Home

Nadia Buari akataa uvumi wa kurudiana na Michael Essien

Leave a comment


Muigizaji wa filamu wa kike nchini Ghana Nadia Buari, amekanusha taarifa za udaku kuwa ana mpango wa kurudiana na mpenzi wake wa zamani, mchezaji wa klabu ya Chelsea, Michael Essien.
Habari za kuwa wapenzi hao huenda wamerudiana zilienea kwenye internet wiki iliyopita baada ya kuonekana kwa picha zao wakibusu kwenye birthday party ya mtangazaji maarufu nchini Ghana wa Diva’s Show, Nana Aba Anamoah.
Nadia ambaye kwa sasa amejiingiza pia kwenye muziki, amezieleleza picha hizo kwa “innocent pictures” zilizopigwa kwenye party hiyo.
“Hakukuwa na kupigana busu; Essien na mimi ni marafiki lakini, hatuna issue kubwa sana. Lakini kuhusiana na ripoti kuwa tumerudiana, hakuna kitu kama hicho,” alisema.
Nadia aliendelea kueleza kwamba “tulikuwa tunajaribu kupiga picha na mapaparazi nao walikuwa wakipiga picha zao. Tulikuwa tupige picha mbili tu lakini wao waliendelea kuchukua picha nyingi na niliona aibu sana hivyo nilijaribu kumwacha Essien, nilitaka kuficha uso wangu tu.
Nadia na Essien waliachana miaka miwili iliyopita.

source:ghanacelebrities

WAREMBO WA MISS VYUO VIKUU TANZANIA WATEMBELEA BUNGENI MJINI DODOMA LEO, KUJIFUNZA SHUGHULI ZA BUNGE

Leave a commentWarembo wanaotarajia kupanda jukwaani kuwania Taji la Miss Vyuo Vikuu 2012, siku ya Ijumaa wiki hii katika Ukumbi wa Maisha Club, wakipozi kwa picha ya pamoja nje ya Ukumbi wa Bunge, wakati warembo hao walipofika kutembelea na kujifunza shughuli za Bunge mjini Dodoma Leo, Julai 03, 2012. Picha zote na Mtandao wa http://www.sufianimafoto.blogspot.com

Irene Uwoya amgeuzia kibao Flora Mvungi

Leave a comment


Vita vya maneno kati ya waigizaji wa filamu nchini Flora Mvungi na Irene Uwoya jana vimechukua sura mpya.
Wiki iliyopita tuliandika habari kuhusiana na Flora kutofurahishwa na kitendo cha Irene kuongea na vyombo vya habari na kusambaza shutuma kuwa mpenzi wake wa zamani H.Baba hajui mapenzi.
Jana Irene Uwoya aliongea na Clouds Fm na kusema Flora na H.Baba wamemchokoza.
Alisema yeye pia anamshangaa Flora kwa kupakaza maneno kuwa aliongea na magazeti ‘kumvua nguo mpenzi wake wa zamani H’Baba kuwa ni zezeta kitandani kitu ambacho alikanusha kukisema.
Irene alisema kwanza anamuona Flora ni mshamba na kumfananisha na ‘vocha’ na kamwe sio saizi yake.
Aliongeza kuwa yeye si mtu wa kutembea na H.Baba na kudai kuwa wako pamoja na Flora kwakuwa wote ni washamba na wote amewafananisha na vocha.
‘Sasa leo nasema kuwa kweli H.Baba hajui mapenzi, hana lolote, ni tegemezi na simtaki,alisema.
Akiongea kwa jaziba, Irene aliongeza kuwa yeye yupo level zingine na anawadharau wapenzi hao.

Picha 18 za BET AWARD

Leave a commentBeyonce

Big-Sean

Big-Sean Michelle na Letoya

Boris Kodjoe

Buster Rhymes

Common

Faith Evans

Future

Jamie Fox

Kanye akishukuru baada ya kupokea tuzo

Jayz na Kanye wakifurahia tuzo yao baada yakuipokea

Meaan good

Miguel

Monica

Rick Ross

Swizz Beatz

Tyger

Willow na Jaden-Smithhabari kamili
Kundi la hip hop la Kenya, Camp Mulla limeshindwa kutamba kwenye tuzo za BET, baada ya kipengele lililokuwa limetajwa kuwania kuwaendea WizKid na Sarkodie.
Kipengele hicho cha Best International Act Africa, kimewaendea wasanii hao wawili kwa pamoja, WizKid wa Nigeria na Sarkodie wa Ghana.
Hata hivyo CampMulla hawakuweza kuhudhuria tuzo hizo baada ya kukosa visa ya kusafiria hadi Los Angeles nchini Marekani.
Hii ni list ya washindi wengine katika tuzo za BET 2012, zilizotolewa alfajiri ya leo kwa saa za Afrika Mashariki.
Centric Awards:
Common
Best Group:
The Throne – Jay-Z and Kanye West
Best Actor:
Kevin Hart – Think Like A Man
Best New Artist:
Big Sean
Best Male R&B Artist:
Chris Brown
Best Collaboration:
Wale featuring Miguel
Best Gospel:
Yolanda Adams
Best Female R&B Artist:
Beyonce
Best Female Hip-Hop Artist:
Nicki Minaj
Video Of The Year:
Jay-Z and Kanye West
Humanitarian Award:
Al Sharpton
Viewers’ Choice:
Mindless Behavior
Video Director Of The Year:
Beyonce and Alan Ferguson
AOL Fandemonium Award:
Chris Brown

Photosource: Getty images for BET

Madaktari 72 wasimamishwa kazi kwa Mgomo

Leave a comment


Mwenyekiti wa Bodi Kaimu [caption id="attachment_3013" align="alignleft" width="500"] Mkurugenzi wa wa hospitali ya rufaa Mbeya Dr E. Sankey akimsikiliza kwa makini kaimu mkuu wa mkoa Mbeya.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Norman Sigara Aikzungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu kusimamishwa kazi kwa madaktari hao.[/caption]BODI ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, imewasimamisha kazi madaktari 72 kwa kosa la kutoingia kazini kwa siku tano jambo ambalo ni kinyume cha makubaliano ya mkataba.

Imeelezwa kuwa madaktari hao ambao 54 ni wale wa mafunzo ambao waliingia mkataba wa miaka miwili na hospitali ya Rufaa na madaktari 18 ni wale walioajiriwa na Wizara ya afya.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Bodi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Norman Sigara, alisema kitendo cha madaktari kutoripoti kazini kwa siku tano ni ukiukwaji wa kanuni za utumisha wa umma toleo la 2009 kifungu namba F.16-F17 na F. 27.

“Hivyo kupitia kanuni hiyo madaktari hao wamesimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa hatua zaidi za kinidhamu,”alisema Sigara.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wa Bodi, imeelezwa kuwa siku ya tarehe 23/6/2012 wafanyakazi 15 waliokuwa zamu(Intern Doctors 12 na Registrars3) hawakufika kazini na tarehe 24/6/2012 wafanyakazi 19(Intern doctors 15 na Registrars 4) hawakufika kazini.

Alisema, kuanzia tarehe 25/6/2012 hadi leo imethibitika kuwa Interns doctor 54 na Registrars 18 hawakufika kazini hadi leo tarehe 28/6/2012 ambapo tarehe 25/6/2012 bodi ya hospitali ilifanya kikao cha dharura kujadili hali ya utendaji kazi na utoaji huduma hospitalini na kutoa uamuzi.

Sigara, aliyataja maamuzi hayo kuwa ni Mwenyekiti wa Bodi akutane na madaktari ambao hawakufika kazini ili awasikilize sababu za kutofika na kujadili namna ya kumaliza matatizo hayo jambo ambalo madaktari hao waligoma.

Alisema, baada ya madaktari hao kukaidi ombi hilo, Bodi ya hospitali ili waandikia barua za kujieleza kwanini wasichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuvunja mkataba walioingia na hospitali na pia kukiuka
kanuni za kudumu za utumishi wa umma nalo walilikaidi

“Iwapo madaktari ambao hawakuripoti au kueleza sababu za kuridhisha ifikapo tarehe 28/6/2012. Kwa kuzingatia kanuni za utumishi wa Umma, madaktari hao watasimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,”alisema.

Aidha, alisema kuwa kwa ujumala madaktari hao waligomea barua zote mbili yaani ya kuitwa kwenye kikao pamoja na ile ya kuwataka kujieleza hivyo Bodi imechukua hatua za kisheria za kuwafukuza kazi.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa bodi, alisema kuwa tayari hospitali ya Rufaa kwa ushirikiano wa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, madaktari watano wamepatikana ili kusaidia huduma kwa hospitali hiyo.

RAIA WAWILI WA IRAN KIZIMBANI NCHINI KENYA KWA KUMILIKI VIFAA VYA MILIPUKO.

Leave a comment


Raia wawili wa Iran wamefikishwa mahakamani mjini Nairobi nchini Kenya kwa tuhuma za kumiliki vifaa vya kulipuka kinyume cha sheria, ikiwa ni siku moja baada ya shambulizi la bomu la mkono katika baa moja lililosababisha vifo vya watu watatu mjini Mombasa.
Polisi nchini Kenya imewataja Wairan hao kuwa ni Ahmed Mohamud na Said Mausud, na kuwa walikamatwa wiki iliyopita kwa kuwa na mahusiano na kundi la kigaidi linalopanga mashambulizi ya mabomu mjini Mombasa na Nairobi.
Aidha Polisi wamesema vifaa vya kulipuka vilipatikana katika mji wa Mombasa kufuatia taarifa zilizotolewa na Wairan hao.
Mahakama ya jijini Nairobi inatarajiwa kupitisha uamuzi juu ya ombi la Wairan hao kutaka waachiwe huru kwa dhamana.
Waongoza mashitaka wameitaka mahakama hiyo kukataa ombi hilo.


source:dewjiblog

WAFANYAKAZI WA UN-WAGOMA

Leave a comment


Wafanyakazi katika ofisi ya Umoja wa Mataifa iliyoko mjini Entebe, Uganda wamefanya mgomo jana Jumatatu kulalamikia mazingira mabaya ya kufanyia kazi pamoja na kutaka nyongeza ya mishahara.

Wafanyakazi zaidi ya 120 walianza mgomo leo asubuhi na hivyo kukwamisha shughuli katika ofisi hiyo ya UN. Wafanyakazi hao wanasema kuwa Umoja wa Mataifa umeipa kampuni ya kibinafsi kandarasi ya kuendesha ofisi hiyo na kwamba kampuni hiyo sasa imekata mishahara yao kwa asilimia kubwa. Wameongeza kuwa hawana bima za afya wala barua za kuajiriwa na hivyo wanahisi kuwa UN inawafanya kuwa watumwa katika nchi yao. Wafanyakazi hao wamesisitiza kuwa hawatorudi kazini hadi pale mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Nchini Uganda atakapofika katika eneo hilo na kutatua matatizo yao.

Older Entries

%d bloggers like this: