Home

AFANDE SELE AKIFUNGUKA KUHUSU SHOW YA ZANZIBAR MUSIC AWARD

Leave a comment


Salaam Ndugu zangu wote mashabiki na wadau wa muziki wetu!!
Tamko langu kuhusiana na lugha zilizotolewa na Twent Percent kuhusiana na show yetu ya Zanzibar Music Award.
“Tulialikwa kwenye ZANZIBAR MUSIC AWARD, na kabla ya kazi makubaliano yote ya kazi kwa mujibu wa mkataba yalifuatwa, makubaliano hayo yalihusisha sisi kujigharamia gharama zote za nauli na Malazi (accomodation).
Tulifika Zanzibar salama, tulipokua Zanzibar twenty alitaka agharamiwe huduma zote ambazo ni nje ya mkataba wetu, nikamuomba na kumsihi sana Ndugu yangu aheshimu mkataba, asitafute matatizo kwani tayari mpaka wakati huu tuna kesi na Halmashauri ya Manispaa ya Moro ambayo kimsingi sikuhusika (nilishatolea ufafanuzi siku za nyuma).
Lakini yeye alipingana na mimi, akanibishia na kunisukuma Mbele ya wageni na wenyeji wetu, wakiwemo Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seiph Ali Idi, Waziri Seiph Khatibu.
Walikuwepo waadishi wa habari wa siku Nyingi Akiwemo Abubakari Liongo (idhaa ya kiswahili radio Ujerumani), Mkurugenzi wa ZENJI FM ndugu Tua Saidi Tua.
Mimi Selemani Abdallah Juma Msindi sihusiki kwa namna yoyote, na tabia zisizo za kuridhisha zinazoonyeshwa na Ndugu yangu Twenty Percent, ambae nimekua nae nyumbani kwangu hata kabla ya Tuzo zake Tano (Kili Music Award) ambazo kazi hizo zote hizo kaandikia nyumbani kwangu siwezi kuwa na tatizo nae ni ndugu yangu kiimani na kikazi, hata kazi yangu niliyofanya nae kabla siku za nyuma “MBELE YAKO NYUMA YANGU” .. Kuna mstari Nilisema ” ..Kuandika Rhyme kwenda Gym kimtindo kuonyesha Ugum, bado unatakiwa uwe na nidhamu ya kweli, sio ya kumzuga Mwalimu, utajihukumu”.
Nimekua nikisisitiza nidhamu kwa Ndugu zangu woote toka enzi za Ghetto BoyZ, Watupori na Mabwasha’Kingdom, ambao wengine hawafanyi sanaa, ila nipo nao kwenye Familia yetu kubwa hapa Tanzania. Nimesikitishwa na kitendo hicho. Siku zote nimekua mwenye kuhitaji suluhu kwa namna ya Amani.
Verry sorry kwa wote ambao mumefadhaika kwa hilo. Tuendelee kuwa pamoja na msisite kutoa ushauri wenu, maoni ili Game letu lisonge. MUNGU ATUBARIKI.
Asanteni sana.
Selemani Juma Abdallah Mutabhazi Msindi.
a.k.a Afande Sele (King of Rhymes)

source:

Madaktari 72 wasimamishwa kazi kwa Mgomo

Leave a comment


Mwenyekiti wa Bodi Kaimu [caption id="attachment_3013" align="alignleft" width="500"] Mkurugenzi wa wa hospitali ya rufaa Mbeya Dr E. Sankey akimsikiliza kwa makini kaimu mkuu wa mkoa Mbeya.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Norman Sigara Aikzungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu kusimamishwa kazi kwa madaktari hao.[/caption]BODI ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, imewasimamisha kazi madaktari 72 kwa kosa la kutoingia kazini kwa siku tano jambo ambalo ni kinyume cha makubaliano ya mkataba.

Imeelezwa kuwa madaktari hao ambao 54 ni wale wa mafunzo ambao waliingia mkataba wa miaka miwili na hospitali ya Rufaa na madaktari 18 ni wale walioajiriwa na Wizara ya afya.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Bodi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Norman Sigara, alisema kitendo cha madaktari kutoripoti kazini kwa siku tano ni ukiukwaji wa kanuni za utumisha wa umma toleo la 2009 kifungu namba F.16-F17 na F. 27.

“Hivyo kupitia kanuni hiyo madaktari hao wamesimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa hatua zaidi za kinidhamu,”alisema Sigara.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wa Bodi, imeelezwa kuwa siku ya tarehe 23/6/2012 wafanyakazi 15 waliokuwa zamu(Intern Doctors 12 na Registrars3) hawakufika kazini na tarehe 24/6/2012 wafanyakazi 19(Intern doctors 15 na Registrars 4) hawakufika kazini.

Alisema, kuanzia tarehe 25/6/2012 hadi leo imethibitika kuwa Interns doctor 54 na Registrars 18 hawakufika kazini hadi leo tarehe 28/6/2012 ambapo tarehe 25/6/2012 bodi ya hospitali ilifanya kikao cha dharura kujadili hali ya utendaji kazi na utoaji huduma hospitalini na kutoa uamuzi.

Sigara, aliyataja maamuzi hayo kuwa ni Mwenyekiti wa Bodi akutane na madaktari ambao hawakufika kazini ili awasikilize sababu za kutofika na kujadili namna ya kumaliza matatizo hayo jambo ambalo madaktari hao waligoma.

Alisema, baada ya madaktari hao kukaidi ombi hilo, Bodi ya hospitali ili waandikia barua za kujieleza kwanini wasichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuvunja mkataba walioingia na hospitali na pia kukiuka
kanuni za kudumu za utumishi wa umma nalo walilikaidi

“Iwapo madaktari ambao hawakuripoti au kueleza sababu za kuridhisha ifikapo tarehe 28/6/2012. Kwa kuzingatia kanuni za utumishi wa Umma, madaktari hao watasimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,”alisema.

Aidha, alisema kuwa kwa ujumala madaktari hao waligomea barua zote mbili yaani ya kuitwa kwenye kikao pamoja na ile ya kuwataka kujieleza hivyo Bodi imechukua hatua za kisheria za kuwafukuza kazi.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa bodi, alisema kuwa tayari hospitali ya Rufaa kwa ushirikiano wa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, madaktari watano wamepatikana ili kusaidia huduma kwa hospitali hiyo.

Mwinyi: Machozi Band ubabaishaji mwingi

1 Comment


Aliyekuwa mwimbaji wa bendi ya Machozi inayomilikiwa na mwanadada Lady Jaydee amesema sababu za kujiondoa kwenye bendi hiyo ni kutokana na ubabaishaji mkubwa unaoendelea.
Akiongea na Clouds Fm jana, Mwinyi amesema hakufukuzwa kwenye bendi hiyo bali aliamua kuondoka mwenyewe baada ya kuchoshwa na ahadi za uongo kutoka kwa uongozi wa bendi hiyo.
Amesema kuwa kwa muda mrefu ameuvumilia ule aliouita ‘mkataba wa kijinga’ aliokuwa anautumikia kwa malipo ya kila mwisho wa wiki ambayo hata hivyo yalikuwa kiduchu na wakati mwingine alikuwa hakuti bahasha yake.
Mwinyi ambaye pia ni model, alieleza kuwa pamoja na bendi nyingi kutangaza nia ya kumchukua kwa ahadi za mkwanja mrefu, aliendelelea kuuvumilia ‘uswahili’ wa Machozi bendi na heshima yake kwa Lady Jaydee huku akiimba ‘for fun tu’.
Amesema Lady Jaydee alikuwa akimwonesha dharau kubwa na kujiona yuko juu wakati bendi yakeisingefika hapo ilipo bila ya mchango wake.
Mwimbaji huyo aliongeza kwa kusema kuwa sifa za nje za bendi hiyo ni kubwa lakini ukweli wa ndani ni kuwa haina lolote zaidi ya uswahili na ubabaishaji mwingi.
Mwinyi si msanii pekee aliyejitoa hivi karibuni kwenye bendi hiyo ya Machozi.
Mwimbaji mwingine aitwaye Sam ameamua kwenda kutafuta riziki kwenye bendi ya Skylight inayomilikiwa na mshiriki wa zamani wa Tusker Project Fame,Aneth Kushaba kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye thamani ya shilingi milioni sita.
Clouds Fm walipojaribu kumpigia simu Gadner Habash kuelezea masuala hayo aliwapa jibu la ‘NO COMMENT’.

source:.bongo5

MISS UNIVERSE TANZANIA 2012 KUSAKWA IJUMAA MAKUMBUSHO YA TAIFA.

Leave a comment


Maria Sarungi Tsehai

Mashindano ya kumsaka mrembo wa Miss Universe Tanzania 2012 kitafanyika Ijumaa hii kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa yaliyopo Posta jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai alisema jana kuwa mashindano hayo yatashirikisha jumla ya warembo 20 kutoka katika mikoa mbali mbali ya Tanzania Bara.
Mikoa hiyo ni Manyara, Arusha, Dodoma, Mwanza, Mtwara, Kilimanjaro na wenyeji Dar es Salaam na kuongeza warembo wote wanaendelea na mazoezi chini ya wakufunzi walioboea katika masuala ya urembo.
“Tunatarajia kuwa na mashindcano bora ili kuweza kumapata mrembo ambaye atatupa sifa katika mashindano ya kimataifa kama ilivyokuwa kwa Flaviana Matata mwaka 2007 ambapo alishika nafasi ya saba katika mashindano yaliyofanyika nchini Mexico,” alisema Maria.
Maria aliwataja warembo hao kuwa ni Bahati Chando, Aisha Maulidi, Catherine Mpulule, Cecilia Moses, Consolata Mosha, Devotha Keregese, Doris Mollel, Doreen Mapunda na Edith Tesha.
Wengine ni Getrude Asanterabi, Jescha Tiba, Kundi Mligwa, Lilian Kolimba, Mary Joel, Naomi Joseph, Nyaso Malilo, Neema Mpanda, Susan Manoko, Theodora Msenya na Winfrida Dominic.
Alisema kuwa shindano hilo limedhaminiwa na gazeti la The Citizen, gazeti dada la Mwananchi kwa kushirikiana na wadhamini wengine, Le Grand Casino, Urban Rose Hotel, Amina Design, Dodoma Hotel na New York Film Academy.
Maria alisema kuwa shindano hilo litaanza saa 1.00 usiku kwa warembo hao kupita jukwaani wakiwa katika aina mbalimbali za mavazi kama vile ya ubunifu na lile l;a usiku.
Alisema kuwa maandalizi kwa ajili ya shindano hilo kubwa la urembo yamekamilika na kinachosubiliwa ni siku ya shindano hili kupata mrithi wa Miss Universe anayemaliza muda wake Nelly Kamwelu.
Alifafanua kuwa wameboresha mashindano ya mwaka huu na wanatarajia kuwa na mashindano bora kabisa tofauti na ya miaka ya nyuma.

source:dewjiblog

Matarajio ya kupata mshindi kutoka Tanzania katika mashindano ya Tusker Project Fame msimu wa tano jana yafikia ukingoni

Leave a comment


Matarajio ya kupata mshindi kutoka Tanzania katika mashindano ya Tusker Project Fame msimu wa tano jana yamefutika rasmi baada ya mshiriki aliyekuwa amesalia kutoka Tanzania kutoka.
Damiani Innocent Mihayo alifungasha virago jana baada ya jitihada zake za kuonesha kuwa aliingia kwenye probation kwa bahati mbaya kugonga mwamba. “Damian is Good…Bad choice ya nyimbo aliyoimba,he also lacks star quality,” aliandika mfuatiliaji mmoja wa mashindano hayo.
“Huyu jamaa (Damian) like two weeks ago alichemka mistari ya Ali Kiba, shame! Aaaa project fame alikua Lina, Msechu na kidoooogo Aneth, yaani hata Hemedi namsifu, he knew how to play the game. Ndo makosa tunafanya hata BBA. Watu kama Hemedi au hata Wema ni watu wanajua kucheza na ni rahisi watanzania kutoa support. Hilda na Julio ppphhheeeew,” aliandika mwingine aitwaye Yvonne kupitia Facebook.
Kutokana na kutolewa kwa Damian sasa watanzania watabakia kuwashuhudia tu washiriki kutoka Uganda, Kenya, Sudan Kusini, Rwanda na Burundi katika shindano hilo. Katika hatua nyingine wiki hii Universal Music Group (UMG) imeingia mkataba na shindano hilo ambapo itamsimamia mshindi wa mwaka huu. Pia itasimamia kurekodi albam ya pamoja ya washiriki kumi bora wa mwaka huu.

Hussein Machozi kuhamia Kenya kimoja

Leave a comment


Mwanamuziki wa Tanzania aliyetamba na vibao kama ‘Kwaaajili Yako’ na ‘Full Shangwe’ Hussein Machozi, amesema anafikiria kuhamia kabisa Kenya kwakuwa anahisi muziki wake unathaminiwa zaidi huko kuliko nyumbani.
Akijibu swali la Bongo5 lililotaka kufahamu kama ana mpango huo kwakuwa ni muda mrefu sana sasa amekuwa akiutumia nchini Kenya kuliko Tanzania, Machozi alisema,”Yap naona pananifaa sana kwa muziki wangu ambao hauna unafiki si unajua watu wa huku sio wanafiki.”
Kwanini anasema Tanzania kuna unafiki? “Okay, watu wa media hawako free kabisa yaani huwa wanafuata upepo wanapoanzisha wale wenye nguvu. Yaani wakitaka kumtoa mtu wao na media zingine zinafuata wala hawashtuki kuwa analazimishwa atoke, wakati kuna ngoma kibao kali wanazipotezea ili mtu wao apite. Matokeo yake wanatoaga ngoma moja inahit baada ya hapo ni pumba tupu. Huwa inaniuma sana.”
“Kwa kenya mambo hayo hakunaga asee! Huku kama ngoma ni kali basi itatandikwa hadi noma, ila kama ni mbaya huwezi hata kuiskia. Nakubalika huku coz ngoma zangu ni kali na zina kichwa na miguu namaanisha wimbo uko na story ya kufuatilia na inaskilizika na rika zote, nadhani hii ni sababu tosha sana,” alisema Machozi.
Msanii huyo tayari ameshafanya ngoma na wasanii wa Kenya wakiwemo Habida,Size 8 na DNA.

SIMBA 6 WAULIWA NAIROBI NATIONAL PARK, WAUWAJI KUPAMBANA NA MKONO WA SHERIA

Leave a comment


Polisi na mamlaka ya wanyama pori nchini Kenya wapo katika msako mkali kuwatafuta wakazi wa Kitengela walioua simba sita kutoka hifadhi ya taifa ya Nairobi.

Simba hao wanaodaiwa kuvamia na kuua kondoo 28 siku ya jumatano asubuhi.

Mkurugenzi wa huduma za wanyama pori Julius kipng’etih amedhibitisha mauaji hayo ya simba 6 na kondoo 28, na kusema Simba hao walipotea kutokea hifadhi ya Nairobi.

“nilazima tuwakamate waliohusika na mauaji haya ya Simba, wanapaswa kupambana na sheria” alisema mkurugenzi huyo.

Simba hao waliua ng’ombe 8 siku ya jumatatu, na hivyo wakazi wa eneo hilo kukosa uvumilivu baada ya Simba kuua tena kondoo siku ya jumatano.

Older Entries

%d bloggers like this: