Home

MH. JANUARY MAKAMBA KUZINDUA RASMI SHIRIKA LA MAENDELEO BUMBULI, NI MIONGONI MWA AHADI ALIZOTIMIZA.

Leave a comment


Napenda kuwatangazia wana-Bumbuli kwamba ile ahadi niliyotoa wakati wa kampeni – ahadi ya kuanzisha Shirika la Maendeleo Bumbuli – imetimia.  Shirika limepata usajili, limefungua ofisi, lina watumishi wa mwanzo na tayari ipo miradi minne ambayo utekelezaji wake utaanza mara moja. Tutazindua Shirika hili tarehe 4 Agosti 2012, katika mkutano wangu na wana-Bumbuli waishio Dar es Salaam na mikoa ya jirani, na baadaye katika mikutano na wananchi jimboni Bumbuli.

Chimbuko

Nilipoamua kugombea Ubunge wa Bumbuli mwaka 2010, niliamua kwamba katika utumishi wangu kama Mbunge nitashirikiana na Wana-Bumbuli pamoja na marafiki na washirika wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi katika kuleta mageuzi ya kiuchumi na kijamii Bumbuli. Jimbo letu ni kati ya majimbo yaliyo nyuma kimaendeleo kwa kiasi kikubwa na hivyo kuhitaji jitihada za ziada – zaidi ya zile za Serikali. Katika kufikia lengo hilo, niliahidi kuanzisha Shirika litakaloratibu shughuli za maendeleo katika Jimbo.

Nilifikia uamuzi wa kuanzisha Shirika nikitambua kwa dhati uwepo wa  jitihada nzuri za serikali katika kuboresha maisha ya watu wa Bumbuli nikitegemea pia serikali kuendeleza jitihada zaidi. Hata hivyo natambua kwamba kazi ya maendeleo si kazi ya serikali pekee, inahitaji ushiriki wa kila mmoja na hasa sekta binafsi ili kuisadia juhudi za serikali kufikia malengo ya maendeleo. Nilitaka kuchambua uwezo wa watu binafsi, wafanyabiashara na taasisi mbalimbali katika kupanua wigo wa ajira na shughuli za kipato kwa watu wa Bumbuli kupitia uwekezaji katika jamii.

Mpango wa Mageuzi Bumbuli

Mpango huu ulitokana na mawazo niliyokuwa nayo nilipoamua kugombea ubunge juu ya haja kuunganisha jitihada za wenyeji wa Bumbuli, wafanyabiashara na taasisi za hapa nchini, na wawekezaji kutoka nje katika kufanikisha mageuzi ya kijamii na kiuchumi. Niliamini jitihada za sekta binafsi  zikioana na mipango ya maendeleo ya serikali kutachochea kasi ya ukuaji wa uchumi wa wana-Bumbuli na hivyo kupanua wigo wa ajira na shughuli za kibiashara za uzalishaji mali katika Jimbo.

Malengo ya mpango wa kuikwamua Bumbuli kupitia uwekezaji katika jamii ni kama ifuatavyo:

1. Kuongeza pato la wakulima wa Bumbuli kutokana na mazao wanayovuna kwa kuboresha mbinu za kilimo, mbinu za kuhifadhi mazao, na hatua mahsusi za kuongeza thamani ya mazao hayo (value-addition).

2. Kuwavutia wawekezaji kujenga taasisi au shule itakayokuwa na wanafunzi, walimu na wafanyakazi wengine watakaotumia bidhaa zinazozalishwa Bumbuli, hivyo kutengeneza ajira na fursa za kujiongezea kipato kwa wananchi.

3. Kuleta huduma za kifedha kwa kuanzisha taasisi ya fedha Bumbuli ambayo hatimaye itakuwa benki ya wananchi wa Bumbuli ambayo itatoa mikopo kwa masharti nafuu.

4. Kuchukua hatua mahsusi za kuhifadhi mazingira ya Milima ya Usambara kwani maisha na maendeleo ya kiuchumi ya watu wa Bumbuli yanategemea sana mazingira na mandhari ya milima ya Usambara.

5. Kuanzisha Shirika la Maendeleo Bumbuli litakalokuwa na jukumu la kubuni, kuratibu na kusimamia uendeshaji wa shughuli zilizoainishwa hapo juu. Shirika hili ndilo litakalokuwa kiini cha mtandao wa kijamii wa uchumi kwa Bumbuli.

Malengo haya yamekusudiwa kuwanufaisha wananchi kwa kuanzisha mtandao wa kimataifa wa kibiashara ambapo wadau mbalimbali watashiriki; na hatamu za uchumi zikishikiliwa na watu wa Bumbuli wenyewe.

Shirika la Maendeleo Bumbuli

Shirika la Maendeleo ya Bumbuli ni shirika la maendeleo lisilotengeneza faida lenye lengo la kukuza uchumi na kuchochea  maendeleo ya Jimbo.  Shirika hili limesajiliwa kama kampuni yenye ukomo wa dhamana, na litafanya biashara ili kulipia gharama za uendeshaji na faida inayopatikana itatumika kugharamia miradi ya maendeleo ili kufikia malengo ya kijamii ya Mkakati wa Mageuzi ya Uchumi wa Bumbuli. Shirika litakuwa na kazi zifuatazo;

1. Kuihamasisha sekta binafsi kushiriki katika maendeleo ya Bumbuli kwa kuwekeza katika maeneo mblimbali.  Uwekezaji huu utahusisha wafanyabiashara wa ndani na wale wa kigeni na Shirika litajihusisha zaidi katika kutoa msaada wa kitaalamu, na kuratibu mtandao wa kibiashara utakaoenea kuanzia ngazi ya wilaya, taifa na kimataifa.

2. Kubuni na kuitangaza ‘Chapa Lushoto’ (Lushoto Brand) pamoja na kutayarisha mafunzo kwa wakulima juu ya kutayarisha mazao yao ili yapate kuwa na thamani bora zaidi. Shirika hili litajenga mfumo utakaosaidia kununuliwa kwa mazao ya wakulima na masoko ya bidhaa, muundo utakaotumiwa na wafanyabiashara binafsi.

3. Kuvutia uwekezaji kwa njia ya kuitangaza Bumbuli pamoja na kuishauri halimashauri na serikali za mitaa kuhusu maeneo ya kuwekeza na miundombinu ya kuboresha ili kuvutia uwekezaji zaidi.

4. Kutafuta fedha kwa ajili ya uwekezaji wa kijamii na kibiashara na kutoa msaada wa kihuduma kwa makampuni ya biashara ya nyumbani na uwekezaji wa kutoka nje.

5. Kuratibu mipango ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya wadau mbalimbali wa maendeleo Bumbuli.

6. Kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika mpango wa Maendeleo na Mpango wa uwekezaji.

Shirika litaongozwa na bodi itakayokuwa na watu kati ya nane na kumi na moja na kuendeshwa na timu ya watu watano ambao watakuwa ni, Mkurugegenzi Mtendaji, Mweka Hazina, Wachambuzi wawili na Mhasibu.

Miradi ya Mwanzo ya Shirika la Maendeleo Bumbuli

1. 1.     Mradi wa Kituo cha Kukusanya, Kusafisha, Kugredi, Kupaki na Kutafuta Masoko ya Mboga na Matunda ya Bumbuli (Bumbuli Packing House)

Wilaya ya Lushoto, jimbo la Bumbuli likiwemo, inasifika kwa kilimo cha mboga na matunda. Hata hivyo, asilimia hamsini (50%) ya mboga na matunda yanayolimwa Bumbuli yanaharibika – kwa kutokufika sokoni au kutopata soko la uhakika. Hata yale mazao yanayonunuliwa, wakulima wanapata mapato kidogo sana ambayo hayaendani na thamani ya jasho lao.

Mradi wa Bumbuli Packing House, ambao utajiendesha kibiashara, una dhamira ya kumaliza tatizo hili. Pamoja na hili mradi huu utawawezesha wakulima kwa pembejeo – mbegu, mbolea, pampu, nk – na mafunzo ili wazalishe mboga na matunda bora zaidi ya kukidhi mahitaji ya soko la kimataifa.

Mradi huu, katika awamu ya kwanza, utagharimu shilingi milioni 780. Utafiti wa Kibiashara (Market Analysis Survey) umefanyika, Andiko la Kibiashara limekamilika. Na majadiliano na wadhamini kupata fedha hizi yamefikia mwisho ambapo ndani ya mwezi mmoja fedha hizo zitapatikana, na baada ya maandalizi kukamilika (ikiwemo kupata professional management), mradi utaanza.

 1. 2.     Mradi wa Kiwanda cha Kusindika Mboga na Matunda

Shirika liko katika hatua za mwisho za mazungumzo ya kukifufua upya kiwanda cha kusindika Mboga na Matunda (Natural Choice) kilichopo Soni, jimbo la Bumbuli, ambacho mwanzoni kwa miaka ya 2000 kilikuwa na sifa kubwa ya kutoa bidhaa nyingi, bora na za thamani kubwa.

Mradi huu utaenda hatua ya mbele zaidi ya Bumbuli Packing House kwa kutengeneza juisi, jams, concentrates na bidhaa nyingine za mboga na matunda kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi. Mradi huu, sio tu utatoa ajira kwa watu wa Bumbuli, bali pia utahakikisha soko la uhakika kwa mboga na matunda ya Lushoto linapatikana na kuongeza thamani ya mazao ya wakulima na hivyo kuwaongezea kipato.

 1. 3.     Mradi wa Kutoa Mikopo kwa Masharti Nafuu (Bumbuli Microfinance Institutition)

Jimbo la Bumbuli halina tawi la benki yoyote na huduma ya fedha ni tatizo kubwa. Shirika la Maendeleo Bumbuli limeomba leseni kutoka Benki Kuu kuanzisha taasisi ya fedha kwa ajili ya ukopeshaji kwa masharti nafuu na pamoja na huduma nyingine za fedha. Andiko la Mradi huu limefanywa kitaalam sana, baada ya utafiti wa karibu miezi nane kuhusu njia muafaka ya kutoa huduma ya fedha kwa masharti nafuu kwa watu wa Bumbuli. Mradi huu utagharimu shilingi milioni 450 kwa kuanzia na baada ya miaka mitatu mtaji utaongezwa na kufikia shilingi bilioni 1.6. Wakati tunasubiri usajili na leseni kutoka Benki Kuu tayari wapo wafadhili ambao, baada ya kusoma andiko letu, wameonyesha nia ya kusaidia mradi huu.

Msingi wa mradi huu ni kuwezesha vikundi vya kuweka na kukopeshana fedha ambavyo tayari vipo lakini vina mtaji mdogo, kutoa mafunzo ya fedha kwa vikundi hivi, na kuhamasisha kuanzishwa kwa vikundi vingine. Kipaumbele na nafuu ya mikopo itatolewa zaidi kwa vikundi vitakavyotumia fedha hizi kwa uzalishaji mali na shughuli ambazo zitaajiri watu wengine.

 1. 4.     Mpango wa Malipo kwa Kufanya Vizuri kwa Shule za Sekondari (Cash-On-Delivery for Secondary Education in Bumbuli)

Shirika la Maendeleo Bumbuli (BDC) litakavyotekeleza program ya msaada ya Malipo kwa kufanya vizuri** au cash on delivery (COD), ambayo itaongeza umakini na tija kwenye kujifunza na matokeo ya mitihani katika shule za sekondari jimboni Bumbuli. Kulingana na utafiti wetu, jimbo la Bumbuli liko kwenye hali ya kukata tamaa ya kupata msaada kwenye Sekta yake ya Elimu ya Sekondari. Shirika la Maendeleo Bumbuli (BDC) litatekeleza  program ya majaribio ya malipo kwa kufanya vizuri (COD), ya miaka mitatu ambayo itafanya malipo kulingana na idadi ya wanafunzi ambao wamefaulu Mitihani ya Taifa ya  Kidato cha Nne. Shirika la Maendeleo Bumbuli (BDC) linalenga kuboresha matokeo ya kujifunza/elimu katika jimbo la Bumbuli kupitia program hii ya kutoa motisha. Program hii itahusu Shule za Sekondari za Serikali za Kata.

Malipo kwa kufanya vizuri (COD) ni utaratibu mpya kutoa  msaada ambapo wafadhili hutoa pesa kwenye maendeleo yanayopimika  kwa kuangalia matokeo maalum. Unahusianisha moja kwa moja malipo na matokeo maalum,  ikiwapatia  watendaji/wapokeaji motisha ya kuongeza nguvu zao za kufanyakazi ili kufikia maendeleo.

Msingi na uhalali wa wazo la CDO, ulioanzishwa awali na  Kituo cha Maendeleo ya Kimataifa(Center for Global Development) mjini Washington, umejikita kwenye mtazamo kwamba kazi za maendeleo ni lazima zitathminiwe kwenye athari (impact) zinazoletwa. Mbinu inawakilisha mabadiliko kutoka kufuatilia nguvu na rasilimali ambavyo  mashirika huwekeza katika kutoa misaada – ‘nyenzo/rasilimali’, na pia shughuli na vifaa/vitendeakazi vinavyotokana na uwekezaji huo – ‘matokeo’. Badala yake, mbinu hii inalenga kujikita kuangalia namna gani maisha ya watu masikini yameweza kubadilishwa kutokana na uwekezaji kwenye sekta au eneo fulani la maendeleo (afya, elimu, n.k)

Mnamo mwezi Septemba 2011, Shirika la Maendeleo Bumbuli lilifanya utafiti wa kina juu ya mazingira ya kujifunzia Bumbuli na kugundua kwamba shule nyingi, walimu, na wanafunzi wa Bumbuli hawana motisha wala rasilimali zinazohitajika kuwawezesha wafanye vizuri kama inavyotarajiwa.

Kwa wastani, kila shule iliyotoa data za matumizi ya pesa ilionyesha ni Sh. 5,268 kwa kila mwanafunzi kwa mwaka 2010 (kiasi kilichotarajiwa kwa shule za Sekondari ni shilingi 25,000 kwa kila mwanafunzi). Pamoja na hayo, utafiti ulionyesha kuwa ni 71% tu ya walimu walikuwepo shuleni, ambapo ni 19% tu walikutwa madarasani. Utafiti huo ulionesha kuwa walimu hupata mishahara yao kwa wakati. Wastani wa mshahara halisi wa mwalimu wa Bumbuli ni Sh.395,000 kutoa malipo ya deni ya Sh.74,000 kila mwezi. Wengi walionesha kuwa na shughuli ya ziada ya kiuchumi (67%), hasa kilimo (90%). Wengi wao (98%) walidai kutokuhusishwa katika hatua za kupanga bajeti za shule. Wastani wa Pato la Mtanzania anayeishi kijijini (ikiwemo Bumbuli) ni Sh.152,000 (HBS, 2010). Wakati 89% ya wanafunzi wanaonesha kushiriki katika shughuli za kiuchumi wa familia, bado 70% wanafanikiwa kupata muda kidogo wa kukamilisha kazi zao za masomo wakiwa nyumbani, huku 34% inaonesha hawakufika shule kwa mwezi uliopita kutokana na kusaidia shughuli za nyumbani.  Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne ya mwaka 2011 kwa Shule za Bumbuli yalikuwa mabaya sana. Kati ya wanafunzi 1,327 waliofanya mtihani, hakuna aliyepata Division 1, waliopata Division 2 ni wanne, waliopata Division 3 ni 39, na waliobakia, yaani  wanafunzi 1,274, walipata Division 4 na 0.

Pamoja na hatua mahsusi ambazo Serikali inachukua kuboresha elimu nchini na kuongeza ufaulu, Shirika la Maendeleo Bumbuli, kupitia Program hii ya COD, linataka kuonesha kwamba fedha zinaweza kugawika vizuri na kwa usahihi ili kuboresha elimu kwa kupima kiwango cha ufaulu wa wanafunzi.

Hatua na mikakati inayopendekezwa

Program ya COD kwa Shule za Sekondari Bumbuli  itahusisha makubaliano kati ya Shirika la Maendeleo Bumbuli, Shule za Sekondari Bumbuli na Halmashauri ya Wilaya kulipa jumla ya kiasi cha Dola za kimarekeni 100 kwa kila mwanafunzi anayefaulu mitihani ya kidato cha IV kwa daraja  la I-III. Malipo ya COD yatafanyika baada ya uthibitisho wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne. Fedha zitapelekwa Halmashauri ya Wilaya, Shule za Sekondari na kwa walimu na wanafunzi. Fedha zitakazogawiwa kwa shule zitatumika kwa ajili ya mahitaji ya kielimu ya shule kama zilivyowekewa vipaumbele na Bodi za Shule.

Watakaonufaika na mradi:

Kwa kila mwanafunzi atakayefaulu mtihani (Div I-III) anapomaliza kidato cha nne, Shirika la Maendeleo Bumbuli kupitia program ya COD litatoa malipo yafuatayo:

1. Walimu:  Tsh 60,040/= kwa kila mwanafunzi anayefaulu mtihani

2. Wanafunzi: Tsh 50,500/= Kwa kila mwanafunzi anayefaulu mtihani

3. Shule: Tsh 31,600/= Kwa kila mwanafunzi anayefaulu mtihani

4. Halmashauri ya Wilaya: Tsh 15,800/= kwa kila mwanafunzi anayefaulu mtihani

Vipimo na Ukaguzi:

Data za mitihani kuanzia mwaka 2011 zitatoa msingi wa awali, na msingi huo utakuwa ukibadilishwa kila mwaka na ufanisi wa utendaji wa shule, hivyo kila mwaka unakuwa msingi kwa ajili ya malipo ya mwaka ujao wa. Kiashiria cha matokeo kitakuwa idadi ya wanafunzi ambao wamefaulu kidato cha nne kwa kupata daraja la I-III. Ili kuyadumisha matokeo hayo, hatua mbalimbali zitakuwa vikiripotiwa kila mwaka na shule na halmashauri. Mkataba, matokeo, na taarifa nyingine zitawekwa wazi kwa wananchi ili kuongeza uwajibikaji wa wafadhili na wapokeaji

Shirika la Maendeleo Bumbuli halina nia ya kusema kwamba COD ndio suluhisho pekee la tatizo la maendeleo ya elimu au ufumbuzi wa matatizo yote katika mfumo wa elimu nchini lakini tunaamini inaonesha matarajio ya kutosha kuona thamani ya kujaribu, kujifunza na kutathmini.

Uendelevu wa program

Ili program iwe endelevu, Shirika la Maendeleo Bumbuli(BDC) litaweka mfumo thabiti wa kufanya tathimini na kutoa mrejesho, ambao utatumika kama zana ya kupimia uwajibikaji, na kuendeleza uwazi. Pia ni muhimu kuzingatia ushirikishwaji wa wenyeji wa Bumbuli na umiliki wa program ya COD. Hili linaweza kufanikiwa kwa kuanzisha kampeni ya kuhamasisha elimu bora kama uwekezaji wa wenyeji, na Mtandao wa Wahitimu wa Shule za Sekondari Bumbuli kwa ajili ya fedha za COD. Zaidi sana, Shirika la Maendeleo Bumbuli litahusisha na kutumia Bodi za Shule, ambazo zinahusisha wazazi na walimu. Hii ndiyo njia itakayowafanya watu wa Bumbuli wathamini juhudi zao wenyewe katika kuboresha jamii zao.

5. Kambi ya Wanafunzi Wanaojiandaa na Mtihani wa Kidato cha Nne 2012

Kuanzia tarehe 4 Agosti hadi 5 Septemba, wakati wa likizo za masomo, Shirika limeandaa kambi maalum kwa matayarisho ya vijana wanaojiandaa na mtihani wa Kidato cha Nne mwaka huu. Kambi hii itakuwepo kwenye Kituo cha Elimu Soni, ambacho kina mandhari, mazingira na eneo la kutosha kufundishia na kuishi wanafunzi katika kipindi hiki.

Kila siku, wanafunzi hao watapigwa msasa kwa masomo ambayo hawakupata fursa ya kuyasoma vizuri katika mwaka wa shule, watafundishwa mbinu za kufanya mitihani (ikiwemo time-management), na kufanya revision ya mitihani ya Kidato cha Nne ya kuanzia mwaka 1984 hadi sasa. Shirika litatafuta walimu wenye sifa za kufundisha masomo ya Hesabu, Kiingereza, Historia, Kemia, Fizikia na Biolojia, hata nje ya Jimboni na kuwalipa posho kuja kufundisha kwenye kambi. Pia tutaomba watu mbalimbali, ikiwemo walimu wastaafu, wenye moyo wa kujitolea waje kufundisha kambi hii.

Mwisho

 

Hadi sasa Shirika la Maendeleo Bumbuli halijapata mfadhili au ufadhili kutoka kokote au kwa mtu yoyote. Miradi hii niliyoitaja ndio iko katika hatua za kupata ufadhili. Fedha ambazo zimetumika hadi sasa kuanzisha Shirika, kuweka ofisi, kuajiri watumishi wa muda na kufanya utafiti na kutengeneza maandiko ya miradi zimetokana na mkopo niliouchukua kama Mbunge, ikiwemo mkopo wa gari ambao sikuutumia kununua gari bali kuanzisha Shirika.

Napenda kutoa mwito kwa wana-Bumbuli wenzangu na Watanzania kwa ujumla kusaidia kuchangia maendeleo ya Jimbo la Bumbuli, hasa kwa miradi ambayo  hatukuitafutia ufadhili kama huu wa COD na kambi.  Kwa kuchangia unaweza kutumia namba ya M-PESA 0762088050. Kwa maelezo zaidi kuhusu Shirika la Maendeleo Bumbuli, tuma barua pepe: getinvolved@bumbuli.org au piga simu:+255 22 2129821/6 au tuma fax: +255 22 2129796

Katika miezi ijayo, BDC pia itatekeleza miradi ya kitaifa yenye manufaa kwa maendeleo na utawala bora kwa nchi yetu. Naamini nchi yetu itapiga hatua za maendeleo kwa kasi zaidi kama kila mmoja wetu, kwa nafasi na uwezo wake, atathubutu, lakini pia kama sote tutasaidiana katika kuchangiana na kupeana mawazo kuhusu shughuli za maendeleo.

January Makamba

Mbunge Bumbuli

8 Julai 2012

source:dewjiblog

Mtandao wa Thunderumblings wampa ushauri Hasheem Thabeet

Leave a comment


Jana ilibainika wazi kuwa mtanzania Hasheem Thabeet amesaini mkataba wa kuichezea timu ya Oklahama City Thunder kwaajili ya misimu miwili ya ligi ya NBA ambapo kwa mwaka atakuwa akilipwa dola 880,000.
Hata hivyo tangu Hasheem aanze kucheza kwenye ligi ya NBA, hajawahi kuonesha kiwango cha kuridhisha na hivyo kujikuta akikoselewa mara nyingi na waandishi wa Marekani.
Hata hivyo mwandishi wa mtandao wa ThunderRumblings uliojikita katika kuandika habari za timu mpya ya Hasheem, Darnell Mayberry amempa ushauri wa kumsaidia mchezaji huyo kama anavyasema:
“Sio rahisi kwa Thabeet kuingia uwanjani mara nyingi msimu ujao. Kitu muhimu kwa Thunder, na Thabeet, ni kufocus kwenye maendeleo.
Ni wazi, kuna kipaji ndani ya urefu wa Thabeet wa 7-foot-3. Hakuwa mchezaji bora wa mwaka wa defense kwa misimu miwili na Co-Big East Player of the Year kwenye msimu wa mwisho wa UConn bure.
Lakini huu ni muda sasa wa kukitumia kipaji hicho. Ni muda wa Thabeet kufanya kazi.
Hii itakuwa ni timu ya nne kwa Thabeet ndani ya misimu minne baada ya kuwa drafted kama mchezaji wa pili kwenye usajili mwaka 2009. Tunaamini kuwa hii ndo itakuwa ni nafasi ya mwisho kuthibitisha kuwa anastahili kuwepo kwenye ligi ya NBA.
Lakini kitu cha kwanza ambacho Thabeet anatakiwa kufanya kuonesha kuwa muda huu, timu hii itakuwa tofauti na misimu mitatu iliyopita ni kwenda Orlando kuungana na wachezaji wenzake wapya kwenye summer league.
Mara nyingi wachezaji maarufu huwa hawashiriki kwenye ligi hii. Lakini katika mtu ambaye anatakiwa kujifanya mjinga ni Thabeet. Kama mimi ningekuwa Thabeet, ninajitolea kwenda na kushindana badala ya kusubiri kocha aniambie niende.

Ni kitu rahisi kuweka ‘good first impression’ na kuprove kuwa yaliyopita, yamepita. Uthibitisho kuwa sasa yupo tayari kufanya kazi kwa bidii na kufanya kinachotakiwa kustawi kuwa mchezaji ambaye wengi waliamini alikuwa na sifa za kuwa.

Iwapo hakuna kingine. Ni nafasi ya kucheza. Na Mungu anajua Thabeet anahitaji hilo.
Kwenye misimu minne iliyopita, Thabeet amecheza kwa dakika 512 pekee. Kwa kulinganisha, mchezaji (guard) chipukizi wa Thunder Reggie Jackson alicheza dakika 501 msimu huu. Ukitengenisha muda wake akiwa na Houston na Portland mwaka huu, Thabeet alicheza dakika 139 tu. Kevin Durant alicheza dakika 213 kwenye fainali za NBA dhidi ya Miami pekee.
Muda wa uwanjani ndicho kitu anahitaji Thabeet kuliko kingine chochote. Kama hatocheza, ama kutokuwa mchezaji aliyetegemewa kuwa defender mzuri, basi na iwe. Lakini kuna njia moja ya kutoka.
Thabeet anahitaji kuchukua hatua hiyo ya kwanza. Anahitajika kwenda Orlando.”

source:bongo5

Mb Dog arudi kwa kishindo, aachia ngoma mpya na kufungua studio

1 CommentBaada ya kupotea kwa muda mrefu kwenye ramani ya muziki, hatimaye Mb Dog amevunja ukimya kwa kuachia wimbo mpya uitwao ‘The Only One’ alioufanya kwenye studio yake mwenyewe aliyoifungua hivi karibuni, Makopa Inc.
Msanii huyo aliyetamba zamani na kibao ‘Latifa’ amesema kwa muda mrefu alikuwa akifanya mambo yake nchini Ujerumani na sasa ameamua kurudi kwenye game.
Katika mazungumzo ya simu aliyofanya na Bongo5, Mb Dog amesema hana wasiwasi kuwa ataishika tena mioyo ya wapenzi wa muziki wa Tannzania kwakuwa haoni kipingamizi na muziki haujabadilika sana.
“Navyoona najua muziki umechangamka katika njia zake, lakini sio kwamba watu wamebadilika kuimba na muziki utafanyika vile vile kama watu walivyozoea kuusikia, sema tu katika kuanzia kuna harakati zitakuwa tofauti muda mfupi wakati nikitulia kwasababu muda mrefu nilikuwa sijajihusisha na haya mazoezi kwasababu ya mambo yangu binafsi,” alisema.
Aliongeza kuwa ujio wake mpya unaweza kuwa zaidi ya Latifa, “hilo ni miongoni mwa mawazo niliyonayo kwasababu sijaona kama kuna vitu tofauti vinavyofanyika labda vya chinichini ambavyo sivifahamu, lakini kimuziki tu naona uko kawaida na ntafanya vizuri zaidi ya hata hivyo.”
Mb Dog amesema hajamsahau P-Funk Majani ambaye ndiye alimtambulisha kwenye muziki wa Tanzania kwa kumtengenezea hit ya Latifa. “Ujue yeye ndo kama father kwenye muziki huu, ni mtu ambaye akinifanyia kazi anatumia nguvu nyingi sana lakini sasa nimerudi, nimefanya hii ngoma mwenyewe sasabu yeye pia ana kazi nyingi, lakini kwasababu muda upo lazima niende pale kupiga ngoma mbili tatu watu waziskie kutoka pale. Katika albam yangu kuna watu muhimu kama yeye hawawezi kukosa kunipigia nyimbo.”

source:bongo5

MAJAJI WA EPIC BONGO STAR KUTEMBELEA MAKAZI RASMI YA ZANTEL SABASABA.

Leave a comment


Mkuu wa mawasiliano ZANTEL Awaichi Mawalla alipata nafasi ya kuelezea njia mpya ambayo wenye vipaji vya kuimba waliokosa nafasi ya kufanya usaili wanaweza kufanya usaili kupitia simu zao za mkononi. Mfumo huu ni wa sauti ambapo mshiriki anapewa nafasi ya kuimba nyimbo aitakayo kwa muda usiiozidi dakika moja na kuweza kupata nafasi ya kusikilizwa na Majaji.

Master J

Rita Paulsen na Mkuu wa Masoko kutoka Zantel bwana . Deepak K. Gupta.

Rita Paulsen na Salama Jabir wa tatu kutoka kulia, wakiwa pamoja na wafanyakazi wa Zantel.

Majaji wa EBSS walipata nafasi ya kutembelea kujionea maonyesho yanaondelea ikiwa ni pamoja na kukutana na waandishi wa habari kuelezea waliyoshuhudia katika usaili wa mikoa mitatu waliyopitia ya Dodoma , Zanzibar na Lindi . Pia waliweza kutoa sifa wanazoziangalia katika kutafuta vipaji vya muziki pamoja na kueleza eneo la usahili unaofuata wiki hii A town Arusha Triple A.

Balotelli kupima ili(DNA) kujua kama ni baba wa mtoto wa Raffaella

Leave a comment


Mshambuliaji wa Manchester City na timu ya taifa ya Italia Mario Balotelli juzi ameviambia vyombo vya habari nchini Italia kuwa atachukua vipimo (paternity test) vya hospitali ili kujua kama yeye ndo baba wa mtoto ambaye mpenzi wake wa zamani anadai kuwa na ujauzito naye.
Raffaella Fico, 24, nyota wa TV na model wa nguo za ndani, aliliambia gazeti la kila wiki la Chi kuwa anategemea kupata mtoto wa Balotelli.
“Nikithibitisha kuwa mimi ndo baba, ntachukua majukumu yote,” alisema Balotelli mwenye miaka 21, kwenye maelezo yake.
“Nilifahamu kupitia kwa mtu mwingine siku chache zilizopita kuwa Raffaella ni mjamzito. Ndio maana niliamua kuwasiliana naye na hapo ndipo aliponiambia kuwa ni kweli.”
“Nimejisikia vibaya, sidhani kama ni kawaida kutoelezwa chochote mpaka mwezi wanne wa ujauzito.”
Uhusiano wa miezi 18 wa wapenzi hao ulikuwa ukizungumzwa na kuandikwa mara kwa mara kwenye vyombo vya habari vya Italia kabla hawajaachana mwezi April mwaka huu

Wema Sepetu na Diva waingia kwenye orodha ya kusaidia wasiojiweza

Leave a comment


Ray Kigosi akitoa msaada

Lady Jay Dee akitoa msaada

Lady Jay Dee

Wema Sepetu

Diva Loveness Love

Muigizaji wa filamu nchini na Miss Tanzania wa zamani (2006),Wema Sepetu anatarajiwa kwenda jijini Arusha mwezi huu na kushiriki uoashaji wa magari ili kukusanya fedha za kusaidia watu wasiojiweza jijini humo.
“On 14th July I will be in Arusha with manager kushiriki uoshaji wa magari ili kuchangia fedha za kusaidia wasiojiweza in Arusha,” alitweet jana.
Mwingine aliyeamua kujitolea nguvu na mali kuchangisha fedha kwaajili ya kuwasaidia watoto yatima ni mtangazaji wa Clouds Fm, Loveness aka Diva.
Kupitia website yake, Diva amesema, “So nimeamua kwa muda mrefu sana kutoa for charity and right now am too busy organizing this charity event inayoitwa Diva giving for charity. Aim is raising much needed funds to support orphans.
June na July imekuwa miezi iliyotumiwa zaidi na mastaa wa hapa nchini kusaidia vituo vya watoto yatima.
June 30, mwanamuziki Lady Jaydee pamoja na familia yake walikitembelea kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre kilichopo Kinondoni jijini Dar es Salaam na kutoa misaada mbalimbali ikiwa pamoja na kushiriki chakula cha mchana na watoto hao.
Katika hotuba yake, kituo hicho kilisema kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na kukosa fedha za kuwalipa wahudumu, Kukosa eneo kubwa la kujenga kituo, Kukosa wafadhili, watoto kutokuwa na sare za shule na kukosa gharama za kuwasomesha (michango ya shule).
Lady Jaydee aliwaahidi kuwatafutia kiwanja kikubwa kwaajili ya kujenga kituo kingine na kusema kuwa iwapo akitokea mtu wa kuwasaidia kiwanja, watachangisha fedha za kuanza ujenzi huo.
Naye muigizaji wa filamu mwenye mafanikio makubwa nchini Raymond Kigosi aka Ray The Greatest, weekend iliyopita alikitembelea kituo hicho cha Maungo na kutoa msaada sambamba na uzinduzi wa filamu yake mpya ya Sobbing Sound.
Kupitia blog yake Ray alisema: “Hili ni jukumu la watanzania wote kuanza kuguswa katika hili maana hapa duniani sisi ni wapangaji tu makazi yetu ni kwa Mungu Baba, sasa unapopata kidogo jaribu kuwafikiria na wale waliokuwa na maisha magumu, yaani tugawane umasikini.”

source:

Producer Ally Baucha afiwa na baba yake mzazi

Leave a comment


Producer mkongwe nchini wa studio za Baucha Records, Ally Baucha, amefiwa na baba yake mzazi usiku wa kuamkia leo.
Leo usiku muda wa saa 6:26, ametutumia ujumbe wa simu unaosema, “Mambo vp…? Nimefiwa na baba mzazi leo usiku huu. Najua wewe ni mtu muhimu kukutaarifu kwanza, nasubiri kuelekea Zanzibar kwa mazishi… Baucha.”
Baucha amesema kifo cha baba yake Mzee Mohamed Yussuf kimetokana na ugonjwa wa ini.
Mzee Yussuf aliyefariki akiwa na umri wa miaka 69,aliwahi kuwa mkuu wa polisi wa wanamaji mkoa wa Mwanza miaka ya 1980 kabla ya kuhamishiwa Zanzibar.

source:bongo5

Older Entries

%d bloggers like this: