Home

Mnyika Kuwa Shahidi Kesi Ya Mauaji

Leave a comment


MBUNGE wa jimbo la Ubungo, John Mnyika atakuwa ni mmoja wa mashahidi wa Serikali watakaoithibitishia mahakama namna walivyohusika washtakiwa wanaotuhumiwa kumuua Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Kata ya Ndago, Yohana Mpinga (30).

Jeshi la Polisi mkoani Singida, limemefikia azimio hilo baada ya kumhoji Mnyika kwa saa tatu juzi usiku, kuhusiana na tukio hilo la mauaji lililotokea baada ya mkutano wake wa hadhara uliofanyika Julai 14 mwaka huu, majira ya jioni.

Mahojiano hayo yaliyoanza saa 11.53 jioni na kumalizika saa 3:15 usiku, yaliendeshwa chini ya kikosi maalum cha askari wa upelelezi kutoka jijini Dar es Salaam kwenye ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoani hapa.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana zilithibitisha kwamba Jeshi la Polisi lilimtaka Mnyika awe tayari kuitwa wakati wowote ili kusaidia kwenye kesi hiyo ya mauaji.

Tayari watu 18 wametiwa mbaroni, miongoni wakiwemo wanachama wa Chadema, kwa tuhuma za kuhusika kwenye mauaji ya kijana huyo wa CCM.

Mnyika alihojiwa huku akiwa na wakili wa Chadema na mbunge wa jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Mauaji hayo ya mwenyekiti wa UVCCM yalifanyika Julai 14 mwaka huu saa 10 jioni huko katika kijiji cha Nguvumali kata ya Ndago jimbo la Iramba magharibi.

Mauaji hayo yanadaiwa kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na vurugu zilizotokea kwenye mkutano wa hadhara ambao Mnyika alikuwa mgeni rasmi.

Katika hatua nyingine, mshauri na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Kitila Mkumbo, ambaye alikuwa ameambatana na Mnyika, alitarajiwa pia kuhojiwa kuhusiana na mauaji hayo jana.
Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz

Wasanii waige mfano wa website ya Diamond

Leave a comment


Katika jambo ambalo wabongo wanasema Diamond kapiga bao ni kuanzisha website yake mwenyewe. Website hiyo iitwayo Thisisdiomond.com imegeuka maarufu kwa mashabiki wake wanaotaka kujua yale ayafanyayo na waandishi wa habari wanaotaka kupata habari zake.
Tofauti na website za wasanii wengine nchini, yake Diamond tunathubutu kusema ndio personal website pekee inayoongoza kwa kuwa updated kila siku kwa matukio mapya. Diamond si mwandishi wa habari lakini anajua kuwa yeye ni mtengeneza habari (newsmaker). Katika uandishi wa habari yeye yupo kwenye ule ubora wa habari (news values) ambao kitaaluma unajulikana kama ‘Prominence’.
Yeye ni mtu maarufu kwahiyo chochote anachokisema ama kukiandika sehemu ni habari kwakuwa ni mtu maarufu. Hivyo ana mengi anayoyaandika kwenye website yake yanayotokana na kile akifanyacho kila siku, bila kusahau picha nzuri na nyingi ambazo huziweka mara kwa mara awapo kwenye ziara zake.
Hakuna show anayoenda na asichukue picha za kuja kuwaonesha mashabiki wake. Hakosi la kuandika kuwajuza mashabiki.
Kwanini tunasema wasanii wengine waige mfano wa website yake? Kwanza wasanii wachache ambao wana website ama blog zao wakumbuke kigezo hicho kuhusu ubora wa habari kuwa wao ni ‘newsworthy’ yaani wanatengeneza habari kwa mengi wanayosema ama kufanya.
Ni jambo la ajabu website ya msanii mkubwa inakuwa updated mara moja kwa mwezi tena kwa habari ya ajabu ajabu tu na wakati mwingine haimhusu yeye mwenyewe! Personal websites/blogs zinapaswa kutoa kwa asilimia kubwa habari kuhusu msanii mwenyewe.

Wasanii wengine wamezigeuza personal blogs zao kama blogs zingine za kawaida zinazotoa habari za watu wengine. Diamond anapaswa kusifiwa kwasababu website yake inamuangaza yeye zaidi. Wapi ameenda kufanya show, amekutana na nani, ana mipango gani n.k.
Ukiwa mtembeleaji mzuri wa website yake utayafahamu hayo. Iweje website binafsi ya msanii mkubwa nchini ijae mambo ya watu wengine tu wakati yeye mwenyewe kila siku kuna mambo anayoyafanya na ambayo kama angeyaandika kwa kuambatanisha na picha mashabiki wake wangefurahia!!
Hivyo wasanii wanaomiliki website/blog binafsi watambue kuwa sio fashion kuwa na website ambayo hubadilishwa habari mara moja ama mbili kwa mwezi. Huna haja ya kuwa na website binafsi wakati huna la kuandika. Inabaki kuwepo tu bila kitu chenye kumrudisha tena msomaji.
Kwa wale ambao hawana website/blog zao ni muda mzuri wa kufikiria kuwa nazo. Ni njia nzuri ya kujitangaza. Waandishi wa habari huzitumia kupata habari halisi na zenye ushahidi kutoka kwa msanii husika. Kumiliki tu akaunti ya Facebook na Twitter hakutoshi.

source:bongo5

AFANDE SELE AKIFUNGUKA KUHUSU SHOW YA ZANZIBAR MUSIC AWARD

Leave a comment


Salaam Ndugu zangu wote mashabiki na wadau wa muziki wetu!!
Tamko langu kuhusiana na lugha zilizotolewa na Twent Percent kuhusiana na show yetu ya Zanzibar Music Award.
“Tulialikwa kwenye ZANZIBAR MUSIC AWARD, na kabla ya kazi makubaliano yote ya kazi kwa mujibu wa mkataba yalifuatwa, makubaliano hayo yalihusisha sisi kujigharamia gharama zote za nauli na Malazi (accomodation).
Tulifika Zanzibar salama, tulipokua Zanzibar twenty alitaka agharamiwe huduma zote ambazo ni nje ya mkataba wetu, nikamuomba na kumsihi sana Ndugu yangu aheshimu mkataba, asitafute matatizo kwani tayari mpaka wakati huu tuna kesi na Halmashauri ya Manispaa ya Moro ambayo kimsingi sikuhusika (nilishatolea ufafanuzi siku za nyuma).
Lakini yeye alipingana na mimi, akanibishia na kunisukuma Mbele ya wageni na wenyeji wetu, wakiwemo Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seiph Ali Idi, Waziri Seiph Khatibu.
Walikuwepo waadishi wa habari wa siku Nyingi Akiwemo Abubakari Liongo (idhaa ya kiswahili radio Ujerumani), Mkurugenzi wa ZENJI FM ndugu Tua Saidi Tua.
Mimi Selemani Abdallah Juma Msindi sihusiki kwa namna yoyote, na tabia zisizo za kuridhisha zinazoonyeshwa na Ndugu yangu Twenty Percent, ambae nimekua nae nyumbani kwangu hata kabla ya Tuzo zake Tano (Kili Music Award) ambazo kazi hizo zote hizo kaandikia nyumbani kwangu siwezi kuwa na tatizo nae ni ndugu yangu kiimani na kikazi, hata kazi yangu niliyofanya nae kabla siku za nyuma “MBELE YAKO NYUMA YANGU” .. Kuna mstari Nilisema ” ..Kuandika Rhyme kwenda Gym kimtindo kuonyesha Ugum, bado unatakiwa uwe na nidhamu ya kweli, sio ya kumzuga Mwalimu, utajihukumu”.
Nimekua nikisisitiza nidhamu kwa Ndugu zangu woote toka enzi za Ghetto BoyZ, Watupori na Mabwasha’Kingdom, ambao wengine hawafanyi sanaa, ila nipo nao kwenye Familia yetu kubwa hapa Tanzania. Nimesikitishwa na kitendo hicho. Siku zote nimekua mwenye kuhitaji suluhu kwa namna ya Amani.
Verry sorry kwa wote ambao mumefadhaika kwa hilo. Tuendelee kuwa pamoja na msisite kutoa ushauri wenu, maoni ili Game letu lisonge. MUNGU ATUBARIKI.
Asanteni sana.
Selemani Juma Abdallah Mutabhazi Msindi.
a.k.a Afande Sele (King of Rhymes)

source:

MAGARI WALIYOZAWADIWA WACHEZAJI WAPYA WA MANCHESTER UNITED NDIO HAYA.

Leave a comment


Shinji Kagawa na Nick Powell

Mjapan Shinji Kagawa amezaliwa miaka 23 iliyopita na club yake ya mwisho kuichezea ni Borussia Dortmund na kaifungia magoli 21 kwa miaka miwili aliyokaa nayo na amezichezea timu za taifa toka mwaka 2006, Powell yeye ameichezea Crew Alexandra kwa miaka miwili na kuondoka na magoli yake 16, Timu za taifa za England amejiunga nazo toka 2009.

Waandishi wa habari walio hudhuria

source:millardayo

PIGO JINGINE KWA RONALDINHO WA BRAZIL.

Leave a comment


Ronaldinho akiwa na Kinywaji cha Pepsi pembeni kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Mkali wa soka kutoka Brazil ambae ni mwezi umepita toka aondoke kwenye club ya Flamengo aliyokua anaichezea kutokana na kushindwa kumlipa mishahara yake, amepatwa na tatizo jingine kwenye moja kati ya madili yake. Kampuni ya vinywaji ya Coca-cola imeukatisha mkataba mnene na mchezaji Ronaldinho baada ya mchezaji huyo kuonekana akiwa na vinywaji vya Pepsi pembeni wakati wa mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na club yake mpya ya Atletico Mineiro. Mkataba wake na Coca-cola ambao hauna hata mwaka toka usainiwe, ulitakiwa kwenda mpaka 2014 ambapo malipo yake kwa mwaka ni dola za kimarekani zaidi ya laki saba.
Pepsi ni wadhamini wa club yake mpya ya Mineiro na kuwepo kwa vinywaji hivyo kwenye mkutano huo na waandishi wa habari sio chaguo au uamuzi wa Ronaldinho, ni maamuzi ya club kwa sababu ndio yenye mkataba na Pepsi na sio Dinho.Unaweza kulike na kutweet hii story ili watu wako waione pia…

CHEKA, WOLPER WAAHIDI KUWATWANGA WAPINZANI WAO KWENYE TAMASHA LA MATUMAINI.

Leave a comment


Bondia Francis Cheka (katikati) akitamba mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuwa atamchakaza mpinzani wake Japhet Kaseba.

Wolper (kulia) akijitapa kuwa atamtwanga mpinzani wake mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani).

Kocha wa Wema, Rashid Matumla (wa tatu kushoto) akizungumza kwa niaba ya Wema (ambaye hakuwepo) kwenye mkutano huo.

Nahodha wa Bongo Fleva, H Baba (kulia) akiahidi ushindi kwa timu yake dhidi ya Bongo Movie.

Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na (kutoka kushoto) kocha wa bondia Francis Cheka (Abdalah Saleh Komando), Francis Cheka, meneja wa mfuko wa elimu (Charles Kapima), mmoja wa waratibu wa tamasha hilo (Luqman Maloto), promota wa pambano hilo, Kaike Silaju, bondia Japhet Kaseba na mwisho ni meneja wa Kaseba (Idd Bakari).

Wakati homa ya mapambano ya ndondi yanayosubiriwa kwa hamu kati ya Francis Cheka na Japhet Kaseba pamoja na wakali wa filamu nchini, Wema Sepetu na Jacqueline Wolper, ikizidi kupanda, baadhi ya mabondia hao wametoa tambo kuwa watawachakaza wapinzani wao siku hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya kisasa ya The Atriums jijini Dar, Jacqueline Wolper alitamba kumpiga vibaya mpinzani wake siku ya Jumamosi kwenye Tamasha la Matumaini pale Uwanja wa Taifa.
“Sipendi maneno, napenda vitendo, nimekuwa nikisikia Wema na rafiki yake wanaongea sana kuhusu mimi kwenye TV.
“Nataka nikate mdomo wake siku hiyo kwa kumpiga” alisema Wolper. Nae Bondia Francis Cheka alitamba kuwa kama kawaida yake atamchachafya mpinzani wake katika tamasha hilo.

source:PICHA/HABARI : ERICK EVARIST/GPL

MAJAJI WA EPIC BONGO STAR KUTEMBELEA MAKAZI RASMI YA ZANTEL SABASABA.

Leave a comment


Mkuu wa mawasiliano ZANTEL Awaichi Mawalla alipata nafasi ya kuelezea njia mpya ambayo wenye vipaji vya kuimba waliokosa nafasi ya kufanya usaili wanaweza kufanya usaili kupitia simu zao za mkononi. Mfumo huu ni wa sauti ambapo mshiriki anapewa nafasi ya kuimba nyimbo aitakayo kwa muda usiiozidi dakika moja na kuweza kupata nafasi ya kusikilizwa na Majaji.

Master J

Rita Paulsen na Mkuu wa Masoko kutoka Zantel bwana . Deepak K. Gupta.

Rita Paulsen na Salama Jabir wa tatu kutoka kulia, wakiwa pamoja na wafanyakazi wa Zantel.

Majaji wa EBSS walipata nafasi ya kutembelea kujionea maonyesho yanaondelea ikiwa ni pamoja na kukutana na waandishi wa habari kuelezea waliyoshuhudia katika usaili wa mikoa mitatu waliyopitia ya Dodoma , Zanzibar na Lindi . Pia waliweza kutoa sifa wanazoziangalia katika kutafuta vipaji vya muziki pamoja na kueleza eneo la usahili unaofuata wiki hii A town Arusha Triple A.

Older Entries

%d bloggers like this: