temeke.Siku zote kuna maeneo ambayo huwa tunaonywa kwamba hata kama tairi la gari yako likiisha upepo usisimame, Temeke pia ni sehemu hatari kwenye ishu kama hizo… mi siku moja usiku nilishawahi kukutana na jamaa wamevaa sare alafu wanasema wanatengeneza taa kumbe sio, ni wakabaji.Pamoja na kwamba Temeke inatajwa kutokua nzuri kiusalama hasa linapotokea swala la ajali, Gari la Chege halijaibiwa hata kitu kimoja lilipopata ajali hiyo jana saa nne usiku, sababu kubwa na pekee ambayo imemuokoa chege ni kwa sababu ni mtoto wa kiumeni, mtu wa watu, umaarufu pia umemsaidia.Chege amesema watu waliosogelea eneo la ajali baada tu ya ajali kutokea na watu kukusanyika, baada tu ya kujua ni yeye ndio kwanza walianza kulilinda gari.. hakuna chochote kilichoibiwa.

source:millardayo

HIZI NDIO KAULI ZA WEMA SEPETU, FRANCIS CHEKA NA MASANJA MKANDAMIZAJI KUHUSU KUWEKA MAJINA BADALA YA NAMBA KWENYE MAGARI YAO.

Leave a comment


Sote tunafaham kwamba Serikali imeruhusu watanzania wenye uwezo wa kulipa milioni tano kwa miaka mitatu ili kuweka majina kwenye magari yao badala ya namba za kawaida wafanye hivyo.
Kwa sababu kwa kiwango kikubwa kwenye nchi nyingine mastaa ndio huwa wanaandika majina yao kwenye magari, nimeanza kuwauliza mastaa kadhaa wa bongo.
Movie star Wema Sepetu amekua wa kwanza kulijibu swali langu kwa kusema “sitotaka kufanya hivyo, wale wanaotaka kuuza watafanya hivyo mi sio mtu wa kuuza bwana, tayari nina gari zaidi ya moja lakini sitopenda kufanya hivyo kwenye gari langu lolote, kwa nini kila mtu nikipita aone Wema yule pale….? napenda magari yangu jinsi yalivyo na namba hizo hizo zinatosha.Bondia Francis Cheka amesema “naweza kufanya hivyo kwa sababu jina langu ni jina ambalo watu wengi wanalifahamu na ni rahisi kufanya hivyo, ni kitu kizuri”
Mchekeshaji Masanja Mkandamizaji wa Orijino Komedi amesema “kama ulimuhoji staa akasema ataandika lile jina kwenye gari yake yani huyo ni anaiga tu tuliotakiwa kufanya hivyo ni sisi tuliookoka kwa sababu kwenye biblia tunaambiwa vyovyote Mungu anavyokubariki simama kutoa ushuhuda, mimi niko tayari kufanya hivyo hata sasa hivi kwa sababu Account zangu, si unaona ndugu Millard nikitembea hivi pochi imetuna, sio imetuna pesa… ni kadi za benki”

Hili ni gari la mwanasoka Mkenya Mariga.

Hili ni gari la Jose Chameleone wa Uganda, magari yake yote kayaandika DOCTOR kwenye namba.

source:millardayo

Campmulla waomba kura kwenye Artist Of The Week ya MTV

Leave a comment


Kila wiki kituo cha MTV huwa na segment ya msanii bora wa wiki ambaye hupigiwa kura na watamazamaji.
Mpango huo uliowekwa na kituo hicho kwaajili ya kupromote wasanii wapya unaitwa MTV Iggy.
Kundi litakalopata kura nyingi zaidi litapewa shavu kwenye mtandao wa MTVIggy.com wiki hii pamoja na interview ndefu ( tell-all interview)
Wiki hii kundi la hip hop la nchini Kenya, Campmulla ni miongoni mwa wasanii/kundi lilitojwa kupigiwa kura.
Wasanii wengine ni pamoja na Leo Justi kutoka Brazil, Mario & Vidis wa Lithuania, Young Empires wa Canada na Fallulah wa Denmark.
Mpaka sasa Campmulla wanaongoza kwenye kura hizo.

Wasanii waige mfano wa website ya Diamond

Leave a comment


Katika jambo ambalo wabongo wanasema Diamond kapiga bao ni kuanzisha website yake mwenyewe. Website hiyo iitwayo Thisisdiomond.com imegeuka maarufu kwa mashabiki wake wanaotaka kujua yale ayafanyayo na waandishi wa habari wanaotaka kupata habari zake.
Tofauti na website za wasanii wengine nchini, yake Diamond tunathubutu kusema ndio personal website pekee inayoongoza kwa kuwa updated kila siku kwa matukio mapya. Diamond si mwandishi wa habari lakini anajua kuwa yeye ni mtengeneza habari (newsmaker). Katika uandishi wa habari yeye yupo kwenye ule ubora wa habari (news values) ambao kitaaluma unajulikana kama ‘Prominence’.
Yeye ni mtu maarufu kwahiyo chochote anachokisema ama kukiandika sehemu ni habari kwakuwa ni mtu maarufu. Hivyo ana mengi anayoyaandika kwenye website yake yanayotokana na kile akifanyacho kila siku, bila kusahau picha nzuri na nyingi ambazo huziweka mara kwa mara awapo kwenye ziara zake.
Hakuna show anayoenda na asichukue picha za kuja kuwaonesha mashabiki wake. Hakosi la kuandika kuwajuza mashabiki.
Kwanini tunasema wasanii wengine waige mfano wa website yake? Kwanza wasanii wachache ambao wana website ama blog zao wakumbuke kigezo hicho kuhusu ubora wa habari kuwa wao ni ‘newsworthy’ yaani wanatengeneza habari kwa mengi wanayosema ama kufanya.
Ni jambo la ajabu website ya msanii mkubwa inakuwa updated mara moja kwa mwezi tena kwa habari ya ajabu ajabu tu na wakati mwingine haimhusu yeye mwenyewe! Personal websites/blogs zinapaswa kutoa kwa asilimia kubwa habari kuhusu msanii mwenyewe.

Wasanii wengine wamezigeuza personal blogs zao kama blogs zingine za kawaida zinazotoa habari za watu wengine. Diamond anapaswa kusifiwa kwasababu website yake inamuangaza yeye zaidi. Wapi ameenda kufanya show, amekutana na nani, ana mipango gani n.k.
Ukiwa mtembeleaji mzuri wa website yake utayafahamu hayo. Iweje website binafsi ya msanii mkubwa nchini ijae mambo ya watu wengine tu wakati yeye mwenyewe kila siku kuna mambo anayoyafanya na ambayo kama angeyaandika kwa kuambatanisha na picha mashabiki wake wangefurahia!!
Hivyo wasanii wanaomiliki website/blog binafsi watambue kuwa sio fashion kuwa na website ambayo hubadilishwa habari mara moja ama mbili kwa mwezi. Huna haja ya kuwa na website binafsi wakati huna la kuandika. Inabaki kuwepo tu bila kitu chenye kumrudisha tena msomaji.
Kwa wale ambao hawana website/blog zao ni muda mzuri wa kufikiria kuwa nazo. Ni njia nzuri ya kujitangaza. Waandishi wa habari huzitumia kupata habari halisi na zenye ushahidi kutoka kwa msanii husika. Kumiliki tu akaunti ya Facebook na Twitter hakutoshi.

source:bongo5

KIGOMA ALL STARS waingia mkoani KIGOMA kwa kishindo.

Leave a comment


Wasanii wale wa bongo fleva waliotokea Kigoma hivi sasa wapo jijini tayari kwa show yao ya tarehe 17/07/2012. Wasanii hao ni kama Linex, Abdu Kiba, Mwasiti, Recho, Banana Zoro, Diamond, Ommy Dimpoz, Queen Dlyn, Macomandor..etc..Show hiyo itakuwa free katika uwanja wa Lake Tanganyika…
Don’t miss..

source:djchoka.

MAGARI WALIYOZAWADIWA WACHEZAJI WAPYA WA MANCHESTER UNITED NDIO HAYA.

Leave a comment


Shinji Kagawa na Nick Powell

Mjapan Shinji Kagawa amezaliwa miaka 23 iliyopita na club yake ya mwisho kuichezea ni Borussia Dortmund na kaifungia magoli 21 kwa miaka miwili aliyokaa nayo na amezichezea timu za taifa toka mwaka 2006, Powell yeye ameichezea Crew Alexandra kwa miaka miwili na kuondoka na magoli yake 16, Timu za taifa za England amejiunga nazo toka 2009.

Waandishi wa habari walio hudhuria

source:millardayo

Older Entries Newer Entries

%d bloggers like this: