Home

ROMA APATA AJALI MBAYA NA GARI LAKE AKIELEA MOROGORO KWENYE SHOW

1 Comment


Muda mchache uliopita msanii wa kizazi kipya kwenye bongo hip hop ROMA amepata ajali mbaya barabara ya Morogoro. Roma anasema alikuwa yupo kwenye mwendo wakawaida ndio tairi la mbele lilipopata pancha na ndipo gari likaacha njia yake na kwenda kugongana uso kwa uso na fuso ambalo lilikuwa upande wa pili na gari hilo dogo alilokuwa akiendesha Roma kurudi lilipotokea.
Roma ananiambia kwa sasa anaelekea Hospital kwa check up zaidi ila aliokuwa nao kwenye gari hakuna aliyeumia wote ni wazima.
Roma akimwelezea police wa usalama barabarani kilichotokea mpaka kupata ajali hiyo mbaya.
 Huyu ni mmoja kati ya marafiki wa Roma aliyekuwa nae kwenye gari wakielekea Morogoro kwenye show

source:djchoka

PICHA ZA MATUKIO YA UOKOAJI WA ABIRIA WALIOZAMA KWENYE MELI YA MV STAR GATE.

Leave a comment


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akiwa katika Eneo la Bandari akishuhudia kuletwa kwa majeruhi mbalimbali waliookolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Amer Kificho pamoja na mawaziri mbalimbali wakiwa katika Eneo la Bandari wakishuhudia kuletwa kwa majeruhi mbalimbali waliookolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.

Majeruhi alieokolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.

Majeruhi wakipatiwa Mablangeti kwa ajili ya kujihifadhi baada ya kuokolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.

Raia wa kigeni waliookolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.

Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Hamad Masoud Hamad akiwa katika hali ya huzuni Baada ya kushiriki katika uokoaji na kuwaona Majeruhi waliookolewa katika Meli iliozama ya Star Gate wakiteremka Bandarini Zanzibar.

Wananchi wakiwa wamekusanyika eneo la Bandari mjini Zanzibar kuona ndugu zao waliookolewa wakiwa hai na waliofariki katika ajali hiyo.

Askari wa Vikosi mbalimbali wakiwa katika kazi ya Uokozi kwa Abiria waliokuwa katika Meli ya Star Gate ambayo iliozama katika ikiwa imebeba abiria 250 huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar.

Daktari akitoa huduma ya kwanza kwa mmoja wa majeruhi wa boti iliozama ikiktokea Dar-es-Salaam kuelekea Zanzibar.

Abiria waliookolewa kutoka katika meli iliozama ya Star Gate katika bahari ya Chumbe Zanzibar.PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR

HII NDIO NDEGE NYINGINE YA CLUB YA TP MAZEMBE.

1 Comment


Hii ni moja kati ya ndege zinazomilikiwa na club ya soka ya Congo DRC Tp Mazembe ambayo wanacheza Watanzania Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu, ndege nyingine waliyonayo ndio ilipata ajali ndogo zaidi ya wiki mbili zilizopita na wachezaji wote kunusurika akiwemo Thomas Ulimwengu, ilisumbua wakati wa kupaa ikaingia porini kidogo.

Kwa nyuma hiyo ndege ndio inaonekana na maandishi ya IN GOD WE TRUST, ni mali ya club hiyo tajiri ya Congo DRC.

source:millardayo.

AJALI MBAYA YA BASI LA BUNDA IMETOKEA GEITA,WATU 11 WAFARIKI PAPO HAPO NA 12 WAJERUHIWA.

Leave a comment


MKUU wa mkoa wa Geita Magalula Said Magalula akiangalia miili ya marehemu waliokufa katika ajali ya Gari leo mchana Wilayani Geita,miili hiyo ilikuwa imelazwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya hiyo.Picha na David Azaria. (Source http://www.hakingowi.com/)

Watu wamefariki Dunia Papo hapo hapo na wengine 12 wakijeruhiwa vibaya baada ya magari matatu mawili kati yao yakiwa ni ya abiria waliyokuwa wakisafiria kupata ajali na kupinduka wilayani Geita Mkoani Geita.

Tukio hilo limetokea leo Jumapili majira ya saa 8:30 katika kijiji cha Chibingo kata ya Katoro eneo ambalo mwaka jana kulitokea ajali ya basi la Bunda na kuua watu 14 papo hapo na kujeruhi wengine 28.

Katika tukio hilo watu 9 wakiwemo watoto watatu wamekufa papo hapo,huku wengine wawili mmoja akifariki njiani wakati wa kukimbizwa hospitalini huku mwingine akifariki wakati akipatiwa matibabu na madaktari katika chumba cha Upasuaji.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Geita Paul Kasabago amelithibitihishia gazeti hili kuwepo kwa tukio hilo,na kueleza kuwa ajali hiyo ni mbaya nay a kwanza kutokea katika kipindi cha mwaka huu huku akitaja magari yaliyopata ajali kuwa ni zenye namba T 344 AZE zote aina ya Toyota Corola,na T 421 BHS Toyota land Cruiser.

Aliwataja waliokufa papo hapo katika ajali hiyo kuwa ni Maria Elisante (18) mkazi wa Mganza wilayani Chato,Masasila Benjamin (17) mkazi wa Mkolani mjini Geita,James Ntungirwenge (36) Mkazi wa Nyankumbu Geita,na Eliud Ngovongo (36) pamoja na watoto wake watatu Amin (10),Emison(7),na Sara(4) wote wakazi wa Kalangalala mjini Geita.

Alisema bado majina ya marehemu watatu mpaka jioni ya jana yalikuwa bado hayajatambuliwa,huku akibainisha kwamba tayari marehemu saba kati ya 11 waliofariki wametambuliwa na ndugu zao.

Kamanda Kasabago alisema katika tukio hilo watu 12 wamejeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya wilaya ya Geita,huku wanne kati yao ambao hali zao ilionekana kuwa mbaya wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando kwa matibabu zaidi.

Mganga mkuu wa Wilaya ya Geita Dk.Abdalah Dihenga jana aliwaongoza madaktari wengine kutoa huduma kwa majeruhi,ambapo mwandishi wa Gazeti hili aliwashuhudia wakitoa huduma kwa wagonjwa katika chumba cha upasuaji hospitalini hapo.

Akisimulia tukio kamanda Kasabago alisema chanzo cha ajli hiyo mbaya ni mwendo kasi wa magari mawili madogo ya abiria yajulikanayo kwa jina la ‘Michomoko’ ambayo yaligongana uso kwa uso na gari linguine aina ya Land Cruiser.

Kamanda Kasabago alisema magari hayo mawili yalikuwa yakifukuzana kutoka mjini Geita kwenda Katika mji mdogo wa katoro huku yakiwa na abiria,ambapo baada ya kufika katika eneo hilomoja liliamua kulipita lingine na ghafla likakutana na gari linguine mbele.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Said Magalula alifika katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Geita,na kushuhudia miili ya marehemu iliyokuwa imelazwa chini katika chumba hicho.

Akizungumza na mamia ya wananchi waliokuwa wamefurika nje ya Viwanja vya jingo hilo la kuhifadhia maiti katika hopspitali ya wilaya hiyo Mkuu huyo wa Mkoa alitoa pole kwa wafiwa,na kuwataka kuwa na moyo wa subira wakati wa maombolezo ya vifo vya ndugu jamaa na marafiki zao.

source:dewjiblog.

Tamko Maalum Kutoka CHADEMA Kuhusu Yaliyojiri Katika Mkutano wa Hadhara wa CHADEMA Uliofanyika Kata ya Ndago Siku ya Jumamosi Tarehe 14 Julai 2012

Leave a comment


Ofisa wa Sera na Utafiti CHADEMA Makao Makuu Bw. Waitara Mwita Mwikwabe


CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

Tamko Kuhusu Yaliyojiri Katika Mkutano wa Hadhara wa CHADEMA  Uliofanyika Kata ya Ndago Siku ya Jumamosi Tarehe 14 Julai 2012

1. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliandaa mikutano ya  hadhara katika Jimbo la Iramba Magharibi. Mikutano hiyo ilitolewa taarifa polisi na jeshi hilo lilitoa baraka zake kama utaratibu wa sheria unavyotaka kwa barua yake ya tarehe 12 Julai 2012 Kumb. Na. KIO/ B1/1/VOL.V/268

2. Mkutano wa kwanza ulipangwa kufanyika katika Kata ya Ndago katika  viwanja vilivyo karibu na kituo cha mabasi ambapo pia ni hatua chache karibu kabisa na Kituo cha Polisi Ndago. Mkutano huu ulipangwa kuanza saa nane mchana.

3. Msafara wa kitaifa unaofanya ziara ya ukaguzi wa chama, katika mkoa  wa Singida chini ya uratibu wa Ofisa wa Sera na Utafiti Makao Makuu, Mwita Mwikwambe Waitara, (ikiwa ni maandalizi ya operesheni nyingine kubwa mkoani humo itakayofanyika baadae), uliwasili katika eneo la  Mkutano majira ya saa tisa na nusu alasiri. Tulikuta wananchi wengi
wakiwa wanatusubiri. Kabla ya Mkutano kuanza tulipewa taarifa kwamba kuna kikundi cha vijana kimeandaliwa kuvuruga mkutano wa CHADEMA kwa kufanya fujo, ikiwemo kurusha mawe ili mkutano huo usifanyike. Suala hilo lilielezwa mkutanoni mapema na Mheshimiwa Waitara, mbele ya askari polisi.

4. Wakati tukijiandaa kuanza hotuba, vijana wapatao wanane walianza chokochoko kwa kutoa matusi na punde mawe yakaanza kurushwa kutoka sehemu mbalimbali. Wakati fujo zinaanzishwa na kile kikundi, Mheshimiwa Waitara alikuwa bado anazungumza na wananchi kuwaandaa kusikiliza wazungumzaji wengine. Vurumai hiyo ilizimwa na wananchi
wenyewe wa Ndago waliokuwa na hamu ya kusikiliza ujumbe wa viongozi wa kitaifa wa CHADEMA.

5. Kwa kweli tunawashukuru wananchi wengi wa Ndago walioonesha ujasiri  mkubwa kuweza kuwaondoa vijana wale eneo la mkutano, kisha mkutano ukaendelea, huku wananchi wakionesha kila hamasa ya kufurahia hoja kutoka kwa wazungumzaji, akiwemo Mheshimiwa John Mnyika, ambaye aliombwa ahudhurie ziara hiyo kwa nafasi yake ya Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA.

6. Mpaka tunamaliza mkutano huo ambao wananchi waliufurahia sana kwa  namna ulivyohutubiwa kwa amani na utulivu huku wazungumzaji wakijenga hoja juu ya mstakabali wa jimbo na taifa lao kwa ujumla, mamia ya wananchi waliohudhuria walitaka tuendelea kuhutubia, lakini tulibanwa na ratiba ya kuwahi mkutano wa pili, eneo la Kinampanda.

7. Lakini kutokana na vurugu hizo zilizokuwa zikisababishwa na kikundi  cha vijana ambao tayari ilishatolewa taarifa yao kwenye mkutano huo, lakini askari waliokuwepo hawakuthubutu kuchukua hatua, tulilazimika kuomba msaada kutoka kwa OCD na R.P.C, ambapo baadae wakati mkutano unakaribia kuisha tuliona gari la polisi kutoka Mjini Singida likiwa na askari waliojipanga rasmi kwa ajili ya kuzuia vurugu likifika pale
eneo la mkutano, lakini wakati huo hali ilishatulia na hotuba zimetolewa vizuri.

8. Kutokana na hali hiyo ya vurugu, zilitolewa taarifa Kituo cha  Polisi cha Ndago, ambapo lilifunguliwa jalada NDG/RB/190/2012. Katika jalada hilo tulitaja baadhi ya majina ya watuhumiwa waliokuwa vinara wa kundi lililokuwa likifanya fujo kwenye mkutano mbele ya askari polisi. Majina hayo ni; 1. Daniel Sima, 2. Tito Nitwa, 3. Bakili Ayubu, 4. Yohana Makala Mpande, 5. Ernest Kadege, 6. Abel John, 7. Athuman Ntimbu, 8. Martin Manase, 9. James Ernest, 10. Simion Makacha, 11. Anton John, 12. Frank Yesaya

9. Kwa hakika askari polisi wa Ndago waliokuwepo mkutanoni mbali ya  kutochukua hatua yoyote dhidi ya fujo tulizofanyiwa ikiwemo kupondwa mawe na kikundi kidogo cha wahuni, fujo zilipozidi askari wote walikimbia eneo la mkutano, akabaki OCS pekee ambaye naye alionekana dhahiri kutotaka kuchukua hatua stahili. Hakuonekana kufanya juhudi zozote za kuhakikisha amani inalindwa na ulinzi unaimarishwa katika eneo la mkutano na hatua zinachukuliwa dhidi ya watu walioonekana kudhamiria kufanya fujo.

 Mtu yeyote makini angeweza kuona kuwa askari wale walikuwepo pale mkutanoni ‘almuradi’ tu lakini kama vile walikuwa na maelekezo maalum ya kuhakikisha hawachukui hatua yoyote katika kuzuia mpango wowote wa kusababisha vurugu na kuvunja amani.

10. Baada ya kumaliza mkutano wa Ndago kwa amani, tulikwenda  Kinampanda ambako tulifanya mkutano mwingine mzuri kwa amani kabisa, ambapo mbali ya wananchi kuwa wametusubiri kwa hamu kubwa na kutusikiliza kwa makini hoja zetu, polisi katika eneo hilo walitupatia ushirikiano mzuri tangu wakati tunafika mpaka tulipomaliza mkutano
huo.

11. Jioni wakati tumerudi hotelini, tukasikia kuna taarifa  zinasambazaa kuwa kuna mtu/watu wamekufa katika eneo la Ndago. Habari hizo zilikuwa zinakanganya kwa sababu zilikuwa zikitaja idadi tofauti tofauti. Lakini kwa vyovyote vile kama ni kweli kuna tukio la mtu
kufariki, CHADEMA tunasikitika sana kwa tukio hilo la uhai wa mtu.

12. Tunalaani taarifa zinazozidi kusambazwa ambazo zinawataja polisi  kuwa wanatuhusisha CHADEMA na tukio la mtu aliyefariki. Hii ni ajabu kubwa kwamba tumetoka kwenye mkutano ule kwa amani kabisa mpaka tumemaliza mkutano wa pili kwa amani na polisi wakiwepo sehemu zote mbili, kisha tunasingiziwa masuala ambayo wenyewe hatukuwa na habari nayo tangu mkutano wa kwanza ukiwa unaendelea mpaka mkutano wa mwisho
ulipomalizika.

13. Kutokana na habari hiyo ya kifo cha mtu inavyoenezwa kwa  kuihusisha CHADEMA, tumebaini kuwepo kwa mbinu na mikakati ya chama tawala pia vyombo vya dola vikihusika kutaka kuwatisha wananchi waSingida, Watanzania wote wapenda mabadiliko na viongozi wa CHADEMA katika mkoa huu, wasifanye kazi ya kisiasa kwa kuwabambikizia tuhuma
na kesi na pia kuwafanya waonekane ni watu wa vurugu.

14. Tunapenda kusema hapa kuwa njama hizo hazitafanikiwa. Zitashindwa  kama zilivyoshindwa njama zingine zote ambazo zimekuwa zikifanywa na vyombo vya dola, viongozi wa serikali na chama tawala dhidi ya CHADEMA na vuguvugu la mabadiliko nchini.

15. Tunawataarifu wananchi kuwa ratiba ya kufanya Operesheni nyingine  kubwa katika Mkoa wa Singida, ikiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Willibrod Slaa, itafanyika baadae kama ilivyoazimiwa na kikao cha Kamati Kuu.


Imetolewa leo Singida, Julai 15, 2012 na;
Waitara Mwita Mwikwabe
Ofisa wa Sera na Utafiti CHADEMA Makao Makuu

source:fatherkidevu

JINSI JOSE CHAMELEONE ALIVYOANZA KUPATA MAFANIKIO KWENYE MAISHA, HIVI NDIVYO ANAVYOPATA PESA.

Leave a comment


Jose Chameleone (katikati) akiwa kwenye shooting ya moja ya video zake.

Baada ya kukutana na staa wa muziki kutoka Uganda Jose Chameleone nimegundua kuna mambo mengi nilikua nayasikia tofauti na kuyasoma ambayo yeye ameyazungumza tofauti kabisa.
Nilikua sijui, kumbe Chameleone alianza kuenjoy kuwa staa kuanzia mwaka 2000 japo alianza muziki 1995, 2003/2004 ndio alianza kupata pesa na hapo ndipo maajabu yalianza kutokea kwa kuanza kutimiza ndoto.Chameleone amesema “nilijenga nyumba yangu kwa miaka miwili ambapo 2005 ilimalizika na ikawa imegharimu shilingi milioni 200 -300 za kitanzania, wakati nilikua naijenga hiyo ndio pesa niliyokua nayo na nikasema kabla sijaipoteza acha nifanye kitu muhimu lakini Mungu akanibariki tena baada ya kujenga hiyo nyumba nikapata bahati nyingine nikaendelea na vitu vingine”
Exclusive na millardayo.com Mwimbaji huyu staa kutoka Uganda amesema vyanzo vyake vikubwa vya mapato kwa sasa ni kununua na kuuza ardhi, kuuza simu za mkononi ziitwazo Chameleone anazozitengeza China, kununua nyumba na kuziuza pia kupangisha nyumba.
kuhusu vyanzo vingine vya mapato Chameleone amesema “show pia zinatulipa sana Uganda japo siwezi kukwambia nalipwa bei gani kwa sababu sipendi kuonekana mtu wa kujisifia lakini kwa wiki moja naweza kupiga show mbili Kampala au Uganda, na kingine kinachotulipa sana ni Kampuni kubwa za biashara ambazo zikikuona una nguvu zinakuchukua na kukulipa vizuri kwa kufanya nao promoshen au mambo mengine ya mkataba wa biashara”

source:millardayo

KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI TIGO YAKUTANA NA BLOGGERS JIJINI DAR.

Leave a comment


Meneja wa Promosheni na Matukio wa Kampuni ya simu za mkononi TIGO Bw. Allan Shilla akizungumza na Bloggers katika hafla fupi iliyoandaliwa na Kampuni hiyo katika hoteli ya Kebby’s jijini Dar yenye lengo la kufahamina na kubadilishana mawazo ambapo wameahidi kuwa karibu na mitandao ya Kijamii inayokua kwa kasi katika kupashana habari pamoja na kutoa offer kemkem zikiwemo line za simu bure, huduma ya Mega Box kwa bloggers wote waliohudhuria na vifurushi vya kutumia bure kwa mwezi mzima.

Blogger Rajabu Mhamila mmiliki wa http://burudan.blogspot.com/ akijitambulisha mbele wafanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi TIGO pamoja na Bloggers wenzake.

Mmiliki wa http://othmanmichuzi.blogspot.com/ na msaidizi wa http://www.issamichuzi.blogspot.com/ Othmani Michuzi akitiririka wakati wa hafla hiyo.

Mmiliki wa mtandao wa http://missiepopular.blogspot.com/ Mariam Ndabagenda wakati wa utambulisho.

Baadhi Wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi TIGO.

Baadhi ya Wamiliki na wasimamizi wa Mitandao mbali mbali nchini wakiwa kwenye picha ya Pamoja wakati wa Tafrija Fupi iliyoandaliwa na Kampuni ya simu za Mkononi Tigo ambapo yenye lengo la kufahamiana na kujenga mahusiano mazuri.

PR Agencies wa TIGO kutoka kampuni ya Trinity wakijitambulisha kwa Bloggers.

Bloggers http://missiepopular.blogspot.com/ (Kushoto) na Mwanzilishi wa http://www.jamiiforums.com/ wakibadilishana mawazo.

source:dewjiblog

Older Entries

%d bloggers like this: