Home

Picha na Matukio yaliyojiri kwenye Tamasha la Matumaini

Leave a comment


Jose Chameleone akitoa burudani.

Jose Chameleone akitoa burudani.

Wabunge mashabiki wa Simba wakishangilia ushindi dhidi ya watani wao wa Yanga.

Nyomi iliyohudhuria tamasha hilo.

Wema na Wolper wakionyeshana ubabe.

Bondia Mchumia Tumbo akimzimisha mpinzani wake.

Jamaa aliyemvaa Wema.

JULAI 7, 2012 Jiji la Dar lilisimama kwa takribani saa 16 kupisha tamasha la kihistoria la Usiku wa Matumaini lililotimua vumbi ndani ya Uwanja wa Taifa, Ijumaa Wikienda linakupa ripoti kamili.
Zilikuwa ni saa 16 za hekaheka, vifijo, nderemo, shangwe na burudani ya hali ya juu kuanzia saa mbili za asubuhi mpaka saa sita za usiku, Jumamosi iliyopita ambapo macho na masikio ya wengi viliekezwa uwanjani hapo.
SHUGHULI ILIVYOANZA
Mpango mzima ulianza majira ya saa mbili asubuhi ambapo wasanii chipukizi walifungua pazia la burudani kwa kuwarusha mashabiki waliokuwa wanaendelea kufurika uwanjani hapo.
Wakati hayo yakiendelea, walinzi na wakata tiketi walikuwa na wakati mgumu kuuhudumia umati wa watu uliokuwa umejazana nje ya lango la kuingilia uwanjani hapo huku Bendi ya FM Academia wakiwa wa kwanza kulianzisha kwa kutoa burudanai ya nguvu.
UPAKO WATAWALA
Baada ya wasanii chipukizi kumaliza kutoa burudani, ilifika zamu ya wasanii wa nyimbo za injili ambapo wakali wa muziki huo wakiongozwa na Upendo Nkone, Bahati Bukuku, Bonny Mwaitege, Martha Mwaipaja na Glorious Celebration waliitangaza vyema injili takatifu kwa kupitia karama ya uimbaji. Wakafuatia wasanii chipukizi wanaochana mistari.
BONGO MOVIES VS BONGO FLEVA
Mvua ya burudani iliendelea kunyesha ndani ya uwanja huo ambapo baada ya pilikapilika za mchana kutwa, hatimaye uliwadia wasaa uliokuwa unasubiriwa na wengi.
Wasanii wa kambi mbili hasimu, Bongo Movie inayoundwa na wasanii wa filamu na maigizo ya Kibongo na Bongo Fleva inayoundwa na wasanii wa muziki wa kizazi kipya, walijitupa dimbani katika mchezo uliovuta hisia za wengi.
Wasanii Jacob Steven ‘JB’, Vincent Kigosi ‘Ray’, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na wengine wengi walikuwa kivutio kikubwa kwa upande wa Bongo Movie huku wasanii Hamis Baba ‘Baba’, Haroun Kahena ‘Inspekta’, Karama Masoud na wengine kibao wakisakata kabumbu la hali ya juu.
Mpaka kipyenga cha mwisho kinapulizwa, Timu ya Bongo Movie iliibuka kidedea kwa kuinyuka Bongo Fleva goli 1-0, lililofungwa na msanii anayejulikana kwa jina moja la Kiduku. Benchi la ufundi la Bongo Movie, likiongozwa na Fatuma Makongoro ‘Bi Mwenda’ lililipuka kwa shangwe wakati kipyenga cha mwisho kikipulizwa.
POLISI WA KIKOSI CHA MBWA WAWAKOSHA MASHABIKI
Baada ya mechi kati ya wasanii wa filamu na wale wa muziki kumalizika, polisi wa kikosi cha mbwa na farasi waliingia uwanjani na kuonesha namna mbwa walivyofuzu katika kukabiliana na uhalifu.
Wakaonesha wanavyoweza kukamata madawa ya kulevya na mabomu. Uwanja mzima ukalipuka kutokana na mashabiki kukoshwa na umahiri wa mbwa hao wanaotunzwa na jeshi la polisi nchini.
WAHESHIMIWA WABUNGE WATOANA JASHO
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaozishabikia timu za Simba na Yanga, nao walijitupa dimbani kucheza mchezo ambao ulikuwa maalum kuhamasisha uchangiaji wa fedha za kujengea mabweni katika shule za sekondari zilizopo vijijini, chini ya Mamlaka ya Elimu Tanzania.
Wabunge Idd Azzan, Zitto Kabwe, Joshua Nasari na wengine wengi waliiongoza timu ya Wabunge wa Simba kukanyaga kandanda safi, huku Mwingulu Nchemba na wenzake wakipiga soka safi upande wa Wabunge wa Yanga.
Mpaka mwamuzi Othman Kazi anapuliza kipyenga cha mwisho, matokeo yalikuwa ni suluhu (0-0).
Mikwaju ya penalti ilipopigwa, Timu wa Wabunge wa Simba iliibuka kidedea kwa kufunga matuta 3-2, shukrani kwa mikwaju ya waheshimiwa Yona Kimube, Amos Makalla na Kikula Abel. Waliokwamisha mpira wavuni kwa upande wa timu ya Yanga ni waheshimiwa Michael Kadege na Sadigo Juma.
NENO LA SHIGONGO, NAPE, ZITTO
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, waandaaji wa tamasha hilo, Eric Shigongo alipanda jukwaani na kutoa nasaha zake kwa dakika kadhaa, aliwasihi Watanzania kurejesha mapenzi kwa nchi yao na kufufua matumaini mapya ya mafanikio.
Naye Katibu wa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye aliwashukuru wote waliohudhuria tamasha hilo na kueleza kuwa wameshiriki katika mkakati wa kuchangia ujenzi wa mabweni. Kwa upande wake, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe naye aliwashukuru wote kwa kushiriki kwenye kampeni ya kuzisaidia shule za vijijini kupata mabweni, burudani ikaendelea.
ZAMU YA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA
Baada ya mapambano hayo ya soka, burudani iliendelea ambapo Juma Kassim Kiroboto ‘Nature’ aliwaamsha mashabiki vitini, akafuatiwa na kundi la muziki la Pah One linalofanya muziki pande za Bondeni (Afrika Kusini). Burudani ikaendelea kwa wasanii wengine kama Rashid Makwilo ‘Chid Benz’ kupanda na kupafomu kwa kiwango cha juu.
WEMA VS WOLPER, NGOMA DROO
Warembo waliolikamata soko la filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper na Wema Sepetu nao walitia fora kwa pambano lao kali la masumbwi. Pambano hilo la raundi tatu ambalo lilitarajiwa kumaliza bifu la siku nyingi kati ya wanyange hao, lilitanguliwa na pambano kati ya Kanda Kabongo na Ramadhan Kido, lililomalizika kwa Kabongo kushinda kwa pointi. Mpaka pambano la Wema na Wolper linamalizika kwa droo, uwanja mzima ulikuwa ukishangilia kwa nguvu.
Katika tukio lingine lililowashangaza wengi, baada ya Wema kumaliza pambano, shabiki mmoja ambaye hakufahamika alikotokea, alimvamia msanii huyo akiwa anateremka ulingoni na kumkumbatia kwa nguvu lakini kabla hajamdhuru msanii huyo, polisi walimdaka juujuu na kumshushia kichapo cha haja kabla ya kutolewa nje mzobemzobe.
CHAMELEONE AACHA GUMZO NA VALUVALU
Baada ya mapambano ya ndondi, msanii mkali kutoka nchini Uganda, Joseph Mayanja ‘Chameleone’ aliingia kwa staili yake uwanjani hapo ambapo umati wote ulilipuka kwa shangwe za nguvu wakati msanii huyo akikamua wimbo wake unaobamba kwa sasa, Valuvalu na nyingine nyingi. Mpaka msanii huyo anamaliza shoo, kila mtu alikuwa amesuuzika moyo vilivyo kutokana na burudani ya nguvu aliyoiangusha.
DIAMOND KAMA KAWAIDA YAKE
Yote tisa, kumi ni shoo ya msanii anayeshikilia tuzo tatu za Kili, Naseeb Abdul ‘Diamond’ ambaye baada ya Chameleone kumaliza shoo, aliingia kwa mbwembwe za hali ya juu.
Wacheza shoo wake waliingia na njiwa weupe ambao waliwaachia uwanjani hapo kabla ya kuanza makamuzi. Diamond aliendeleza makamuzi ya nguvu na kuwadatisha vilivyo maelfu ya mashabiki waliofurika ukumbini humo.
Mpaka inatimu saa sita za usiku, kila aliyehudhuria uwanjani hapo alikuwa ametosheka kwa kiwango kikubwa na burudani ya nguvu iliyoangushwa uwanjani hapo kuanzia saa mbili za asubuhi.

source:globalpublishers

MUME WA JACK PATRICK AHENYA KORTINI

Leave a comment


MUME wa mwanamitindo maarufu Bongo, Jacqueline Patrick, Abdulatif Fundukira (pichani katikati), Jumatatu iliyopita alihenya kusaka dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na ombi lake kutupiliwa mbali, Risasi Mchanganyiko linahabarisha.
Abdulatif alifikishwa mahakamani hapo akitokea mahabusu katika Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam kutokana na tuhuma za kuhusika katika biashara ya madawa ya kulevya.
Mtuhumiwa huyo akiwa na wenzake watano baada ya kupandishwa kizimbani, aliiomba mahakama hiyo impatie dhamana lakini hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Riyad Chamshama alimwambia kuwa kulingana na uzito wa kesi yake hawezi kupata dhamana na kumtaka kupeleka madai yake mbele ya sheria kama ataona kuna umuhimu wa kufanya hivyo.
Baada ya kupewa jibu hilo Abdulatif aliiomba mahakama hiyo impatie nakala ya mwenendo wa kesi hiyo kwa ajili ya matayarisho ya kulipeleka shauri hilo mbele ya sheria ili kupata dhamana ambapo aliambiwa atapatiwa wakati kesi hiyo itakapotajwa tena.
Hakimu Chamshama aliihairisha kesi hiyo hadi Julai 16, mwaka huu itakapotajwa tena Mahakamani hapo.
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki waliofika mahakamani hapo walisikika wakijadili kitendo cha mke wa Abdulatif, Jack Patrick ambaye aliwahi kuingia katika kinyang’anyiro cha kumsaka Miss Tanzania miaka ya nyuma kutoonekana mahakamani hapo.
“Inawezekana kuwa ameamua kumtosa mume wake?” alihoji mmoja wao huku wengine wakisema huenda mlimbwende huyo ametingwa na mambo muhimu.

source:globalpublishers.

Mwinyi: Machozi Band ubabaishaji mwingi

1 Comment


Aliyekuwa mwimbaji wa bendi ya Machozi inayomilikiwa na mwanadada Lady Jaydee amesema sababu za kujiondoa kwenye bendi hiyo ni kutokana na ubabaishaji mkubwa unaoendelea.
Akiongea na Clouds Fm jana, Mwinyi amesema hakufukuzwa kwenye bendi hiyo bali aliamua kuondoka mwenyewe baada ya kuchoshwa na ahadi za uongo kutoka kwa uongozi wa bendi hiyo.
Amesema kuwa kwa muda mrefu ameuvumilia ule aliouita ‘mkataba wa kijinga’ aliokuwa anautumikia kwa malipo ya kila mwisho wa wiki ambayo hata hivyo yalikuwa kiduchu na wakati mwingine alikuwa hakuti bahasha yake.
Mwinyi ambaye pia ni model, alieleza kuwa pamoja na bendi nyingi kutangaza nia ya kumchukua kwa ahadi za mkwanja mrefu, aliendelelea kuuvumilia ‘uswahili’ wa Machozi bendi na heshima yake kwa Lady Jaydee huku akiimba ‘for fun tu’.
Amesema Lady Jaydee alikuwa akimwonesha dharau kubwa na kujiona yuko juu wakati bendi yakeisingefika hapo ilipo bila ya mchango wake.
Mwimbaji huyo aliongeza kwa kusema kuwa sifa za nje za bendi hiyo ni kubwa lakini ukweli wa ndani ni kuwa haina lolote zaidi ya uswahili na ubabaishaji mwingi.
Mwinyi si msanii pekee aliyejitoa hivi karibuni kwenye bendi hiyo ya Machozi.
Mwimbaji mwingine aitwaye Sam ameamua kwenda kutafuta riziki kwenye bendi ya Skylight inayomilikiwa na mshiriki wa zamani wa Tusker Project Fame,Aneth Kushaba kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya shilingi milioni sita.
Clouds Fm walipojaribu kumpigia simu Gadner Habash kuelezea masuala hayo aliwapa jibu la ‘NO COMMENT’.

source:.bongo5

Kuwa makini na story za mtandao wa Global Associated News!

2 Comments


Hivi karibuni hujasikia watu wakiulizana, “umesikia 50 Cent amekufa kwa ajali ya gari?” Na kwa wale waandishi wenye allergy na ‘Google’ huenda moja kwa moja kwenye blog zao na kuandika kichwa cha habari kwa mbwembwe nyiiiingi kuwa ana breaking news kuwapa wasomaji wake, “50 Cent hatuko naye tena, afa kwa ajali mbaya ya gari,” kumbe kaingia chaka! Akisikia kuwa zilikuwa ni story za uzushi tu, anageuka kuwa mdogo kama pilton na siku inaharibika.
Kiukweli mchezo huu sasa hivi umekuwa maarufu sana na wengi wanaingia mkenge kwa kufikiria ni kweli. Kumbe ni wapuuzi fulani tu ambao wameamua kucheza na akili za watu. Ni ngumu kujua lengo lao, kwakuwa tukisema wanataka kuongeza traffic ya wasomaji kwenye website yao tunapata mashaka kuamini kwasababu wanatumia story hiyo hiyo moja, picha ile ile,halafu wanabadilisha tu majina.Leo watasema 50 Cent, kesho Usher,kesho kutwa Drake lakini story ni ile ile neno kwa neno!
So leo blog moja iitwayo sambweti.blogspot.com imeandika story yenye kichwa cha habari: Breaking news…………..Usher Dies In Car Cras! Akimaanisha ‘Crash’
Kwa kujiamini akaweka msisitizo, “follow the link its tell all about the accident and if you will not satisfy the words just go the bottom of the story there is another link go ahead”
Ni rahisi kutambua ni mwandishi wa aina gani kutokana na kiingereza chake hapo juu!
Anyways, story hizi zinasambazwa na mtandao uitwao Global Associated News!
Huu ndo mfumo wa jinsi story hiyo wanavyoiandika:
THIS STORY IS STILL DEVELOPING…
(Local Team News 9) Usher died in a single vehicle crash on Route 80 between Morristown and Roswell. He was pronounced dead at the scene by paramedics responding to the vehicle accident and was identified by photo ID found on his body. Alcohol and drugs do not appear to have been a factor in this accident – June 26, 2012
Highway Safety Investigators have told reporters that Usher lost control while driving a friend’s vehicle on Interstate 80 and rolled the vehicle several times killing him instantly.
The vehicle was believed to have been traveling at approximately 95 miles per hour in a 55mph zone at the time of the accident.

Witnesses have stated that Usher’s car crossed the double lines several times prior to the accident and hit the center lane divider causing the vehicle to flip and roll.
Toxicology tests will be performed to determine whether he was driving under the influence, however initial findings indicate that durgs or alcohol did not contribute in any way to this accident as it was more likely to been caused by road conditions.
Memorial services for Usher have not yet been announced. The service is expected to be a closed casket funeral due to the severe head trauma.
Additional details and information will be forthcoming as they become available.
Ushauri: Tujitahidi kutumia Google kuthibitisha masuala ya msingi kabla hatujayasema ama kuandika.

source:bongo5

Wadau Kumradhi kwa picha hizi:lori laua wawili na kujeruhi vibaya wengine nane kibaoni-tegeta jijini Dar jana.

Leave a comment


Wananchi wa eneo la Tegeta Kibaoni, jijini Dar es Salaam wakisaidiani na polisi kuupakiza mwili wa mmoja wa mwananchi kwenye gari kati ya watu waliokufa katika ajali iliyotokea baada ya Lori la mchanga kupata hitilafu ya breki na kuacha barabara na kugonga Daladala kabla ya kuvamia baa na kusababisha vifo vya watu wawili papo hapo na wengine nane kujeruhiwa jana


Wananchi wa eneo la Tegeta Kibaoni, jijini Dar es Salaam wakijaribu kutoa mwili wa mmoja wa mwananchi kati ya watu waliokufa katika ajali iliyotokea baada ya Lori la mchanga kupata hitilafu ya breki na kuacha barabara na kugonga Daladala kabla ya kuvamia baa na kusababisha vifo vya watu wawili papo hapo na wengine nane kujeruhiwa jana

OMOTOLA KUZINDUA SUPERSTAR YA WEMA GIRAFFE HOTEL

Leave a commentNi onyesho maalum la familia.
MKALI wa filamu nchini Nigeria na Afrika, Omotola Jalade atazindua filamu ya Wema Sepetu Jumapili hii katika Ukumbi wa Hoteli ya Girafee Ocean View, iliyopo Mbezi Beach.Filamu hiyo iitwayo Super Star imechezwa na Wema, ikionyesha maisha ya mtu maarufu na changamoto anazozipata ikiwemo kuandikwa mambo mbalimbali ikiwemo taarifa za vyombo vya habari.

Katika uzinduzi huo, bendi kutoka Tanzania House Of Talent (THT) watatoa burudani, kabla ya mashabiki kupata nafasi ya kupiga picha na msanii huyo. Omotola, ambaye ni mke wa rubani Kapteni Matthew Ekeinde, ambao walifunga ndoa yao angani kwenye ndege atatoa nafasi ya kupiga picha na watu kadhaa.

Katika uzinduzi huo, pamoja na burudani ya muziki, mashabiki watakaofika hapo, watapata pia fursa ya kuiona filamu ya Super Star katika viwanja hivyo vya hoteli hiyo iliyoko ufukweni. Omotola ambaye yuko kwenye ndoa kwa miaka 16 akiwa na watoto wanne, ana jumla ya albamu mbili za muziki.

Msanii huyo ambaye mwaka jana alitangaza kuachana na kucheza filamu kutokana na kuandikwa vibaya, anatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kwenye uzinduzi huo ambao kiingilio kitakuwa Sh 30, 000 kwa wakubwa na watoto 10,000.

Taifa Stars yarejea nyumbani salama

Leave a comment


Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es Salaam jana usiku wakitokea nchini Msumbuji waliposhiriki katika Mchezo wa mtoano wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika CAF. Taifa Stars ilitolewa katika michuano hiyo kw kufungwa kwa mikwaju ya penati na Msumbiji 8-7.

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ wakiwa ndani ya basi mara baada ya Kuwasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es Salaam jana usiku wakitokea nchini Msumbuji waliposhiriki katika Mchezo wa mtoano wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika CAF. Taifa Stars ilitolewa katika michuano hiyo kw kufungwa kwa mikwaju ya penati na Msumbiji 8-7.[caption id="attachment_2111" align="alignleft" width="500"] Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa, Kim Polsen akizungumza na Sunday Kayuni mara baada ya kuiwasili uwanjani hapo.


[/caption]

Photosource:mrokim

Older Entries

%d bloggers like this: