Home

Mnyika Kuwa Shahidi Kesi Ya Mauaji

Leave a comment


MBUNGE wa jimbo la Ubungo, John Mnyika atakuwa ni mmoja wa mashahidi wa Serikali watakaoithibitishia mahakama namna walivyohusika washtakiwa wanaotuhumiwa kumuua Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Kata ya Ndago, Yohana Mpinga (30).

Jeshi la Polisi mkoani Singida, limemefikia azimio hilo baada ya kumhoji Mnyika kwa saa tatu juzi usiku, kuhusiana na tukio hilo la mauaji lililotokea baada ya mkutano wake wa hadhara uliofanyika Julai 14 mwaka huu, majira ya jioni.

Mahojiano hayo yaliyoanza saa 11.53 jioni na kumalizika saa 3:15 usiku, yaliendeshwa chini ya kikosi maalum cha askari wa upelelezi kutoka jijini Dar es Salaam kwenye ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoani hapa.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana zilithibitisha kwamba Jeshi la Polisi lilimtaka Mnyika awe tayari kuitwa wakati wowote ili kusaidia kwenye kesi hiyo ya mauaji.

Tayari watu 18 wametiwa mbaroni, miongoni wakiwemo wanachama wa Chadema, kwa tuhuma za kuhusika kwenye mauaji ya kijana huyo wa CCM.

Mnyika alihojiwa huku akiwa na wakili wa Chadema na mbunge wa jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Mauaji hayo ya mwenyekiti wa UVCCM yalifanyika Julai 14 mwaka huu saa 10 jioni huko katika kijiji cha Nguvumali kata ya Ndago jimbo la Iramba magharibi.

Mauaji hayo yanadaiwa kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na vurugu zilizotokea kwenye mkutano wa hadhara ambao Mnyika alikuwa mgeni rasmi.

Katika hatua nyingine, mshauri na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Kitila Mkumbo, ambaye alikuwa ameambatana na Mnyika, alitarajiwa pia kuhojiwa kuhusiana na mauaji hayo jana.
Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz

AFANDE SELE AKIFUNGUKA KUHUSU SHOW YA ZANZIBAR MUSIC AWARD

Leave a comment


Salaam Ndugu zangu wote mashabiki na wadau wa muziki wetu!!
Tamko langu kuhusiana na lugha zilizotolewa na Twent Percent kuhusiana na show yetu ya Zanzibar Music Award.
“Tulialikwa kwenye ZANZIBAR MUSIC AWARD, na kabla ya kazi makubaliano yote ya kazi kwa mujibu wa mkataba yalifuatwa, makubaliano hayo yalihusisha sisi kujigharamia gharama zote za nauli na Malazi (accomodation).
Tulifika Zanzibar salama, tulipokua Zanzibar twenty alitaka agharamiwe huduma zote ambazo ni nje ya mkataba wetu, nikamuomba na kumsihi sana Ndugu yangu aheshimu mkataba, asitafute matatizo kwani tayari mpaka wakati huu tuna kesi na Halmashauri ya Manispaa ya Moro ambayo kimsingi sikuhusika (nilishatolea ufafanuzi siku za nyuma).
Lakini yeye alipingana na mimi, akanibishia na kunisukuma Mbele ya wageni na wenyeji wetu, wakiwemo Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seiph Ali Idi, Waziri Seiph Khatibu.
Walikuwepo waadishi wa habari wa siku Nyingi Akiwemo Abubakari Liongo (idhaa ya kiswahili radio Ujerumani), Mkurugenzi wa ZENJI FM ndugu Tua Saidi Tua.
Mimi Selemani Abdallah Juma Msindi sihusiki kwa namna yoyote, na tabia zisizo za kuridhisha zinazoonyeshwa na Ndugu yangu Twenty Percent, ambae nimekua nae nyumbani kwangu hata kabla ya Tuzo zake Tano (Kili Music Award) ambazo kazi hizo zote hizo kaandikia nyumbani kwangu siwezi kuwa na tatizo nae ni ndugu yangu kiimani na kikazi, hata kazi yangu niliyofanya nae kabla siku za nyuma “MBELE YAKO NYUMA YANGU” .. Kuna mstari Nilisema ” ..Kuandika Rhyme kwenda Gym kimtindo kuonyesha Ugum, bado unatakiwa uwe na nidhamu ya kweli, sio ya kumzuga Mwalimu, utajihukumu”.
Nimekua nikisisitiza nidhamu kwa Ndugu zangu woote toka enzi za Ghetto BoyZ, Watupori na Mabwasha’Kingdom, ambao wengine hawafanyi sanaa, ila nipo nao kwenye Familia yetu kubwa hapa Tanzania. Nimesikitishwa na kitendo hicho. Siku zote nimekua mwenye kuhitaji suluhu kwa namna ya Amani.
Verry sorry kwa wote ambao mumefadhaika kwa hilo. Tuendelee kuwa pamoja na msisite kutoa ushauri wenu, maoni ili Game letu lisonge. MUNGU ATUBARIKI.
Asanteni sana.
Selemani Juma Abdallah Mutabhazi Msindi.
a.k.a Afande Sele (King of Rhymes)

source:

MUKAMA AKUTANA NA BILIONEA WA AFRICA

Leave a comment


Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akimkaribisha kwa bashasha, Mwekezaji kutoka Nigeria, Aliko Dangote, wa Dangote Industries Ltd alipowasili Ofisi Ndogo ya Makamo Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es Salaam, leo, Julai 15, 2012, kwa ajili ya mazungumzo mbalimbali ikiwemo namna mwekezaji huyo anavyoweza kufanyakazi na Chama Cha Mapinduzi katika nyanja kadhaa za kibiashara. Katikati ni Balozi wa Nigeria hapa nchini, Dk. Ishaya Nanjabu. (Picha na Bashir Nkoromo).

Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akimkaribisha katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Mwekezaji kutoka Nigeria, Aliko Dangote, wa Dangote Industries Ltd alipowasili Ofisi Ndogo ya Makamo Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es Salaam, leo, Julai 15, 2012, kwa ajili ya mazungumzo mbalimbali ikiwemo namna mwekezaji huyo anavyoweza kufanyakazi na Chama Cha Mapinduzi katika nyanja kadhaa za kibiashara. Kulia ni Balozi wa Nigeria hapa nchini, Dk. Ishaya Nanjabu.

Mfanyabiashara wa Kampuni ya Dangote Industries Ltd ya Nigeria, Aliko Dangote akitia saini kitabu cha wageni Ofisini kwa Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama (kulia) baada ya kiwasili. Kushoto ni Balozi wa Nigeria hapa nchini, Dk. Ishaya Nanjabu.

Mukama na Ujumbe wa mgeni huyo wakiwa katika mazungumzo kwenye ukumbi wa sektretarieti Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM.

Mukama na Ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni huyo na Ujumbe wake, mbele ya Ofisi Ndogo ya Makamo Makuu ya CCM, kwenye jengo ilimozaliwa TANU.

SOURCE:dewjiblog

Wema Sepetu na Diva waingia kwenye orodha ya kusaidia wasiojiweza

Leave a comment


Ray Kigosi akitoa msaada

Lady Jay Dee akitoa msaada

Lady Jay Dee

Wema Sepetu

Diva Loveness Love

Muigizaji wa filamu nchini na Miss Tanzania wa zamani (2006),Wema Sepetu anatarajiwa kwenda jijini Arusha mwezi huu na kushiriki uoashaji wa magari ili kukusanya fedha za kusaidia watu wasiojiweza jijini humo.
“On 14th July I will be in Arusha with manager kushiriki uoshaji wa magari ili kuchangia fedha za kusaidia wasiojiweza in Arusha,” alitweet jana.
Mwingine aliyeamua kujitolea nguvu na mali kuchangisha fedha kwaajili ya kuwasaidia watoto yatima ni mtangazaji wa Clouds Fm, Loveness aka Diva.
Kupitia website yake, Diva amesema, “So nimeamua kwa muda mrefu sana kutoa for charity and right now am too busy organizing this charity event inayoitwa Diva giving for charity. Aim is raising much needed funds to support orphans.
June na July imekuwa miezi iliyotumiwa zaidi na mastaa wa hapa nchini kusaidia vituo vya watoto yatima.
June 30, mwanamuziki Lady Jaydee pamoja na familia yake walikitembelea kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre kilichopo Kinondoni jijini Dar es Salaam na kutoa misaada mbalimbali ikiwa pamoja na kushiriki chakula cha mchana na watoto hao.
Katika hotuba yake, kituo hicho kilisema kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na kukosa fedha za kuwalipa wahudumu, Kukosa eneo kubwa la kujenga kituo, Kukosa wafadhili, watoto kutokuwa na sare za shule na kukosa gharama za kuwasomesha (michango ya shule).
Lady Jaydee aliwaahidi kuwatafutia kiwanja kikubwa kwaajili ya kujenga kituo kingine na kusema kuwa iwapo akitokea mtu wa kuwasaidia kiwanja, watachangisha fedha za kuanza ujenzi huo.
Naye muigizaji wa filamu mwenye mafanikio makubwa nchini Raymond Kigosi aka Ray The Greatest, weekend iliyopita alikitembelea kituo hicho cha Maungo na kutoa msaada sambamba na uzinduzi wa filamu yake mpya ya Sobbing Sound.
Kupitia blog yake Ray alisema: “Hili ni jukumu la watanzania wote kuanza kuguswa katika hili maana hapa duniani sisi ni wapangaji tu makazi yetu ni kwa Mungu Baba, sasa unapopata kidogo jaribu kuwafikiria na wale waliokuwa na maisha magumu, yaani tugawane umasikini.”

source:

KUONDOKA KWA KALALA JR BENDI YA MAPACHA 3 HAITAYUMBA.!

Leave a comment


Pichani kati ni Mwanamuziki mahiri Josee Mara akifafanua kuhusiana na mikakati yao waliyonayo kwa sasa mara baada ya mwanamuziki mwenzao mmoja,Kalala Jr kutimka na kuwaacha wakiwa wawili badala ya watatu.Josee Mara amesema wao wako fiti na hakuna kilichoharibika,kwani kuna wanamuziki wengine kadhaa ambao ni wazuri na watafanya nao kazi kama ilivyokuwa kwa Kalala Jr.”Na sasa hivi nakuhakikishia Da’Suzzy tutapiga kazi ile mbaya,kwa sababu hao vijana tunaowaongeza ni wanamuziki wazuri na tunawahamu toka kitambo,kwa hivyo naamini mambo yatakuwa sawa na washabiki wetu wasivunjike moyo,waendelee kutuunga mkono tu,sisi ni wapambanaji kwa hiyo ni lazima tupambane”amesema Josee Mara.Aidha Khalid Chokoraa ameongeza kuwa katika kuonesha bado wako fiti wamekwisharekodi singo yao moja iitwayo ONA NAONEWA,ambayo wataitambulisha hivi karibuni kwa mashabiki wa muziki wa dansiMmoja wa watangazaji wa Clouds FM,kupitia kipindi cha Wikend Bonanza,Da’ Suzzy akizungumza na wanamuziki mahiri wa dansi hapa nchini waliokuwa wakijiita Mapacha 3,ambapo kwa sasa mmoja wao Kalala Jr ameamua kuachia ngazi na kuwaacaha wenzake Khalid Chokoraa na Josee Mara kama uwaonavyo pichani wakiwa na Meneja wao Hamis Dacota pichani kulia.Da’Suzzy alikuwa akitaka kujua kwanini msanii mwenzao Kalala Jr ameamua kutimka kwenye bendi yao na kwamba wana mikakati gani ya kuliziba pengo la mwanamuziki huyo aliyetimka.Kwa mujibu wa Meneja wa bendi hiyo ya Mapacha 3,Hamis Dacota amebainisha kuwa Kalala Jr aliamua kuondoka mwenyewe bila kuwepo na ugomvi wowote baina yao,”hivyo kama mwanamuziki mwenzetu,kijana mwenzetu tunamtakia kila kheri huko aendako,lakini kama akitaka kurudi pia milango iko wazi anakaribishwa sana,kwa sababu yeye ni mmoja wa waasisi wa bendi ya mapacha 3″,alisema Dacota.

source:dewjiblog.

Ray Azindua Filamu kwa Kutoa Msaada Kwa Yatima

Leave a comment


Kampuni ya usambazaji wa filamu za kitanzania Steps Entertainment ya Jijini Dar-Es-Salaam ikishirikiana na Msanii wa filamu wa Bongo Movies, Vincent Kigosi almaarufu kama Ray, wametoa Msaada wa vitu mbali mbali kwenye kituo cha watoto yatima cha Maunga Center kilichopo maeneo ya Kinondoni ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa filamu yake mpya.

Msaada huo ni sehemu ya mpango wa matukio ya uzinduzi wa filamu yake ‘Sobing Sound’ na pia kurudisha fadhila kwa jamii ambayo ndio wateja wakubwa wa filamu za kitanzania.

Filamu hiyo imezinduliwaa kwa staili tofauti ambapo badala ya kuzindua ukumbini kama ilivyozoeleka na wasanii wengi, msanii huyo ameamua kuzindua filamu hiyo katika kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh. Milioni 1.5.

Akizungumza na http://www.bongo5.com mara baada ya kuzindua filamu hiyo, akiwa pamoja na watoto yatima wa kituo hicho, Ray, ambaye pia aliongozana na afisa masoko wa kampuni ya steps,bwana Ignatusu Kambarage ,alisema ameamua kufanya hivyo kutokana na ukweli kwamba watu wengi wamekuwa wakifurahia maisha huku wengine wakiendelea kutaabika, kitendo ambacho amesema, si kizuri.


Alisema ujio wa filamu hiyo ni kama azma yake aliyoipanga tangu awali kuhakikisha filamu zake zote zinafanya vizuri ,na atahakikisha japo kidogo,kwa namna yoyote anawakumbuka watoto yatima, kwani anawapenda.

“Hii ni filamu ya kwanza kutoa, tangu kifo cha mwigizaji mwenzangu Steven Kanumba alipofariki dunia, Aprili mwaka huu, na najisikia furaha kuja hapa na kutoa msaada kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu” alisema Ray

source:bongo5

Je wamjua aliye Nyuma ya Mafanikio ya Diamond??

Leave a comment


Diamond akiwa stajini

Diamond akiperform

Diamond na Masela wake

Hapa ndo palipofanyika Miss Reds arusha Mt. Meru Hotel

Ruge akimpa maelekezo Diamond Kuhusu Drums

Ruge akimfundisha jinsi ya kuplay Kinanda

Ulishajiuliza kwanini Diamond yuko smart sana kwa namna anavyozipeleka issue zake za muziki? Hushangai iweje msaniii huyu ambaye wengi walitegemea awe na elimu ya chuo kikuu ndio aweze kuufanya muziki kwa umaridadi mkubwa kiasi cha kutochuja kwa show zake japo zinajipanga kama mayai kwenye tray!
Well, wengi hili wanaweza kuwa wanalijua juu juu tu ama hawalijui kabisa kuwa the person behind Diamond’s music creativity is none other than Ruge Mutahaba!!
Yeah, habari ndio hiyo, hate it or love it.
Tangu show ya aina yake ya Diamonds Are Forever iliyowapa mkwanja mnene wa kuweka benki na kula bata, show ya Dar Live iliyompa sifa Diamond kwa kutua kwenye ‘Uwanja huo wa taifa wa burudani mpaka show ya Big Brother Stargame aliyoifanya mwaka huu. He (Ruge) was the mastermind!
Ameweza kumtengeneza Diamond kuwa bidhaa ya thamani isiyochuja.Hautakosea ukimwita Russell Simmons wa Tanzania. Kwa uzoefu alionao kupitia show zinazoandaliwa na kituo cha Clouds Fm, ameweza kuzijua ramani zote za kupitia ili kufanikiwa ‘kibiashara’ kwenye muziki wa Tanzania. He has the music map in the palm of his hands and never missed a shot!
Kuna mtu mmoja wa karibu sana na Diamond hivi karibuni ametuambia kuwa maandalizi ya show ya ‘Diamonds Are Forever ya pale Mlimani City yalichukua takribani wiki nzima. Ruge alikuwa akienda kila siku kuangalia maendeleo ya rehearsal and he was like, “mmh mmh! Hapo bado,ongezeni nguvu zaidi.”
Kwenye show ya hivi karibuni ya Miss Redds Tanzania huko Arusha, Ruge alionekana kwenye picha akimwelekeza Diamond namna ya kupiga kinanda na ngoma. Haijalishi kama anajua kupiga hivyo vitu ama la,hilo si suala letu, cha msingi ni kuwa ushauri wake unafanya kazi kwa Diamond.
And tell you what, hakuna mtu mwenye connection ya masuala ya muziki iwe ndani ya nchi ama nje kama Ruge! Hivyo kuchuja kwa Diamond katika ramani ya muziki wa kibiashara bado sana.

source:bongo5

Older Entries

%d bloggers like this: