Home

ALICHOKIANDIKA JOSE CHAMELEONE KUHUSU ERICK SHIGONGO KUENDELEA KUISHIKILIA PASSPORT YAKE.

Leave a comment


Kama kumbukumbu zako zipo fresh, muda mfupi baada ya Jose Chameleone kumaliza show yake Uwanja wa taifa July 7 2012 na kufanya kama walivyokubaliana kwenye mkataba, siku mbili baadae stori gazetini ziliandikwa kwamba mwimbaji huyu staa wa Uganda ameshindwa kurudi kwao kutokana na Passport yake ya kusafiria kushikiliwa na Eric Shigongo C.E.O wa Global Publishers walioandaa show hiyo kutokana na kumdai pesa ambazo ilidaiwa alishawahi kulipwa kipindi cha nyuma kuja kufanya show Tanzania lakini hakutokea.
Pamoja na hati yake ya kusafiria kuzuiliwa na Erick Shigongo, aliweza kusafiri kurudi kwao… sasa baada ya kuwa kimya kidogo…… hiki ndicho alichoandika kwenye ukurasa wake wa facebook kuhusu hiyo ishu.
Kwa ufupi ni kwamba Jose Chameleone amemlalamikia Big Boss Erick Shigongo kuhusu kuendelea kuishikilia Passport yake wakati meneja wake Chemeleone hakuhusika kuchukua hizo dola za Kimarekani 3500 zinazodaiwa kupokelewa na Meneja wa Chameleone kwa ajili ya show iliyopangwa siku nyingi kidogo.
Chameleone amesema aliporudi Uganda alifanikiwa kumkamata na kumpeleka polisi George, mtu ambae ndio anadaiwa kuzichukua hizo pesa akijidai ni meneja wa Chameleone lakini baadae akaachiwa huru ambapo baada ya kuona hivyo ilibidi Chemeleone aende kwa balozi wa Tanzania Uganda ili kupata msaada lakini hakufanikiwa.
Amesema wakati passport yake ilipozuiliwa na Erick Shigongo alikwenda kwenye ubalozi wa Uganda Tanzania na ndio uliomsaidia kumpa Document zilizomuwezesha kurudi nyumbani, kwa sasa amepata mialiko ya shows South Africa, England, Belgium, Norway, Sweeden, Canada n.k lakini hajui itakuaje na anahitaji ushauri kuhusu Erick Shigongo ambae ameshikilia Passport yake kwa zaidi ya mwezi mmoja.

source:millardayo

Leave a comment


Kindly visit this link of ChannelOTV and support New Tanzania Rapper-JanB by a THUMB ”LIKE” and SHARE this link to your BLOGS, WEBSITE, SOCIAL NETWORKS like twitter and facebook to let the public know about Tanzania Talents doing music in international level. Here is the link: http://channelo.dstv.com/2012/07/new-music-video-pretty-girl-2/

Thomas Ulimwengu anusurika kifo katika ajali ya ndege

Leave a comment


MSHAMBULIAJI nyota wa TP Mazembe, Thomas Ulimwengu jana alinusurika kifo katika ajali ya ndege iliyotokea nchini DR Congo.
Ulimwengu raia wa Tanzania anayekipiga TP Mazembe alinusurika katika ajali hiyo akiwa katika ndege iliyokuwa inajaribu kuruka lakini ikashindwa.
Kutokana na kushindwa kupaa, ndege hiyo iliacha njia na kuingia vichakani, Ulimwengu akiwa ndani pamoja na wachezaji wengine 15 wa TP Mazembe na timu ya benchi la ufundi.
Taarifa za ajali hiyo jana zilipatikana saa 8 mchana kupitia katika ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Facebook wa Ulimwengu ambaye aliweka maneno haya.
“Dakika chache zilizopita kungelewa mambo mengine, labda ningeitwa marehemu au ningekuwa hospitali. Niko ndani ya ndege mimi na wachezaji kama kumi na tano na viongozi na makocha. Ndege imeacha njia na kuingia vichakani, ni baada ya kushindwa kupaa. Mungu mkubwa.”
Baada ya maneno hayo ya Ulimwengu, watu kadhaa walikuwa wakimpa pole mfululizo huku wakimuombea afya njema.
Championi Ijumaa lilifanya juhudi kumpata ili aweze kufafanua maswali mengi kama ndege hiyo ilikuwa inatokea wapi kwenda wapi na kama alikuwa pamoja mchezaji Mtanzania Mbwana Samatta au la.

source:globalpublishers.

Fally na Mr. Flavour wafanya kazi Pamoja

Leave a comment


Mwanamuziki wa kizazi kipya cha lingala ya Congo, Fally Ipupa amezidi kuonesha ukaribu zaidi na wasanii wa Nigeria na kufanya nao ngoma.
Jana kupitia Facebook, alipost picha mbili akiwa kwenye ‘video shoot’ nchini Ufaransa na msanii wa Nigeria Flavour na kumaanisha kuwa wamefanya wimbo pamoja.
Wimbo huo mpya ni wa Flavour utakaokuwepo kwenye albam yake mpya.
Fally Ipupa amewahi pia kushirikishwa na Jay Martins katika remix ya wimbo wake uitwao Jukpa.
Jumamosi iliyopita, June 30, Flavour, kundi la Bracket na Dontom, walikuwa mjini Paris Ufaransa kwa mara yao ya kwanza na kutumbuiza mbele ye umati wa wapenzi wao wa muziki nchini humo.
Ziara hiyo ilimpa nafasi Flavour ya kumpata Fally Ipupa ambaye mara nyingi huwepo Paris na kufanya video yao jana.
Wasanii wa Afrika kutoka nchi zingine zisizozungumza kifaransa, wameanza kujipatia soko na umaarufu mkubwa nchini Ufaransa husasan wasanii wa Nigeria.
Mwezi March mwaka huu Flavour N’Abania alisaini mkataba na label kubwa ya muziki ya nchini Afrika Kusini iitwayo Sould Candi.
Mkataba huo ulifanikisha uuzwaji wa albam yake Uplifted, iliyokuwa na hit ‘Nwa Baby’ kuuzwa nchini Afrika Kusini.
Kwa upande wake Fally Ipupa, mwishoni mwa mwezi uliopita, aliungana na Ferre Gola mjini Paris kuimba wimbo wa kizalendo kwa nchi yao uitwao “Congo, my country.”
Wasanii wengine wa Congo walioshiriki kwenye wimbo huo ni Lokwa Kanza, Djessi Matador, Aimelia, Celeo Schramme na wengine ambapo jumla wapo wanamuziki 30.

Pipi – Proud Mama to be!!

Leave a comment


Mwanamuziki wa kike nchini Tanzania aliyewahi kutamba na wimbo ‘Njia Panda’, Doreen Aurelian Cassian Ponera aka Pipi, ameamua kuweka wazi furaha aliyonayo kwa kuwa mama mtarajiwa.
Pipi ambaye kwa sasa ana wimbo mpya uitwao ‘Unapokuwa mbali’ ameyaondoa mashaka waliyokuwa nayo baadhi ya watu walioiona video hiyo na kugundua kuwa kuna mabadiliko kwenye saizi ya tumbo lake na hivyo kuhisi kuwa tayari ni mjamzito.
Jana kupitia Facebook ameamua kuonesha live tumbo lake na kuwapa jibu wale walioukuwa na mashaka na hali yake ya sasa.
Kitendo chake cha kuwa wazi kiasi hicho na kujivunia kuwa mama mtarajiwa, kimesifiwa na watu wengi.
“It’s hard kwa wanawake wengi kudisclose their affairs especially pregnancy but umeweza, unastahili pongezi kwa kweli, kwanza kwa kukubali kuitunza mpaka hapo maana wengi hupendelea abortion,” aliandika mmoja wa rafiki zake.
Nasi pia baada ya kuona picha hizo tulimtupa pongezi kwa ujasiri huo kwa kumwambia, “Naona you are a proud mama to be! Hongera sana,” na yeye akajibu, “Hahaha, yes am very proud, thanks a lot!

source:bongo5.

Esther Wassira awashutumu madaktari kwa kifo cha uzembe cha mtoto wa rafiki yake

Leave a comment


Mwanamuziki wa zamani ambaye kwa sasa ni mwanasheria, Esther Wassira amewatupia shutuma nzito madaktari wa hospitali ya Amana ya jijini Dar es Salaam kwa kile alichokiita ‘uzembe’ wa makusudi uliosababisha kifo cha mtoto mchanga wa rafiki yake.
“Naenda pia kwenye msiba wa rafiki yangu amefiwa na mtoto wake wa siku moja,aliyefia hospitali Amana,baada ya Madaktari kuwachomolea watoto ishirini Oxygen na kuwaacha wakiteketea!!! Kweli jamani??? Doctors??? You can kill innocent infants??? Si mngewaachia hiyo oxygen tu mkaondoka??? Serikali!!! Do something jamani..! Just give them what they want!! Think of the loss..mama abebe mimba miezi tisa,mwanae auliwe?” Esther aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
“This is a catastrophe to the nation..hivi kweli!!!!, it is very serious..yupo kwa mama yake anakandwa tumbo na mwanae ameshamzika!!! This is BAD! Naogopa nchi yangu!!”
Hata hivyo shutuma hizo nzito dhidi ya madaktari wa Amana zilizotolewa na mwanadada huyo zilipokelewa kwa hisia tofauti kutoka kwa watu wengine.
“Pole na msiba huo..ila usiwe unakurupuka na kuleta uzushi kuwa madaktari wamewachomolea oxygen watoto..ukiambiwa thibitisha sijui utasemaje…u r a lawyer..think before u leap….usiwe kama layperson kukurupuka na kusema habari za uvumi….madaktari sio wajinga kama serikali yako kufanya kitu kama hicho kwa infants kama hao….kifo cha watoto ni kawaida tu..kama ingekuwa hakuna huu mgomo na kukatokea hilo sidhani kama ungesema hivyo Esther,” aliandika mtu mmoja aitwaye Pedro Juan.
“Pedro usinifrustrate!! I have enough frustrations!!! Ninakwambia am sitting with a woman hapa my friend ananiambia exactly what has happened wewe unaniambia uzushi!!! Ni heri ushtuke na uombe kuliko kunistress zaidi..do you think I want to accuse doctors au unadhani nafurahi kuona insensitivity ya government!! Am a human being,a woman for that matter!! Lawyer or not!!!,” alijibu Esther.
Mtu mwingine aitwaye Isaac Ruge Abraham alisema, “Nimeisoma hii post na kusikitika sana.Mimi na daktari kwa miaka 6 sasa na siamini kabisa kama kuna daktari anaweza kuchomolea watoto oxygen kwa madai yake.Kama amefanya hivyo ni kosa la jinai.Ila kama kuna mgomo na daktari hakwenda wodini kwa sababu kuna mgomo haya ni mambo mawili tofauti.
Kwa sasa mgomo umekamata pabaya maana hakuna hata emergencies zinazoguswa na ni kipindi kibaya sana kuumwa hata kama wewe ni daktari.Nadhani ni vibaya kutumia maelezo ya upande mmoja na kuyatumia kuweka presumptive judgement.
Esther Wasira mdogo wangu.Kwa kazi hii madaktari hujitoa mara zote wanapofanya kazi wakati mwingine bila kulala hadi masaa 36 na sidhani mtu anayejitoa kiasi hicho anaweza kufanya jambo kama ulilolielezea hapo.Wapo wazembe kwenye hii fani lakini hakuna wa kutenda hivi na kama yupo basi hafai kufanya fani hii.”
Kwa upande wake Esther aliongeza kwa kusema, “Isaac I do understand you brother..na wewe kama daktari umejibu vyema tena very objectively!! As you say,ni ngumu kuamini kuna daktari angekuwa mnyama kiasi hiki..what this lady was narrating on the incident ya mwanae,anasema,it was chaotic, they were many of them,charged into the room and switched them off,as a sign of “no more service guys”..!
Mimi nili-panic sana asubuhi..huyu mtu msibani anasema “cause of death” ni mwanangu kutolewa oxygen wakati akiwa Amana anaendelea na matibabu!! So as u say,it might be a presumptive judgment based on the testimony of the mother,but am not pronouncing anybody guilty!! I said earlier,if it gets to the level where the issue has been taken to the hands of the law and the accused tried,the state will declare their status,whether innocent or guilty!! Take this as a charge sheet,that’s the accusation,kinywa cha Mtanzania aliyepoteza mtoto wake ndio kimenena hayo!! So treat me as a spokesperson right now!!”
Mgomo wa madaktari nchini unaendelea kuchukua sura mpya kila kukicha,ambapo juzi Mwenyekiti wa Jumuiya ya madaktari nchini Dr. Stephen Ulimboka, alitekwa na watu wasiojulikana walimpiga kinyama. Kwa sasa bado amelazwa katika hospitali ya Muhimbili akiendelea kupewa matibabu.

source:bongo5

Hermy B awataka wasanii nchini kuwa na umoja ili kupata haki yao

Leave a comment


Producer na mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya B’Hits Music Group Limited, Hermes Tarimo aka Hermy B amesema kama wasanii nchini wakiunganisha nguvu pamoja na kupigania haki zao ni rahisi kufanikiwa.
Kupitia mtandao wa Facebook jana Hermy B amesema umoja ndio njia pekee itakayowasaidia wasanii hao kupigana na kupata wanachostahili. “Natamani kuishi na kuona wasanii wote Tanzania wanafanikiwa, namaanisha kila mtu anayevuja jasho kwa ajili ya tasnia hii anastahili tuzo kwa namna fulani na nahisi kufanikiwa ni sehemu ya hili,” aliandika.

“Inaniuma sana ninapoona baadhi yetu tunafanikiwa na wengine hawafanikiwi, naumia napoona vipaji halisi vikipuuziwa na kutopongezwa, naumia sana ninapoona watu walionyuma ya utengenezaji wa nyota halisi wakipuuziwa na pengine walikilipwa kiduchu na mambo mengine yakikuzwa bila sababu.”

“Lakini moyoni mwangi najua; katika kila vita baadhi watafika mwisho na wengine hawatafika. Umoja ni kitu pekee kitakachotusaidia sisi kushinda vita vyetu vingi, hivyo natamani wasanii wa Tanzania waunganishe nguvu pamoja na kupigania haki zao, kupigania kile tunachostahili na kwakweli kupigana kwaajili ya mafanikio.”

source:bongo5

Older Entries

%d bloggers like this: