Home

Picha na Matukio yaliyojiri kwenye Tamasha la Matumaini

Leave a comment


Jose Chameleone akitoa burudani.

Jose Chameleone akitoa burudani.

Wabunge mashabiki wa Simba wakishangilia ushindi dhidi ya watani wao wa Yanga.

Nyomi iliyohudhuria tamasha hilo.

Wema na Wolper wakionyeshana ubabe.

Bondia Mchumia Tumbo akimzimisha mpinzani wake.

Jamaa aliyemvaa Wema.

JULAI 7, 2012 Jiji la Dar lilisimama kwa takribani saa 16 kupisha tamasha la kihistoria la Usiku wa Matumaini lililotimua vumbi ndani ya Uwanja wa Taifa, Ijumaa Wikienda linakupa ripoti kamili.
Zilikuwa ni saa 16 za hekaheka, vifijo, nderemo, shangwe na burudani ya hali ya juu kuanzia saa mbili za asubuhi mpaka saa sita za usiku, Jumamosi iliyopita ambapo macho na masikio ya wengi viliekezwa uwanjani hapo.
SHUGHULI ILIVYOANZA
Mpango mzima ulianza majira ya saa mbili asubuhi ambapo wasanii chipukizi walifungua pazia la burudani kwa kuwarusha mashabiki waliokuwa wanaendelea kufurika uwanjani hapo.
Wakati hayo yakiendelea, walinzi na wakata tiketi walikuwa na wakati mgumu kuuhudumia umati wa watu uliokuwa umejazana nje ya lango la kuingilia uwanjani hapo huku Bendi ya FM Academia wakiwa wa kwanza kulianzisha kwa kutoa burudanai ya nguvu.
UPAKO WATAWALA
Baada ya wasanii chipukizi kumaliza kutoa burudani, ilifika zamu ya wasanii wa nyimbo za injili ambapo wakali wa muziki huo wakiongozwa na Upendo Nkone, Bahati Bukuku, Bonny Mwaitege, Martha Mwaipaja na Glorious Celebration waliitangaza vyema injili takatifu kwa kupitia karama ya uimbaji. Wakafuatia wasanii chipukizi wanaochana mistari.
BONGO MOVIES VS BONGO FLEVA
Mvua ya burudani iliendelea kunyesha ndani ya uwanja huo ambapo baada ya pilikapilika za mchana kutwa, hatimaye uliwadia wasaa uliokuwa unasubiriwa na wengi.
Wasanii wa kambi mbili hasimu, Bongo Movie inayoundwa na wasanii wa filamu na maigizo ya Kibongo na Bongo Fleva inayoundwa na wasanii wa muziki wa kizazi kipya, walijitupa dimbani katika mchezo uliovuta hisia za wengi.
Wasanii Jacob Steven ‘JB’, Vincent Kigosi ‘Ray’, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ na wengine wengi walikuwa kivutio kikubwa kwa upande wa Bongo Movie huku wasanii Hamis Baba ‘Baba’, Haroun Kahena ‘Inspekta’, Karama Masoud na wengine kibao wakisakata kabumbu la hali ya juu.
Mpaka kipyenga cha mwisho kinapulizwa, Timu ya Bongo Movie iliibuka kidedea kwa kuinyuka Bongo Fleva goli 1-0, lililofungwa na msanii anayejulikana kwa jina moja la Kiduku. Benchi la ufundi la Bongo Movie, likiongozwa na Fatuma Makongoro ‘Bi Mwenda’ lililipuka kwa shangwe wakati kipyenga cha mwisho kikipulizwa.
POLISI WA KIKOSI CHA MBWA WAWAKOSHA MASHABIKI
Baada ya mechi kati ya wasanii wa filamu na wale wa muziki kumalizika, polisi wa kikosi cha mbwa na farasi waliingia uwanjani na kuonesha namna mbwa walivyofuzu katika kukabiliana na uhalifu.
Wakaonesha wanavyoweza kukamata madawa ya kulevya na mabomu. Uwanja mzima ukalipuka kutokana na mashabiki kukoshwa na umahiri wa mbwa hao wanaotunzwa na jeshi la polisi nchini.
WAHESHIMIWA WABUNGE WATOANA JASHO
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaozishabikia timu za Simba na Yanga, nao walijitupa dimbani kucheza mchezo ambao ulikuwa maalum kuhamasisha uchangiaji wa fedha za kujengea mabweni katika shule za sekondari zilizopo vijijini, chini ya Mamlaka ya Elimu Tanzania.
Wabunge Idd Azzan, Zitto Kabwe, Joshua Nasari na wengine wengi waliiongoza timu ya Wabunge wa Simba kukanyaga kandanda safi, huku Mwingulu Nchemba na wenzake wakipiga soka safi upande wa Wabunge wa Yanga.
Mpaka mwamuzi Othman Kazi anapuliza kipyenga cha mwisho, matokeo yalikuwa ni suluhu (0-0).
Mikwaju ya penalti ilipopigwa, Timu wa Wabunge wa Simba iliibuka kidedea kwa kufunga matuta 3-2, shukrani kwa mikwaju ya waheshimiwa Yona Kimube, Amos Makalla na Kikula Abel. Waliokwamisha mpira wavuni kwa upande wa timu ya Yanga ni waheshimiwa Michael Kadege na Sadigo Juma.
NENO LA SHIGONGO, NAPE, ZITTO
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, waandaaji wa tamasha hilo, Eric Shigongo alipanda jukwaani na kutoa nasaha zake kwa dakika kadhaa, aliwasihi Watanzania kurejesha mapenzi kwa nchi yao na kufufua matumaini mapya ya mafanikio.
Naye Katibu wa CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye aliwashukuru wote waliohudhuria tamasha hilo na kueleza kuwa wameshiriki katika mkakati wa kuchangia ujenzi wa mabweni. Kwa upande wake, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe naye aliwashukuru wote kwa kushiriki kwenye kampeni ya kuzisaidia shule za vijijini kupata mabweni, burudani ikaendelea.
ZAMU YA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA
Baada ya mapambano hayo ya soka, burudani iliendelea ambapo Juma Kassim Kiroboto ‘Nature’ aliwaamsha mashabiki vitini, akafuatiwa na kundi la muziki la Pah One linalofanya muziki pande za Bondeni (Afrika Kusini). Burudani ikaendelea kwa wasanii wengine kama Rashid Makwilo ‘Chid Benz’ kupanda na kupafomu kwa kiwango cha juu.
WEMA VS WOLPER, NGOMA DROO
Warembo waliolikamata soko la filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper na Wema Sepetu nao walitia fora kwa pambano lao kali la masumbwi. Pambano hilo la raundi tatu ambalo lilitarajiwa kumaliza bifu la siku nyingi kati ya wanyange hao, lilitanguliwa na pambano kati ya Kanda Kabongo na Ramadhan Kido, lililomalizika kwa Kabongo kushinda kwa pointi. Mpaka pambano la Wema na Wolper linamalizika kwa droo, uwanja mzima ulikuwa ukishangilia kwa nguvu.
Katika tukio lingine lililowashangaza wengi, baada ya Wema kumaliza pambano, shabiki mmoja ambaye hakufahamika alikotokea, alimvamia msanii huyo akiwa anateremka ulingoni na kumkumbatia kwa nguvu lakini kabla hajamdhuru msanii huyo, polisi walimdaka juujuu na kumshushia kichapo cha haja kabla ya kutolewa nje mzobemzobe.
CHAMELEONE AACHA GUMZO NA VALUVALU
Baada ya mapambano ya ndondi, msanii mkali kutoka nchini Uganda, Joseph Mayanja ‘Chameleone’ aliingia kwa staili yake uwanjani hapo ambapo umati wote ulilipuka kwa shangwe za nguvu wakati msanii huyo akikamua wimbo wake unaobamba kwa sasa, Valuvalu na nyingine nyingi. Mpaka msanii huyo anamaliza shoo, kila mtu alikuwa amesuuzika moyo vilivyo kutokana na burudani ya nguvu aliyoiangusha.
DIAMOND KAMA KAWAIDA YAKE
Yote tisa, kumi ni shoo ya msanii anayeshikilia tuzo tatu za Kili, Naseeb Abdul ‘Diamond’ ambaye baada ya Chameleone kumaliza shoo, aliingia kwa mbwembwe za hali ya juu.
Wacheza shoo wake waliingia na njiwa weupe ambao waliwaachia uwanjani hapo kabla ya kuanza makamuzi. Diamond aliendeleza makamuzi ya nguvu na kuwadatisha vilivyo maelfu ya mashabiki waliofurika ukumbini humo.
Mpaka inatimu saa sita za usiku, kila aliyehudhuria uwanjani hapo alikuwa ametosheka kwa kiwango kikubwa na burudani ya nguvu iliyoangushwa uwanjani hapo kuanzia saa mbili za asubuhi.

source:globalpublishers

Mtanzania aliyepotea Norway; Polisi wanaomba msaada

Leave a comment


Tromøy, Arendal (Norway).
Mwanamke mwenye asili ya Tanzania anatafutwa, ametoweka nyumbani baada ya kudai kudundwa na mmewe tangu Jumatatu .

Huyu ndiye dada wa Kitanzania aliyepotea toka Jumatatu hajaonekana mpaka leo. Bado anatafutwa! Polisi wanaomba msaada wa wananchi kwa yeyote anayefahamu lolote kuhusu huyu dada.
Mbwa wa polisi wakisaidia kwenye msako wa kumtafuta mwanamke mwenye asili ya Tanzania aliyepotea Tromøy, Arendal. Picha na Anne Karin Andersen (Agderposten)
Jana saa moja mwanamke mmoja alipiga simu polisi na kusema kuwa amepigwa nyumbani kwake. Baada muda mfupi, akaonekana ametoka nyumbani kwake, maeneo ya Tromøy, Arendal. Ametoweka na hajaonekana tokea jana. Mwanamke huyo ana asili ya Tanzania.
Mumewe alitoa taarifa polisi baada ya kutoonekana kwa muda mrefu. Tokea jana amekuwa akitafutwa na helikopta, boti za polisi, polisi wenye mambwa, jamaa wa msalaba mwekundu na watu wa kujitolea.
Source: watanzaniaoslo

Matarajio ya kupata mshindi kutoka Tanzania katika mashindano ya Tusker Project Fame msimu wa tano jana yafikia ukingoni

Leave a comment


Matarajio ya kupata mshindi kutoka Tanzania katika mashindano ya Tusker Project Fame msimu wa tano jana yamefutika rasmi baada ya mshiriki aliyekuwa amesalia kutoka Tanzania kutoka.
Damiani Innocent Mihayo alifungasha virago jana baada ya jitihada zake za kuonesha kuwa aliingia kwenye probation kwa bahati mbaya kugonga mwamba. “Damian is Good…Bad choice ya nyimbo aliyoimba,he also lacks star quality,” aliandika mfuatiliaji mmoja wa mashindano hayo.
“Huyu jamaa (Damian) like two weeks ago alichemka mistari ya Ali Kiba, shame! Aaaa project fame alikua Lina, Msechu na kidoooogo Aneth, yaani hata Hemedi namsifu, he knew how to play the game. Ndo makosa tunafanya hata BBA. Watu kama Hemedi au hata Wema ni watu wanajua kucheza na ni rahisi watanzania kutoa support. Hilda na Julio ppphhheeeew,” aliandika mwingine aitwaye Yvonne kupitia Facebook.
Kutokana na kutolewa kwa Damian sasa watanzania watabakia kuwashuhudia tu washiriki kutoka Uganda, Kenya, Sudan Kusini, Rwanda na Burundi katika shindano hilo. Katika hatua nyingine wiki hii Universal Music Group (UMG) imeingia mkataba na shindano hilo ambapo itamsimamia mshindi wa mwaka huu. Pia itasimamia kurekodi albam ya pamoja ya washiriki kumi bora wa mwaka huu.

Picha za Dimond akiwa Ndani ya Mj-Recordz akiumiza kichwa kutengeneza Tangazo la Coca Cola

Leave a comment


Marco Chali na Diamond wakiwa studio wakitengeneza Tangazo hilo

Diamond akiwa anaandika Mistari,

Muziki sio rahisi kama mnavyo dhani, Angali jinsi jamaa anavyojituma kufanya kazi


Muziki sio rahisi kama mnavyo dhani, Angali jinsi jamaa anavyobadilisha mapozi, Lakini anaonekana anaipenda sana kazi yake


Muziki sio rahisi kama mnavyo dhani, Angali jinsi jamaa anavyoumizwa kichwa kutengeneza kazi zake.

UFISADI MWINGINE WA ATCL ULIOWEKWA HADHARANI NA MWAKYEMBE!

1 Comment
Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe ameibua ufisadi mkubwa uliofanywa na waliokuwa watendaji wakuu wa shirika la ndege Tanzania ATCL chini ya aliyekua kaimu Mkurugenzi Mtendaji Paul Chizi kufuatia kuingia mkataba usio na tija wa ukodishaji wa ndege kubwa aina ya Airbus 320 MSN 630 kutoka nchini Liberia, ndege ambayo ni mbovu.
Amesema “ni mkataba wa kipuuzi kabisa sijawahi kuuona katika historia, ni wa kipuuzi kuliko hata wa Richmond, tumeingizwa mjini peupe kabisa, tumeanza kuilipia Airbus wakati iko kwenye anga yani Tanzania inalipa pesa ya kukodisha hiyo ndege miezi sita iko kule, sisi tunalipa kwa pesa ya wakulima na wafanyakazi wanaolipa kodi… leo tunadaiwa bilioni 69 na jamaa wamefungua kesi, serikali imechoka kuibeba ATCL na mtalikumbuka baadae”
Ndege ya ATCL iliyokodiwa hivi karibuni chini ya uongozi wa Paul Chizi aliyesimamishwa kazi.
Mwakyembe amezungumza na wafanyakazi wa shirika hilo katika ziara aliyoifanya ambapo amesema mabadiliko ya kiuongozi aliyoyafanya na kumteua rubani wa siku nyingi katika shirika hilo Captain Lusajo Lazaro kukaimu nafasi iliyokua inashikiliwa na Chizi yamezingatia uwajibikaji, na kuhusu taarifa za kumlaumu Mwakyembe kwa kuchagua mtu wa kabila lake amesema “wanaosema hivyo ni kutokana na elimu ndogo, ufinyu wa kufikiri kama top management alikuepo huyo hivi jamani nitafute mtu mwingine kwa sababu ya ukabila? mnafikiria ukabila leo hii watanzania? nimewasimisha wakurugenzi wanne wote ni Wanyakyusa”
Kuhusu waliokasirika juu ya maamuzi ya kuwasimamisha kazi wakurugenzi wa ATCL, kwa hasira Mwakyembe amesema “waliokasirika ondokeni ATCL simameni muondoke, nani anawahitaji? aliekasirika aondoke sasa hivi na nitawafukuza kwelikweli, ndege za kukodisha zinatija gani?”
Mwakyembe pia ameshangazwa na ufisadi wa kukithiri kutokana na kitendo cha uongozi uliosimamishwa ATCL kutumia shilingi milioni 79.8 za kitanzania kwenda China kushonesha sare jozi 17 za wafanyakazi huku pia maafisa wawili wakiwa nchini humo kwa siku 48 kusimamia hiyo kazi ya sare.

SOURCES:MILLARDAYO

Masanja Mkandamizaji: Twitter Addict Lakini Anakimbiza

1 Comment


Masanja Mkandamizaji


Tangu alipojiunga twitter Mei 14 mwaka huu Masanja Mkandamizaji au masanjawani ametokea kuwa kipenzi cha watu wengi wanaomfuata. Kama ilivyo mtaani ambapo hana maringo na ni mtu wa watu hata twitter imekuwa hivyo. Lakini wapo mastaa kibao ambao mtaani wako poa lakini kwenye social media hawajabamba kwa muda mfupi kama Masanja, ni kwa nini?

Kitu cha kwanza kinachomtofautisha na waigizaji wengine waliopo twitter, masanja ameendelea kuwa yeye. Hajajaribu kuiga uhusika wa mastaa wa nje kama ilivyo kwa baadhi ya ndugu zetu ambao wanaleta Umarekani mwingi kwenye tweets zao. Jamaa ukitembelea timeline yake lazima ufurahi, ni utani na vichekesho kwa kwenda mbele huku akigusa kila kona na bila kumuogopa mtu. Pia amekuwa mstari wa mbele kwenye kutengeneza Trending Topics ambazo mara nyingi watu huzidakia na kuendelea kuzitumia katika tweets na mwisho wa siku ni raha kuzisoma tweet za TT husika.

Tofauti na watu maarufu wengine ambao akiingia twitter anafanya kufuata watu wachache anaowafahamu, Masanja yeye anafuata asilimia kubwa ya Watanzania. Mara ya mwisho nilipoangalia idadi yake ya followers alikuwa na followers 2,288 na yeye anafuata 2,133. Ukipiga hesabu ya haraka ni anafuata 98% ya followers kitu ambacho ni mara chache kuiona kwa wenye majina wengine.

Ugonjwa mwingine wa wenye majina bongo ambao Masanja kafanikiwa kuuepuka ni ile tabia ya kupotezea tweets za watu wanaomsemesha. Pamoja na kuandikiwa na watu wengi sana lakini jamaa anajibu kila mtu anaemuuliza swali au kumsemesha, anashukuru pale mtu anapomsifia na mwisho ni ile tabia ya kujichanganya kwenye mazungumzo ya wafuasi wake. Unajua watu wengi wanachukulia ukiwa maarufu wewe ndiye unatakiwa kusemeshwa au ukiongea wewe ndio unajibiwa na unaamua kujibu au kutojibu, Na asilimia kubwa ukimuandikia kitu au kumsifia badala ya kusema asante anaishia ku-Retweet. Kwa Mwanawani yeye kukiwa na kitu kinachofurahisha atakujibu au ku-Retweet na kuongeza utani wake.

Naamini akiendelea kuwa kama alivyo ndani ya muda mfupi ataingia kwenye orodha ya watu wenye followers wengi Tanzania na pia wenye ushawishi kwenye social media zaidi ya wanasiasa wengi ambao wamejiunga muda mrefu tu.

source:tanganyikan

Watu wengi Wajitokeza kwenye mazishi ya Mwili wa Aliyekua Mchezaji wa Timu ya Simba SC Patrick Mafisango

1 Comment


Watu wengi Wajitokeza kwenye mazishi ya Mwili wa Aliyekua Mchezaji wa Timu ya Simba SC Patrick Mafisango

Wachezaji wa timu ya soka ya Taifa (Taifa Stars), wakiwa wamebeba mwili wa aliyekuwa mchezaji wa timu ya Simba, marehemu Patrick Mafisango, tayari kutolewa heshima za mwisho leo kwenye viwanja vya TCC Chang’ombe, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Simba Aden Rage akimtuliza mchezaji wa timu hiyo, Haruna Moshi ‘Boban’ wachezaji walipokuwa wakitoa heshima zao za mwisho

Jamaa wakimfariji mlinda mlango wa Simba, Juma Kaseja aliyekuwa akilia kwa uchungu

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Mafisango

Viongozi wa michezo wakitoa heshima za mwisho kulia ni kanali mstaafu iddi kipingu

Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Mafisango

Mchezaji Nurdin Bakari akimfariji Kazimoto

Mwanachama maarufu wa Simba, Philemon Sarungi akimfariji Mwenyekiti wa Simba , Aden Rage ambaye alishindwa kuendelea kusoma risala na kuangua kilio.

%d bloggers like this: