Home

Lisa kuelekea China kushiriki Miss World 2012

Leave a comment


Miss World Tanzania 2012, Lisa Jensen akipunga mkono wakati akiondoka katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akieklekea nchini Nchina kushiriki shindano la Miss World 2012. Lisa anaiwakilisha Tanzania katika shindano hilo.

Lisa akisikiliza jambo kutoka kwa Mkurugenzi wa Lino International Agency, Waandajai wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga(hayupo pichani).

Lundenga akimsindikiza Lisa kwenda kukaguliwa tayari kwa safari ya nchini China.

Lisa akiwaeleza jambo Mkurugenzi wa Lino International Agency, Waandajai wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kushoto) na Afisa Habari wa Kamati ya Miss Tanzania, Hidan Rico

Lisa akisikiliza jambo kutoka kwa Mkurugenzi wa Lino International Agency, Waandajai wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga

Lisa akiwaeleza jambo Mkurugenzi wa Lino International Agency, Waandajai wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kushoto) na Mkuu wa Itifaki wa kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye.

Hashim Lundenga akisalimiana na mama mzazi wa Lisa Jensen wakati wa kumsindikiza mrembo huyo.

photosource:fatherkidevu

Photos: Nollywood actress Omotola Jalade arrives in Dar es Salaam

Leave a commentNigerian actress Omotola Jalade, who has won a huge following in Tanzania, is finally in the country following an invitation by fellow actress and former beauty queen Wema Sepetu.

Omotola arrived at Julius Nyerere International Airport at 3am Sunday morning and to receive her was the former Miss Tanzania, her host Wema Sepetu in company of other former beauties Miriam Odemba and Mange Kimambi. Omotola was scheduled to attend Wema’s movie launch which took place earlier that night however this could not happen due to flight delays.

Earlier on the day, speaking to the press Wema said she had extended an invitation to three of Nollywood’s leading actresses, Genevieve Nnaji, Omotola Jalade and Rita Dominic, but it was Omotola who accepted her invitation.

“The other two had other contractual commitments to fulfill, Genevieve is working on a project with Vivica Fox and likewise Rita is in the final steps of her upcoming movie so they could not honour the invitation” said Wema.

Rumor has it that Wema Sepetu together with her guest the Nollywood star Omotola Jalade are expected to meet with the President of the United Republic of Tanzania, his excellence Jakaya Mrisho Kikwete tomorrow at the state house in Dar es Salaam.

sources:bongo5

TAIFA STARS YATOLEWA KWA PENATI

Leave a commentTaifa Stars imetolewa kwenye mechi za mchujo za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kufungwa kwa penalti na wenyeji Msumbiji (The Mambas) katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Taifa ulioko Zimpeto pembeni kidogo ya Jiji la Maputo.

Refa Bennett Daniel alipopuliza filimbi ya kumaliza dakika 90 za pambano hilo timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1, hivyo kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo yanayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) mikwaju ya penalti ikatumika kupata mshindi. Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Dar es Salaam, Februari 29 mwaka huu timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. Msumbiji ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 9 lililofungwa na mshambuliaji Jeremias Sitoe akiungnisha krosi ya Elias Pelembe ambaye mabeki wa Taifa Stars walifikiri ameotea.

Stars ilisawazisha bao hilo dakika ya 89 likifungwa kwa kichwa na
Aggrey Morris kutokana na mpira wa kona uliopigwa Amir Maftah. Mikwaju ya penalti tano tano walioifungia Stars walikuwa Amir Maftah, Shabani Nditi na Shomari Kapombe wakati Aggrey Morris na Kevin Yondani. Kwa vile The Mambas nao walikosa mbili ikabidi iongezwe penalti moja moja. Waliofunga kwa upande wa Stars walikuwa John Bocco, Frank Domayo na Mrisho Ngassa wakati Mbwana Samata alikosa.

Akizungumzia pambano hilo, Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen aliwapongeza wachezaji wake kwa kupambana hadi dakika ya mwisho. Taifa Stars itarejea nyumbani Juni 19 mwaka huu, ambapo itaaondoka hapa saa 4.40 asubuhi kwa kupitia Nairobi, Kenya na kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 1.50 usiku.

Kikosi kilipangwa hivi; Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni/John Bocco, Aggrey Morris, Kevin Yondani, Shaabani Nditi, Mrisho Ngasa, Frank Domayo, Thomas Ulimwengu/Haruna Moshi, Mbwana Samata na Mwinyi Kazimoto/Amir Maftah.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

MUME WA JACK PATRICK KUNASWA

Leave a comment


Mume wa Jacqueline Patrick, Abdullalatif Fundikira.


Kamanda wa Kikosi cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya nchini, Godfrey Nzowa akionyesha madawa yaliyokamatwa na kumuhusisha Abdullalatif Fundikira.HATIMAYE Jeshi la Polisi Tanzania kupitia Kikosi cha Kupambana na Madawa ya Kulevya limemnasa mume wa ndoa wa Miss Mzizima na Mshiriki wa Miss Tanzania 2005 ambaye sasa ni modo, Jacqueline Patrick ‘Jack’, Abdullalatif Fundikira, UWAZI linaanika sinema nzima.
Kutiwa mbaroni kwa Fundikira kumethibitishwa na kamanda wa kikosi hicho, Godfrey Nzowa alipozungumza na gazeti hili Jumamosi iliyopita ofisini kwake, Kilwa Road Jijini Dar es Salaam.
KWA NINI ALINASWA?
Kamanda Nzowa alisema kuwa jeshi lake limelazimika kumkamata Fundikira baada ya kuwa katika orodha ya watu waliotajwa kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya.
SINEMA YA KUNASWA KWAKE
Aliongeza kuwa mtuhumiwa huyo alidakwa nyumbani kwake, Mbezi Beach, Kinondoni Jijini Dar es Salaam saa 12.00 asubuhi.
“Fundikira tulimkamata nyumbani kwake, ilikuwa saa kumi na mbili asubuhi. Kwa sasa tunamshikilia na upelelezi unaendelea, utakapokamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili,” alisema Kamanda Nzowa.
Akaongeza: “Fundikira alikuwa akitafutwa na jeshi tangu Mei 16 mwaka huu baada ya kutajwa na mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Mariam Mohamed Said, 29, kuwa ni miongoni mwa wauza madawa ya kulevya.
“Huyu mwanamke alinaswa katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere katika operesheni ya polisi ya ‘kufagia’ mtandao wa madawa ya kulevya.”
Kamanda Nzowa alisema Mariam alikamatwa akiwa na begi lenye uzito wa kilo 10 likiwa na mabunda 23 ya bangi yenye thamani ya shilingi milioni 12. Alikuwa akienda nchini Uturuki.
Alisema mara baada ya mwanamke huyo kunaswa, alimtaja Fundikira kuwa ‘memba’ wa mzigo huo. Ndipo jeshi la polisi lilianza kumtafuta mtuhumiwa hadi nyumbani kwake lakini akawa anajificha.
Akasema: “Hatimaye Jumamosi (Juni 9, 2012) alikamatwa kwa ushirikiano wa askari wangu na raia wema.”
AKUTWA JUU YA DARI
Habari zaidi za kipolisi mbali ya Kamanda Nzowa zilisema kuwa saa 11:00 alifajiri ya siku ya tukio, kikosi kazi kinachoongozwa na kamanda mwenyewe kiliizingira nyumba ya Fundikira na baada ya dakika kadhaa polisi waligonga geti.
Ikadaiwa kuwa mlinzi wa mtuhumiwa huyo alileta mvutano kati yake na polisi lakini hata hivyo, hakufua dafu kwani maafande hao waliingia ndani na kumsaka mtuhumiwa ingawa bila mafanikio.
Habari zikazidi kudai kuwa polisi walimkuta mke wa mtuhumiwa, Jack Patrick (pichani) ambaye naye alipobanwa aseme alipo mumewe huyo, hakutaka kutoa ushirikiano badala yake akawa anatetemeka.
Baadaye walisikia kitu kikitambaa kama nyoka juu ya dari, wakawa na shaka nako, walipozamia walimkuta mshukiwa huyo amejificha hivyo kumchomoa na kumpiga pingu hadi kwa mjumbe wa nyumba kumi wa eneo hilo.
Baada ya kukamilisha taratibu za kiserikali kwa mjumbe huyo, Nzowa na maafande wake walimfikisha mtuhumiwa Makao Makuu ya Kitengo cha Madawa ya Kulevya kilichopo Kilwa Road Jijini Dar es Salaam.

WASIWASI WA UTAJIRI WAIBUKA
Habari zaidi zilieleza kwamba, mtuhumiwa alihojiwa kuhusu nyumba ya ghorofa moja anayoishi kama ni yake ambapo alijibu amepanga na amekuwa akiilipia shilingi laki saba kwa mwezi (shilingi 8,400.000 kwa mwaka).
SHUKURANI KWA WANANCHI
Aidha, kwa upande wake, Kamanda Nzowa aliwashukuru raia wema kwa ushirikiano walioutoa katika kufanikisha kunaswa kwa mtuhumiwa huyo, akawaomba waendelee na moyo huo ili jeshi lake liweze kupambana na waovu wote.
TAHADHARI
Kwa upande mwingine, Nzowa aliwatahadharisha wale wote wanaojihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya kuacha mara moja kwani jeshi lake limejipanga vizuri kukabiliana na wahusika.
MAWAKILI MIDOMO WAZI
Katika Gazeti la Ukweli na Uwazi No. 739 la Mei22-28, 2012 ukurasa wa mbele kulikuwa na habari ya pili yenye kichwa; MADAI YA POLISI; MUME WA JACK PATRICK MUUZA UNGA.
Ndani ya habari hiyo, Kamanda Nzowa alithibitisha kuwa, jeshi lake linamsaka Fundikira kwa madai (kama kichwa cha habari kilivyosema, madai) kujihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya.
Baada ya habari hiyo kutoka hewani, Fundikira kupitia mawakili wake waliliandikia Uwazi barua ya kisheria wakidai kuwa habari hiyo haikuwa ya kweli na ilikuwa na lengo la kumchafulia jina mteja wao kwa kuwa hatafutwi na jeshi la polisi.
Aidha, katika barua hiyo, wanasheria hao walilitaka gazeti hili (LA KUFICHUA MAOVU) kumwomba radhi mteja wao sanjari na kulipa fedha kiasi cha shilingi milioni mia sita (600,000,000) kama fidia.
SHERIA IKO WAZI
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jeshi la polisi linaweza kumkamata mtu kwa tuhuma yoyote ile ambapo baada ya upelelezi kukamilika, humfikisha mahakamani au kumuachia huru wakiona hana kosa.
Endapo mtuhumiwa atafikishwa mahakamani na ikamuona hana hatia, ina uwezo wa kumwachia lakini bila kulaumu jeshi la polisi.
WANA HABARI NA KAZI YAO
Kwa kawaida vyombo vya habari vina uhuru wa kuandika habari zinazotolewa na jeshi la polisi katika ngazi husika, kama lilivyofanya Gazeti la Uwazi, bila kubughudhiwa na mtuhumiwa au mwanasheria wake.

source:

%d bloggers like this: