Home

BAADA YA Z ANTO KUACHANA NA HUYU BINTI, ASEMA YUKO TAYARI KUOA TENA.

Leave a comment


Z anto

Wote tunafahamu kwamba Z Anto star wa hits kama Binti Kiziwi na Mpenzi Jini, alioa akiwa na umri wa miaka 22 tu tena siku chache baada ya video ya Binti kiziwi ilipotoka ambapo alimuoa mrembo alieuza kwenye hiyo video. Walikaa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda wa mwaka mmoja na kuoana kwenye ndoa ambayo haikumaliza mwaka mmoja, ilivunjika Miaka mitatu iliyopita. Z Anto anasema “niliamua kumuoa kwa sababu pesa ninazo mali ninazo na nikawa sipendi kuendelea kutenda dhambi, lakini tuliachana kwa sababu ya tamaa zake za kibinaadamu”

Huyu ndio mrembo alieonekana kwenye video ya Binti Kiziwi ambae ndio Z Anto alimuoa na wakaachana baadae.

“Kwa sasa niko tayari kuoa tena manake dini yangu inanilazimisha mimi kuoa, nina mtu ambae bado sijamchumbia na kwa bahati nzuri nimebahatika kupata nae mtoto pia aliezaliwa miezi mitatu iliyopita, plan yangu ni lazima nioe maishani kwa sababu kosa la mtu mmoja haliwezi kunifanya niwaadhibu watu 100, yeye nilimuadhibu na nimeshasahau pia… wakati namuoa alikua na umri wa miaka 20 na mimi nilikua na kati ya 21 au 22″ – Z Anto

source:millardayo

WAFANYAKAZI WA MIGODINI WACHARUKA AFRIKA KUSINI, WAWATUHUMU VIONGOZI WA ‘NUM’ KUJAZA MATUMBO YAO.

Leave a comment


Wakiongozwa na Chres Manyaka, wafanyakazi wenye hasira kali wakiandamana dhidi ya viongozi wanao jinufaisha kutokana na jasho la wafanyakazi wachini migodini.
Wakiwa nje ya Mgodi wafanyakazi waliwaonyesha waandishi nakala za mishahara “salary slip” ikiweka wazi mshahara wa randi 3,746.78 sawa na dola 460 kwa mwezi. Na baada ya makato mfanyakazi huchukua randi 2,659.26 sawa na dola 330 kwa mwezi.
Kiongozi wa chama cha PTAWU Reckson Baloyi, amesema Wafanyakazi wamesisitiza kutatuliwa matatizo yao na hawataki kusikia siasa.

MSANIFU MAARUFU WA MAGARI YA FERRARI ITALI PININFARINA AFARIKI.

Leave a comment


Msanifu maarufu wa utengenezaji wa magari ikiwemo miundo ya Ferrari na Fiat Sergio Pininfarina (pichani) wa nchini Italia amefariki dunia nyumbani kwake katika mji wa Turin baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Pininfarina alisanifu miundo maarufu ya magari ikiwa ni pamoja na Ferrari, Fiat na Maseratis na pia magari aina ya Peugeot na Mitsubishi.
Sergio Pininfarina pia alikuwa mbunge wa bunge la Ulaya hadi mwaka wa 1988 na baadaye kukiongoza Chama cha Wafanyabiashara wa Italia.
Waziri Mkuu wa Italia Mario Monti amesema kuwa Pininfarina alizaliwa na kipaji cha kuleta pamoja uzuri na ubora katika kazi yake.
Sergio Pininfarina alizaliwa katika mji wa viwanda wa Turin Kaskazini mwa Italia na amefariki akiwa na umri wa miaka 85.

Ziara ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Washington DC

Leave a comment


Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wameanza ziara ya siku mbili Washington DC, kuanzia tarehe 2 – 4 Julai 2012. Pichani, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Lowassa (Mb.) akiweka saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwneye ubalozi wa Tanzania Washington DC.

Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Lilly Munanka akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Lowassa (Mb.) kwenye ofisi za ubalozi

Kaimu Balozi wa Tanzania Mhe. Lilly Munanka akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama walioanza ziara ya siku mbili Washington DC

Baadhi ya wafanyakazi wa ubalozi wakipata picha ya pamoja na wajumbe wa kamati hiyo

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Lowassa (Mb.)akifuatilia taarifa kutoka Ubalozi wa Tanzania Moscow, kutoka kwa mjumbe wa kamati hiyo Mhe. Vita Kawawa aliyejumuika na msafara huo akitokea Moscow.

source:father kidevu

Hali ya Dkt Ulimboka yaendelea vyema

Leave a commentHali ya afya ya Dkt. Steven Ulimboka ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania, inaendelea vyema baada ya kushambuliwa na watu wasiofahamika usiku wa kuamkia jana jijini Dar es Salaam.
Dkt. Ulimboka aliokotwa jana akiwa hajiwezi na mwili ukiwa na majeraha mengi baada ya kupigwa na watu hao na baade kufikishwa Hospitali ya taifa Muhimbili na wasamaria wema.
Ulimboka anaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhumbili kitengo cha mifupa MOI aliko lazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) huku jopo la madaktari Bingwa wakiendelea kumnusuru.

source:fatherkidevu

Kanumba apelekwa sabasaba

Leave a comment


FAMILIA ya msanii wa filamu za Swahiliwood, Steven Kanumba, imeamua kuuza bidhaa za marehemu katika uwanja wa maonyesho wa Sabasaba uliopo Temeke katika kujenga utaratibu wa kumbukumbu dhidi yake.

Bidhaa za marehemu Kanumba kama aina ya nguo alizokuwa akipenda kuvaa, filamu alizowahi kuigiza, picha zake zitaonyeshwa katika maonyesho ya Sabasaba mwaka huu, familia ya marehemu imechukua banda kwa ajili ya maonyesho hayo ambayo yatakuwa ya aina yake kufanyika katika uwanja huo, anasema Magulu.

Katika banda hilo pamoja na kuona bidhaa za msanii huyo lakini pia kwa wale watakaolitembelea, watapata fursa ya kuongea na wanafamilia kama Seth Bosco mdogo wa marehemu aliyekuwa naye karibu sana, Mama yake mzazi, wafanyakazi wa kampuni yake.

Alisema hiyo itakuwa fursa nzuri kwa watakaotaka kujua mengi yamhusuyo Kanumba.

Kanumba alifariki miezi miwili iliyopita katika kifo kilichojaa utata huku msanii mwingine, Elizabeth Michale ‘Lulu’ akikabiliwa na kesi inayomtuhumu kuhusika na kifo hicho kilichotokea mara baada ya wawili hao kuzozana chumbani kwa Kanumba.

Utabiri TB Joshua Matatani

Leave a comment


Bingu Wa Mutharika


Chama tawala cha zamani cha nchini Malawi, DPP, kinashinikiza ufanyike uchunguzi dhidi ya mhubiri maarufu wa Nigeria, TB Joshua kutokana na kifo cha rafiki yake rais wa zamani wa Malawi, Bingu wa Mutharika.

TB Joshua


Katika ripoti iliyoandikwa kwenye gazeti la Nyasa Times, rais Joyce Banda alitangaza kufanyika kwa uchunguzi kuhusiana na kifo chenye mzozo cha kiongozi huyo wa zamani April 5, yakiwemo matibabu aliyoyapata.
TB Joshua alitabiri kifo cha Mutharika huku rais huyo mpya wa Malawi akiwa pia mtu wa karibu wa ‘nabii’ huyo kama ajiitavyo.
Msemaji wa chama cha DPP Nicholas Dausi, amesisitiza kuwa TB Joshua anatakiwa aulizwe maswali. Kifo cha ghafla cha Mutharika April 5 kilitokea miezi miwili kabla ya tarehe hii ambapo TB Joshua alisema rais wa Afrika atakufa baada ama ndani ya miezi miwili.

“Lazima tujue ni jinsi gani huwa anatabiri mambo” Dausi ambaye ni mbunge wa Mwanza Central aliliambia bunge la Malawi.
Dausi alitoa wito wakati akichangia bajeti ya nchi hiyo kuwa wananchi wa Malawi wapuuzie tambo za baadhi ya TV kama Emmanuel TV na TB Joshua kuwa walijua kutatokea kifo cha Mutharika.

source:bongo5

Older Entries

%d bloggers like this: