Home

Mnyika Kuwa Shahidi Kesi Ya Mauaji

Leave a comment


MBUNGE wa jimbo la Ubungo, John Mnyika atakuwa ni mmoja wa mashahidi wa Serikali watakaoithibitishia mahakama namna walivyohusika washtakiwa wanaotuhumiwa kumuua Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Kata ya Ndago, Yohana Mpinga (30).

Jeshi la Polisi mkoani Singida, limemefikia azimio hilo baada ya kumhoji Mnyika kwa saa tatu juzi usiku, kuhusiana na tukio hilo la mauaji lililotokea baada ya mkutano wake wa hadhara uliofanyika Julai 14 mwaka huu, majira ya jioni.

Mahojiano hayo yaliyoanza saa 11.53 jioni na kumalizika saa 3:15 usiku, yaliendeshwa chini ya kikosi maalum cha askari wa upelelezi kutoka jijini Dar es Salaam kwenye ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoani hapa.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana zilithibitisha kwamba Jeshi la Polisi lilimtaka Mnyika awe tayari kuitwa wakati wowote ili kusaidia kwenye kesi hiyo ya mauaji.

Tayari watu 18 wametiwa mbaroni, miongoni wakiwemo wanachama wa Chadema, kwa tuhuma za kuhusika kwenye mauaji ya kijana huyo wa CCM.

Mnyika alihojiwa huku akiwa na wakili wa Chadema na mbunge wa jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Mauaji hayo ya mwenyekiti wa UVCCM yalifanyika Julai 14 mwaka huu saa 10 jioni huko katika kijiji cha Nguvumali kata ya Ndago jimbo la Iramba magharibi.

Mauaji hayo yanadaiwa kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na vurugu zilizotokea kwenye mkutano wa hadhara ambao Mnyika alikuwa mgeni rasmi.

Katika hatua nyingine, mshauri na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Kitila Mkumbo, ambaye alikuwa ameambatana na Mnyika, alitarajiwa pia kuhojiwa kuhusiana na mauaji hayo jana.
Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz

AJALI MBAYA YA BASI LA BUNDA IMETOKEA GEITA,WATU 11 WAFARIKI PAPO HAPO NA 12 WAJERUHIWA.

Leave a comment


MKUU wa mkoa wa Geita Magalula Said Magalula akiangalia miili ya marehemu waliokufa katika ajali ya Gari leo mchana Wilayani Geita,miili hiyo ilikuwa imelazwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya hiyo.Picha na David Azaria. (Source http://www.hakingowi.com/)

Watu wamefariki Dunia Papo hapo hapo na wengine 12 wakijeruhiwa vibaya baada ya magari matatu mawili kati yao yakiwa ni ya abiria waliyokuwa wakisafiria kupata ajali na kupinduka wilayani Geita Mkoani Geita.

Tukio hilo limetokea leo Jumapili majira ya saa 8:30 katika kijiji cha Chibingo kata ya Katoro eneo ambalo mwaka jana kulitokea ajali ya basi la Bunda na kuua watu 14 papo hapo na kujeruhi wengine 28.

Katika tukio hilo watu 9 wakiwemo watoto watatu wamekufa papo hapo,huku wengine wawili mmoja akifariki njiani wakati wa kukimbizwa hospitalini huku mwingine akifariki wakati akipatiwa matibabu na madaktari katika chumba cha Upasuaji.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Geita Paul Kasabago amelithibitihishia gazeti hili kuwepo kwa tukio hilo,na kueleza kuwa ajali hiyo ni mbaya nay a kwanza kutokea katika kipindi cha mwaka huu huku akitaja magari yaliyopata ajali kuwa ni zenye namba T 344 AZE zote aina ya Toyota Corola,na T 421 BHS Toyota land Cruiser.

Aliwataja waliokufa papo hapo katika ajali hiyo kuwa ni Maria Elisante (18) mkazi wa Mganza wilayani Chato,Masasila Benjamin (17) mkazi wa Mkolani mjini Geita,James Ntungirwenge (36) Mkazi wa Nyankumbu Geita,na Eliud Ngovongo (36) pamoja na watoto wake watatu Amin (10),Emison(7),na Sara(4) wote wakazi wa Kalangalala mjini Geita.

Alisema bado majina ya marehemu watatu mpaka jioni ya jana yalikuwa bado hayajatambuliwa,huku akibainisha kwamba tayari marehemu saba kati ya 11 waliofariki wametambuliwa na ndugu zao.

Kamanda Kasabago alisema katika tukio hilo watu 12 wamejeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya wilaya ya Geita,huku wanne kati yao ambao hali zao ilionekana kuwa mbaya wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando kwa matibabu zaidi.

Mganga mkuu wa Wilaya ya Geita Dk.Abdalah Dihenga jana aliwaongoza madaktari wengine kutoa huduma kwa majeruhi,ambapo mwandishi wa Gazeti hili aliwashuhudia wakitoa huduma kwa wagonjwa katika chumba cha upasuaji hospitalini hapo.

Akisimulia tukio kamanda Kasabago alisema chanzo cha ajli hiyo mbaya ni mwendo kasi wa magari mawili madogo ya abiria yajulikanayo kwa jina la ‘Michomoko’ ambayo yaligongana uso kwa uso na gari linguine aina ya Land Cruiser.

Kamanda Kasabago alisema magari hayo mawili yalikuwa yakifukuzana kutoka mjini Geita kwenda Katika mji mdogo wa katoro huku yakiwa na abiria,ambapo baada ya kufika katika eneo hilomoja liliamua kulipita lingine na ghafla likakutana na gari linguine mbele.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Said Magalula alifika katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Geita,na kushuhudia miili ya marehemu iliyokuwa imelazwa chini katika chumba hicho.

Akizungumza na mamia ya wananchi waliokuwa wamefurika nje ya Viwanja vya jingo hilo la kuhifadhia maiti katika hopspitali ya wilaya hiyo Mkuu huyo wa Mkoa alitoa pole kwa wafiwa,na kuwataka kuwa na moyo wa subira wakati wa maombolezo ya vifo vya ndugu jamaa na marafiki zao.

source:dewjiblog.

Washington D.C:Polisi atishia kumuua Michelle Obama

Leave a comment


Afisa wa polisi wa jijini Washington D.C. anayehusika na kulinda maafisa wa ikulu ya White House nchini Marekani, amejikuta akipumzishwa kazi baada ya kudaiwa kutishia maisha ya First Lady, Michelle Obama.
Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post, ofisa huyo anafanya kazi ya escort ya pikipiki na anadaiwa kusema kuwa angempiga risasi First Lady huyo.
Inasemekana aliwaonesha polisi wenzake picha ya bunduki ambayo angeitumia kumuulia.
Hata hivyo idara ya polisi ya jijini Washington imesema haina maelezo mengi kuhusiana na tukio lakini msemaji wake Gwendolyn Crump amesema kwenye maelezo:
“We received an allegation that inappropriate comments were made. We are currently investigating the nature of those comments.”
Idara hiyo pia iliwasiliana na ‘Secret Service’ kuhusiana na kitisho hicho.
Msemaji wa Secret Service Ed Donovan amesema mamlaka hiyo inalifahamu tukio hilo na inachukua hatua zinazotakiwa kwa uchunguzi maalum.

source:bongo5

Jose Mourinho kuidhamini safari ya sonara wa Kenya nchini Poland

Leave a comment


Miaka miwili iliyopita,kocha wa klabu ya Real Madrid,Jose Mourinho alizuru nchini Kenya na alisema amenununua kidani kwa msichana sonara ambaye alimtumia aliporudi Hispania.
Na sasa gazeti la The Star la Kenya limesema msichana huyo aitwaye Lelesit Silvana, anatarajiwa kusafiri hadi nchini Poland mwezi September mwaka huu kukutana na Mourinho.
Msichana huyo mwenye miaka ishirini na kitu amesema amekuwa akiwasiliana na kocha huyo kwa e-mail na ziara yake hiyo itakayolipiwa kila kitu nchini Poland itamfanya akae mwezi mzima na kutembelea majiji mbalimbali.
Hata hivyo Silvana alikuwa wa haraka kukanusha uhusiano wowote wa kimapenzi kati yao kwa kusema kuwa ana mpenzi tayari.
“Nina furaha na hii ilikuwa ni ndoto yangu, lakini nina mpenzi mkenya mwenye asili ya kisomali ambaye tumekuwa wapenzi kwa muda,” Silvana aliliambia The Star.
Wakati wa ziara hiyo ya Kenya mwaka 2010 Jose Mourinho alikaa kwenye hoteli ya kifahari ya pwani nchini Kenya ya Almanara akiwa na mke wake na watoto wao wawili (wa kike na wa kiume) wakiwa chini ulinzi mkali.
Ndio hapo alipokutana na Silvana na kumpa order amtengenezee mkufu wa Tanzanite wenye gharama ya shilingi 500, 000 za Kenya(Milioni 9 za Tanzania).
Kulikuwa na uzushi kuwa katika ziara yake ya siku 12 nchini humo, kocha huyo alikutana na waganga wa kienyeji ili wamfanyie mambo kwakuwa ndo alikuwa anaenda kuanza kazi ya kuinoa Real Madrid.

source:bongo5.

WEMA AITWA IKULU

2 Comments


Wema Isaac Sepetu.

WEMA Isaac Sepetu amelidokeza gazeti alipendalo la Ijumaa Wikienda kuwa ameitwa ikulu ya Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza kwa mwaliko maalum.
Wema alisema mwaliko huo aliupata mara tu baada ya kuzindua ile filamu yake ya Super Star wiki mbili zilizopita ambapo katika mwaliko huo wa ujumbe kutoka ikulu hiyo ulimuomba kutoisambaza kwanza kabla ya kwenda kuizindua nchini humo.
“Waliniambia juu ya mimi kuomba uraia wa nchi hiyo ili kukuza filamu zao. Kusema kweli nilikuwa nina ratiba ya kwenda kuizindua filamu yangu Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Yaani sijui hata walijuaje. Sijui ni nini kimetokea, nina wasiwasi. Hata sijui nitaongea nini na Rais wa Burundi,” alisema Wema na kuongeza kuwa maandalizi yakikamilika atatii wito huo muda wowote

source:globalpublishers.

50 CENT KUPIGA SHOW KAMPALA, ATOA MISAADA YA HISANI NCHINI KENYA.

Leave a comment


Kwa mujibu wa gazeti la Daily post la nchini Kenya mwanamuziki 50 Cent kutoka marekani anatarjiwa kufanya concert kubwa jijini Kampala nchini Uganda mwezi Septemba mwaka huu.
Hivi karibuni mwanamziki 50 Cent alikuwa nchini Kenya kwa misaada ya Hisani kwa watu wenye mahitaji maalum.
Ikiwa Uganda inasherehekea miaka 50 ya Uhuru mwezi huo wa Septemba mwanamuziki huyo anatarajiwa kukusanya umati mkubwa wa mashabiki.

Flora Mvungi amkingia kifua H.Baba dhidi ya madai ya Irene Uwoya

Leave a comment


Frola Mvungi.

Baada ya mrembo na muigizaji wa filamu nchini Tanzania,Irene Uwoya kuliambia gazeti la Baabkubwa kuwa katika wanaume ambao hawezi kurudiana nao, H.Baba ni wa kwanza kwasababu ni ‘mchovu’ kitandani, mpenzi wake mpya Flora Mvungi ameibuka kujibu shutuma hizo.
Kupitia Clouds Fm jana, Flora amesema anamshangaa Irene kwa madai hayo, na kusema kuwa H.Baba humpagawisha kwa an ‘earth shaking and mind-blowing sex’ na huenda yeye (Irene) alikuwa anadate na H.Baba mwingine.
Flora amesema katika uhusiano wote na msanii huyo wa Bongo Flava amekuwa akiridhishwa na wala haoni hayo anayoyasema Irene.
Ameongeza kuwa anachojua yeye ni kuwa mapenzi ni kusikilizana na kuzungumza,kuheshiamiana,kujaliana na mwisho kabisa suala la kitandani ndio hufuata ambalo hata hivyo mzee wa ‘Mpenzi Bubu’ analimudu vyema.
Muigizaji huyo pia amesema anashangaa kwanini Irene ameendelea kuongea sana kuhusu mpenzi wake wa zamani H.Baba wakati kila mmoja ana maisha mapya na mpenzi mpya.
Amesema hafurahishwi na tabia hiyo ya Irene ya kumsema na kumzushia scandal H.Baba ambaye huwa hapendi kuzungumza mambo hayo hadharani, tena kwenye vyombo vya habari.

source:bongo5

Older Entries

%d bloggers like this: