Home

HAWA NDIO WACHEZAJI WA SIMBA KOCHA ALIOSEMA HARIDHISHWI NA VIWANGO VYAO.

Leave a comment


KOCHA Mkuu wa Simba Milovan Cirkovic amesema kikosi chake hakipo imara katika kiwango kile anachokihitaji kwa ajili ya Michuano ya Kagame ambayo timu nyingi zinajiandaa vizuri.
Wachezaji ambao viwango vyao havijamridhisha ni Haruna Moshi ‘Bobani’, Mwinyi Kazimoto, Juma Nyosso na Amir Maftar na hivyo amepanga kuwapa mazoezi kuwarudisha kwenye line.
Simba inatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza Jumatatu ijayo na URA ya Uganda saa kumi jioni na mchezo mwingine utapigwa kati ya Villa Club na Ports saa 8:00 mchana kwenye Uwanja wa Taifa. (Stori imeandikwa na shaffihdauda.com)

LINAH NA AJ KUZINDUA VIDEO YAO MPYA JUMAPILI

Leave a comment


Linah akiwa katika mazoezi ya kucheza


Recho,Keby,Sundi,Asia,Mwasiti na Linah baada ya Mzoezi


MWANAMUZIKI LINAH WA TANZANIA NA “AJ UBAO” AISHIE MAREKANI WATAZINDUA VIDEO YA WIMBO WAO MPYA WALIYOUTENGENEZEA WASHINGTON DC SAMBAMBA JUMAPILI HII USIKU WA TAREHE 24/6 NDANI YA “MAISHA CLUB” DAR-ES-SALAAM NA ” LUX LOUNGE” WASHINGTON DC,KUANZIA SAA 3 USIKU,NA PIA UTAWEZA KUIONA ONLINE/YOU TUBE KUANZIA JUMATATU TAR 25/6 ASUBUHI.
VIDEO HIYO INAITWA “ALL I NEED” IMETENGENEZWA NA KAMPUNI YA “DMK GLOBAL PROMOTIONS” YA MAREKANI CHINI YA DIRECTOR DICKSON MKAMA a.k.a “DMK”

source:bongo5

Airtel Blackberry Internet Service Sasa Tsh 5000 tu

Leave a commentAirtel wamezindua gharama mpya kwa watumiaji wa Blackberry ambapo sasa unaweza kujiunga na kifurushi cha wiki nzima kwa shilingi elfu tano tu. Hii inamaanisha Airtel sasa wanakuwa ndio wanakuwa na gharama nafuu zaidi za Blackberry Internet Service (BIS) ambapo kabla tIGO na Vodacom ndio walikuwa na huduma ya Internet ya wiki kwa shilingi 7,000 huku zantel ya kwao ikiwa shilingi 11,000. Kujiunga unatakiwa kutuma neno KAMILI7 kwenda namba 15344 na utaunganishwa.
Kitu pekee ninachokitegemea hapa ni kuongezeka kwa wateja watakaohamia Airtel na kama hawajajipanga wataishia kuwa kama tIGO ambao ukiwa Dar es Salaam kuna baadhi ya maeneo BIS ina kasi ndogo mno inazidiwa hata na mtu anaetumia WAP. Mfano ni ukiwa Kinondoni na Mwenge ambako nadhani kuna wingi wa watu.
Zaidi ya hapo tunawashukuru kwa kusikia kilio cha muda mrefu cha watumiaji wa Internet kwa kupunguza bei ya BIS

source:tanganyikan blog

HUU NDIO MFANO MZURI WALIO UFANYA WHITEDENT

1 Comment


Wanafunzi wa Mbagala kuu Primary School wakiwa na zawadi zao kutoka Whitedent.


Nawapongeza Whitedent kwa hili kwa sababu ya zoezi lao kubwa lakini lenye urahisi wa kupata zawadi ambalo wamekua wakiliendesha kupitia TV, T he Whitedent manufacturers Chemi & Cotex Industries Ltd jana wametoa zawadi mbalimbali yakiwemo matank ya maji kwa shule mbili za primary Dar es salaam..

Alfur-Qaan Primary School iliyopo Ilala Malapa Mferejini na Mbagala Kuu Primary School wilayani Temeke ambapo kila shule imepata tank lenye kuhifadhi maji kwa lita elfu tatu, mara ya mwisho kwa Whitedent kufanya Quiz kama hii ni 2008, Mwaka huu imerudi tena na itafanyika kwenye mikoa ya Arusha, Mbeya, Mwanza na Dar es Salaam.

Ili kupata washiriki wengi zaidi, inaendeshwa campaign ya wiki nzima kupitia TV ambapo mtangazaji atakua anauliza swali kuhusu shule na wanafunzi watakua wanatuma msg kujibu ili kujiweka kwenye nafasi ya kushinda zawadi ambapo wanafunzi wanaweza kuiwezesha shule yao kushinda tank la maji kupitia maswali yanayoulizwa kwenye TV kila alhamisi saa moja kamili mpaka na nusu usiku na kurudiwa jumapili saa sita kamili mpaka na nusu mchana, imeanza may 17 2012 inaisha July 12 2012.

Michael Omari akiwa na zawadi ya Polytank.

Source:millardayo.com

%d bloggers like this: