Home

Maafa Ya Kuzama Kwa Meli, Watu 30 wa Fariki dunia mpaka Asubuhii!!

Leave a comment


Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia Julai 19 hadi Julai 21 kufuatia maafa ya ajali ya Meli ya Mv. Skagit iliyozama karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein akitangaza maombolezo hayo, alisema bendera zote zitapepea nusu mlingoti na kwamba shughuli za sherehe na burudani zimefutwa kwa muda wa siku tatu za maombolezo.

Dk. Shein alisema shughuli za Serikali zitaendelea kama kawaida. Katika taarifa yake aliyoitoa Ikulu usiku wa kuamkia Julai 19, Rais Dk Shein amewahakikishia wananchi na hasa waliopoteza jamaa zao kuwa Serikali itabeba gharama zote za mazishi na pia kugharamia huduma za matibabu kwa majeruhi.

“Nimesikitishwa sana na msiba huu, Katika wakati huu si vema tukaanza kulaumiana jambo la muhimu hivi sasa ni kuokoa maisha ya watu” Alisema Rais Dk. Shein.

Mbali ya taarifa hiyo, Rais Dk Shein aliungana na wananchi, viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, Viongozi wa dini katika kutambua maiti zilizofikishwa katika eneo maalum la viwanja vya Maisara Suleiman.

Mbali ya kwenda katika viwanja hivyo, pia alifika katika eneo la bandari ya Zanzibar kufuatilia taarifa za tukio hilo. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana lilisitisha shughuli zake kufuatia maafa hayo ambapo wakati wa jioni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Nchimbi alitarajiwa kufanya majumuisho ya bajeti yake.

Baadhi ya Wabunge wakiongozwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Shamsi Vuai Nahodha, Mkuu wa Jeshi la Polisi walitembelea majeruhi katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja pamoja na eneo la viwanja vya Maisara ambapo maiti hufikishwa kwa ajili ya utambuzi.

Mbali ya Bunge, pia Baraza la Wawakilishi Zanzibar jana lilisitisha kwa muda shughuli zake ili kutoa nafasi kwa Wawakilishi hao wa wananchi kushiriki katika shughuli za uokozi ambapo wengi walifika bandarini kusaidia kazi mbalimbali ikiwemo kuwafariji waliopoteza ndugu zao.

Taarifa kutoka Mamlaka za Serikali zinaeleza kwamba hadi asubuhi hii maiti 30 zilipatikana ambapo 20 kati ya hizo zimetambuliwa na kuchukuwa na jamaa zao huku wananchi wengine wakiendelea na kuzitambua maiti zinazofikishwa katika eneo la Maisara.

Aidha, katika taarifa hiyo, watu 145 wameokolewa wakiwa hai, wengi wao wapo katika hali nzuri wameruhusiwa kuungana na familia zao baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar.

Meli ya Mv. Skagit ilizama Julai 18,2012 saa 7:50 mchana ikitokea Bandari ya Dar es Salaam kwenda Zanzibar ikiwa imebeba abiria 250 watu wazima, watoto 31 na mabaharia 6.

Kazi ya utafutaji na uokoaji zinaendelea asubuhi hii katika eneo la tukio ilikozama meli hiyo umbali wa maili sita Kusini mwa Kisiwa cha Yasin karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.

HUYU NDIO YULE MWANAFUNZI ALIEANDIKA MISTARI YA BONGOFLEVA KWENYE MTIHANI WA FORM FOUR, HIKI NDICHO ALICHOSEMA.

2 Comments


Julius a.k.a Elinaja.

Unakumbuka February 8 2012 wakati baraza la mitihani lilipotangaza matokeo ya kidato cha nne? stori kubwa ilikua mwanafunzi alieamua kuandika mistari ya bongo fleva kwenye sehemu ya kujibia maswali.

“nashukuru sana wanaosahihisha mitihani hii ya shule yangu, nitakapofeli naendelea na fani yangu ya bongofleva, Majita wangu wako levo za juu na sio East Zuu, kukosa ni kawaida kwa binadamu” hiyo ilikua ni swali namba 6 na 7

kwenye swali la 11 kwenye moja ya mitihani yake aliandika mistari ya bongofleva kwamba “acha utani my girl, unakuja nyumbani umezizi mwenzako huku naona sijiwezi, kazi hiyo ya kuzizi nakwambia ukweli mwanzo ulikua mzuri lakini mwisho ukawa mbaya”

Baada ya hayo matokeo watu wengi ana walitamani kumfahamu huyu mwanafunzi, Jina lake la kuzaliwa ni Julius lakini la kisanii ni Elinaja, na ametoa sababu 5 za kwa nini aliamua kuandika hiyo mistari ya bongo fleva kwenye mitihani yake ya kumaliza kidato cha nne.

Amesema “1 ni kutaka kutuma ujumbe kwa watu wanaosimamia Elimu kwa ujumla, sababu ya pili ni kutaka kusaidia watu wanaoteseka mtaani ambao wanaishi maisha magumu kwa sababu tu ya kushindwa kwendana na system ya elimu iliyopo ambayo ukishindwa kwenda nayo sawa umefeli, tulivyoumbwa kuna mtu anaweza akawa anashindwa kitu flani lakini ni mzuri kwenye kitu kingine sasa mfumo uliopo hautoi nafasi kwa wasioweza hiyo system, sababu ya tatu ni kutokana na utaratibu wa usaishaji wa mitihani kwa sababu sijui kama kuna mwanafunzi yeyote aliewahi kufanya mtihani wake wa mwisho alafu mtihani wake ukarudishwa ili kuona wapi alipokosa na wapi alipopata”

“Sababu ya nne ni kuhusu wazazi kutambua uwezo wa watoto wao toka wakiwa wadogo kipi wanaweza kipi hawawezi ili kuokoa muda na pesa, sababu ya tano ni kwa serikali ijaribu kuweka shule za vipaji toka mwanafunzi akiwa mdogo kabisa, leo hii kuna mtu amepata degree pale chuo kikuu kasoma miaka mitatu na kupewa degree ya sanaa lakini hawezi kukuonyesha cheti hata kimoja kwamba alikua na elimu ya awali ya hiyo degree, huwezi kuniambia una degree wakati hukupata elimu ya msingi ya ulichosomea”

“Kwa namna moja au nyingine sidhani kama nimefanikiwa kwa sababu nilichofanya watu walikichukulia tofauti sikufanikiwa ndio maana nimeamua kujitokeza kumalizia kazi ambayo niliianza kuifanya kule kwa sababu nafsi yangu ilikua inanisuta, ila kwa sasa watu watakua wameelewa na ninaweza kuwasaidia watu wengine” – Julius (Elinaja)

Unaweza kulike au kutweet hii story ili na wenzako wa facebook na twitter waione, shukrani!

source:millardayo

Balotelli kupima ili(DNA) kujua kama ni baba wa mtoto wa Raffaella

Leave a comment


Mshambuliaji wa Manchester City na timu ya taifa ya Italia Mario Balotelli juzi ameviambia vyombo vya habari nchini Italia kuwa atachukua vipimo (paternity test) vya hospitali ili kujua kama yeye ndo baba wa mtoto ambaye mpenzi wake wa zamani anadai kuwa na ujauzito naye.
Raffaella Fico, 24, nyota wa TV na model wa nguo za ndani, aliliambia gazeti la kila wiki la Chi kuwa anategemea kupata mtoto wa Balotelli.
“Nikithibitisha kuwa mimi ndo baba, ntachukua majukumu yote,” alisema Balotelli mwenye miaka 21, kwenye maelezo yake.
“Nilifahamu kupitia kwa mtu mwingine siku chache zilizopita kuwa Raffaella ni mjamzito. Ndio maana niliamua kuwasiliana naye na hapo ndipo aliponiambia kuwa ni kweli.”
“Nimejisikia vibaya, sidhani kama ni kawaida kutoelezwa chochote mpaka mwezi wanne wa ujauzito.”
Uhusiano wa miezi 18 wa wapenzi hao ulikuwa ukizungumzwa na kuandikwa mara kwa mara kwenye vyombo vya habari vya Italia kabla hawajaachana mwezi April mwaka huu

Esther Wassira awashutumu madaktari kwa kifo cha uzembe cha mtoto wa rafiki yake

Leave a comment


Mwanamuziki wa zamani ambaye kwa sasa ni mwanasheria, Esther Wassira amewatupia shutuma nzito madaktari wa hospitali ya Amana ya jijini Dar es Salaam kwa kile alichokiita ‘uzembe’ wa makusudi uliosababisha kifo cha mtoto mchanga wa rafiki yake.
“Naenda pia kwenye msiba wa rafiki yangu amefiwa na mtoto wake wa siku moja,aliyefia hospitali Amana,baada ya Madaktari kuwachomolea watoto ishirini Oxygen na kuwaacha wakiteketea!!! Kweli jamani??? Doctors??? You can kill innocent infants??? Si mngewaachia hiyo oxygen tu mkaondoka??? Serikali!!! Do something jamani..! Just give them what they want!! Think of the loss..mama abebe mimba miezi tisa,mwanae auliwe?” Esther aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
“This is a catastrophe to the nation..hivi kweli!!!!, it is very serious..yupo kwa mama yake anakandwa tumbo na mwanae ameshamzika!!! This is BAD! Naogopa nchi yangu!!”
Hata hivyo shutuma hizo nzito dhidi ya madaktari wa Amana zilizotolewa na mwanadada huyo zilipokelewa kwa hisia tofauti kutoka kwa watu wengine.
“Pole na msiba huo..ila usiwe unakurupuka na kuleta uzushi kuwa madaktari wamewachomolea oxygen watoto..ukiambiwa thibitisha sijui utasemaje…u r a lawyer..think before u leap….usiwe kama layperson kukurupuka na kusema habari za uvumi….madaktari sio wajinga kama serikali yako kufanya kitu kama hicho kwa infants kama hao….kifo cha watoto ni kawaida tu..kama ingekuwa hakuna huu mgomo na kukatokea hilo sidhani kama ungesema hivyo Esther,” aliandika mtu mmoja aitwaye Pedro Juan.
“Pedro usinifrustrate!! I have enough frustrations!!! Ninakwambia am sitting with a woman hapa my friend ananiambia exactly what has happened wewe unaniambia uzushi!!! Ni heri ushtuke na uombe kuliko kunistress zaidi..do you think I want to accuse doctors au unadhani nafurahi kuona insensitivity ya government!! Am a human being,a woman for that matter!! Lawyer or not!!!,” alijibu Esther.
Mtu mwingine aitwaye Isaac Ruge Abraham alisema, “Nimeisoma hii post na kusikitika sana.Mimi na daktari kwa miaka 6 sasa na siamini kabisa kama kuna daktari anaweza kuchomolea watoto oxygen kwa madai yake.Kama amefanya hivyo ni kosa la jinai.Ila kama kuna mgomo na daktari hakwenda wodini kwa sababu kuna mgomo haya ni mambo mawili tofauti.
Kwa sasa mgomo umekamata pabaya maana hakuna hata emergencies zinazoguswa na ni kipindi kibaya sana kuumwa hata kama wewe ni daktari.Nadhani ni vibaya kutumia maelezo ya upande mmoja na kuyatumia kuweka presumptive judgement.
Esther Wasira mdogo wangu.Kwa kazi hii madaktari hujitoa mara zote wanapofanya kazi wakati mwingine bila kulala hadi masaa 36 na sidhani mtu anayejitoa kiasi hicho anaweza kufanya jambo kama ulilolielezea hapo.Wapo wazembe kwenye hii fani lakini hakuna wa kutenda hivi na kama yupo basi hafai kufanya fani hii.”
Kwa upande wake Esther aliongeza kwa kusema, “Isaac I do understand you brother..na wewe kama daktari umejibu vyema tena very objectively!! As you say,ni ngumu kuamini kuna daktari angekuwa mnyama kiasi hiki..what this lady was narrating on the incident ya mwanae,anasema,it was chaotic, they were many of them,charged into the room and switched them off,as a sign of “no more service guys”..!
Mimi nili-panic sana asubuhi..huyu mtu msibani anasema “cause of death” ni mwanangu kutolewa oxygen wakati akiwa Amana anaendelea na matibabu!! So as u say,it might be a presumptive judgment based on the testimony of the mother,but am not pronouncing anybody guilty!! I said earlier,if it gets to the level where the issue has been taken to the hands of the law and the accused tried,the state will declare their status,whether innocent or guilty!! Take this as a charge sheet,that’s the accusation,kinywa cha Mtanzania aliyepoteza mtoto wake ndio kimenena hayo!! So treat me as a spokesperson right now!!”
Mgomo wa madaktari nchini unaendelea kuchukua sura mpya kila kukicha,ambapo juzi Mwenyekiti wa Jumuiya ya madaktari nchini Dr. Stephen Ulimboka, alitekwa na watu wasiojulikana walimpiga kinyama. Kwa sasa bado amelazwa katika hospitali ya Muhimbili akiendelea kupewa matibabu.

source:bongo5

Differentsourcestz kuuzwa na kubadilishwa jina kwenda Infosourcetz.

Leave a comment


Wadau wetu tunapenda kuwa tangazaikuwa blog yetu tunaibadilishajina kutoka Differentsourcestz to infosourcestz baada ya kuuziwa kwa mtu mwingine ambaye ameamua kubadilisha jina. Kuanzia leo Differentsourcestz itaitwa infosourcestz. Management yake itaendelea kama kawaida , nakila kitu kitakuwa kama mwanzo ila kutakuwa na marekebisho ya vitu vichache , na kuongezwa vitu ambavyo havikuwepo mwanzoni, nakufanya kuongeza nyongeza nyingi ambazo zitawafurahisha nyie wadau wetu wakuu, ambao nyie ndio mnafanya infosourcetz kuwepo. Napia haitakuwa dot wordpress tena bali itakuwa infosourcestz.com.

HII NI EMAIL ILIYOANDIKIWA NA HERMY B KWA BLOG YA TEENTZ

1 Comment


Tarehe 23/05/2012 TEENTZ waliandika makala inayosema: ‘Ay na B’Hits na urafiki uliochuja kimya kimya’. Makala hiyo ilijaribu kuangalia uhusiano wa Ambwene Yesaya na Hermy B ambaye ni producer na mwenyekiti mtendaji katika kampuni ya B’Hits Music Group.

Hermy B kulia akiwa na MC wa TPF


AY(Ambwene Yessaya)


Hermy B ambaye ameisoma makala hiyo, ametuandikia email kukanusha baadhi ya mambo tuliyoyaandika na pia kutoa ufafanuzi wa namna mambo yalivyokuwa na yalivyo sasa:

“Ningependa kujibu shutuma zilizoandikwa na blog yako kuhusu uhusiano wangu na swahiba wangu A.Y. Ningependa ifahamike kwamba mimi na A.Y kwa kipindi cha miaka 4 tumefanya kazi za muziki kwa karibu pamoja na kazi nyingine za biashara. Ni kawaida na inaeleweka kwamba mahali popote watu wanapofanya kazi pamoja kugongana katika mawazo au lugha ni jambo la kawaida, na ndio changamoto zenyewe. Si jambo la ajabu kama mimi na swahiba wangu A.Y. kupishana katika kazi.

Baada ya kusoma makala inayonihusu kwenye blog yako nimeona ni umuhimu wa kujibu ni makala yako haswa kuhusu swali linalohusu utu na tamaa ya pesa. Kwanza ningependa ieleweke kwamba umeniweka katika picha ya mtu mwenye tamaa kubwa ya pesa na nisiejali utu picha amabayo imeanza kunisumbua katika shuhuli zangu kwa muda mfupi tu kwani wananchi wameanza kuniona hivyo.

Hivyo nimeona ni lazima nijibu kwani nikiiacha bila kujibu madhara yake yatakuwa mabaya. Kwanza napenda uelewe sijawahi kuwa msimamizi wa kazi za A.Y zaidi ya kuwa producer wa nyimbo zake tu. Kipindi chote hicho nimekua natumia utaalamu wangu kwenye kutengeneza tu muziki wake. Maswala mengine yoooote amekuwa akifanya mwenyewe tena bila msaidizi.

Pia ufahamu bila A.Y na MwanaFA kunipa nafasi kutengeneza muziki wao nisingekua hapa nilipo. Nadhani inaeleweka mahali popote duniani kwamba kipaji ili kifahamike kwa watu lazima kipitie kwa mtu fulani au mkondo fulani. Si ajabu kama kipaji changu cha kuproduce muziki kimeweza kufahamika kwa kupitia kwa A.Y. Mimi sio mungu labda ningekua sehemu nyingine na mafanikio makubwa zaidi au machache zaidi,lakini nachojua rafiki yangu amenipa ngazi ya kufika huku nilipo sasa, sijawahi kuficha hilo na hata wao wenyewe wanajua na bado nashukuru kwa hilo.

A.Y hajawahi kuingia mkataba wa aina yoyote na kampuni ya BHits Music Group Limited wala mimi binafsi uliombana kufanya kazi na mimi na sio mtu mwingine yoyote. Nimetengeneza nyimbo zisizopungua 30 za A.Y, kwa ajili ya albamu yake katika kipindi cha mwaka 2008 mpaka 2011. Baadhi ya nyimbo hizo zimeshatoka na nyingine bado zipo zikisubiri uhitaji wake. Wote tulikua na lengo la kutengeneza muziki kwa wingi na kuuza kwenye soko zuri la muziki ili tufaidike kwa pamoja.

Muda wote muziki ulikua unatolewa na unafanya vizuri kwa radio na T.V na show zilikua zinafanyika na zote nilikua nazijua iwe ndani ya nchi au nje ya nchi hii hata malipo nilikua nafahamu ni kiasi gani na sijawahi kufichwa na A.Y kuhusu hilo.

Utata umekuja kwenye malipo yaliyotajwa kwenye blog yako ambayo yameniudhi sana na baadhi ya wasanii wanaopenda kurekodi kwangu wameanza kuwasiliana na mimi kuuliza bei imepanda lini na kama inawahusu pia.

Kutoelewana kwetu kwetu kibiashara ilikuwa mwezi February mwaka huu yakihusu malipo ya album hiyo. Baada ya hapo niliamua kufunga mdomo wangu na nisingesema chochote kwani haya yalikua yananihusu mimi na rafiki yangu tu. Nimeamua kuongea sasa kwani nahisi nimeshambuliwa kwa mara ya pili kuhusu makubaliano haya na mara ya kwanza niliamua kukaa kimya.

Kwanza nataka ufahamu Katika kipindi cha kutokea 2008 mpaka leo hii (miaka 4) kwa matumizi ya nyimbo hizo, ambazo amekwishafanyia show nje na ndani ya nchi na nyingine kumpatia nominations na tuzo tofauti, nilichowahi kulipwa hakitaweza kuzidi shilingi milioni tatu kwa malipo ya awamu tofauti kwa miaka minne.

Kilichotokea ni kwamba, mwaka huu mwanzoni kabisa, A.Y aliwasiliana na mimi akiwa na mipango ya kuzindua albamu yake. Na alitaka kuzinunua zile nyimbo kutoka kwangu akiwa na mpango mpya wa kuiuza albamu kwa mpango wake binafsi pasi na mimi. Nilishindwa kuelewa nini anakifanya hasa alipoomba alipie wimbo mmoja mmoja tena kwa bei ya msanii wa kawaida anaehangaika kutoka.

Niliamua kukubali kwamba ameamua kufanya hivyo na sina nguvu ya kumzuia basi nikajaribu kupata malipo halisi ya kazi yangu. Ubishi wangu ulikua kwamba msanii mdogo hawezi kulipa bei sawa ya kurekodi na msanii mkubwa, kwani hata malipo ya msanii mkubwa na mdogo baada ya kazi yoyote iwe ya matangazo ama show huwa hayafanani. Bei niliyotaja haikua millioni kumi, ni uongo mtupu na kwa wimbo mmoja niliomba nilipwe millioni 2.

Akakubali kwa bei hiyo ya Millioni 2 japo nilihisi hakuridhika kabisa. Nilimtumia mkataba wa makubaliano yetu ambayo kweli baadae aliona kwamba bei hiyo kwake ni kubwa sana hivyo hatukusaini makubaliano. Tulibadilishana meseji kwa simu kwa muda mrefu sana na niliona biashara hii itavunja urafiki wetu.

Nilifikiria sana kwamba nyimbo hizi nimekaa nazo toka 2008 bila kuingiza chochote na maisha yanaenda pia. Sikuona sababu ya kuharibu urafiki wetu wa muda mrefu kwa mabishano haya. Kwa Ujumbe wa simu nilimueleza A.Y anakaribishwa aje achukue nyimbo zoooooote anazohitaji kwa albamu yake BURE (bila malipo).Lakini nilimuomba anisamehe sitomix zile ambazo bado hazijamixiwa, ila ampatie producer mwingine amfanyie hiyo kazi.

Mpaka naona hii makala A.Y hajaja kuchukua hizo nyimbo na ndio naelewa kua hayupo na BHits tena na wala taarifa zote hizo mbili hajawahi kunipatia. Huu ndio ukweli halisi.

Swala la mimi kuwa na wivu na kinyongo na mafanikio ya A.Y ni uongo na nashangaa umetoa wapi maneno hayo. Kama kulipwa kidogo, huku nikiona A.Y anaingiza fedha nyingi kwa muziki tunaotengeneza pamoja basi ningekua nimegombana nae toka mwaka 2009 labda.

Narudia kwamba nilikua najua kila show yake inapofanywa na sikuwahi kujisikia vibaya. Nataka utambue pia nilikua na akili timamu wakati nafanya kazi na A.Y na muda wowote nilikua na uwezo wa kubadili mawazo na kutaka tuandike makubaliano kwa karatasi ila sikufanya hivyo na wala sijutii chochote kwa utaratibu wetu wa hatari wa kufanya kazi bila mkataba wa maandishi na ndio maana nipo radhi hata sasa kumpatia nyimbo hizo bure kama nlivomwambia hapo mwanzo.

Nina meseji zote na email za mazungumzo yetu ambazo nilihifadhi nikijua ipo siku nitaonekana mimi ndie mkorofi, hivyo nachokisema nina hakika nacho asilimia 100.

Picha nyingine mbaya ulioichora ni kujaribu kuonyesha kuna kutopendana kati ya maproducer. Mimi Master Jay na Marco Chali ni marafiki wazuri tu na mpaka leo hii nikiwa na shida na nikamhitaji Marco Chali au Master Jay nitampigia simu bila aibu kwani hakuna ugomvi kati yetu. A.Y, Master Jay na Marco Chali pia ni marafiki wa siku nyingi na katika kipindi cha miaka minne akiwa Bhits kwa hiari yake na sio mkataba, A.Y amekuwa akienda MJ records anapojiskia na mara kadhaa mimi nimeenda na A.Y na mara kadhaa nimeenda peke yangu tena kwa ajili ya shughuli zangu binafsi.

Pia ufahamu katika kipindi hicho A.Y alikua akitumia muda mwingi MJ Records kuliko Bhits na hiyo yote ilikua ni mipango yake binafsi. A.Y hajawahi kuzuiwa kufanya kazi na mtu mwingine kwani ni msanii huru.

Ndugu yangu mimi ni mtu mpole nisiye na ugomvi na mtu hapa mjini. Nasikitika sana kwa jinsi kwenye makala yako ulivyojitahidi kuonyesha kwamba mimi na swahiba wangu tumejenga uadui.

Wasalaam
Hermes Bariki Joachim (Hermy B)
Managing Director”

source:TEENTZ

Magari wanayo endesha matajiri wakubwa duniani.

1 CommentCARLOS SLIM HELU ni tajiri wa kwanza duniani kutoka kwenye Forbes,. Ni mexico anayemiliki mitandao ya simu anaenesha gari aina ya BENTLEY CONTINENTAL FLYING SPUR yenye thamani ya dola laki 3

Bill Gates nitajiri wapili duniani anaendesha gari aina ya PORSCHE 959 COUPE ambayo n magari 230 yaliyopo duniani kote. Ili bidi raisi Bill Clinton kasaini mkataba wakumruhusu tajiri huyo kuendesha gari hilo ambalo halikujaribu kwenye testini ya majaribio kama linafaa kuendeshwa. Kipindi alipo linunua lili kuwa lina mgharimu dola laki 2 na 25 elfu lakini sasa lina thamani ya dola laki nne

Tajiri mwingine ni Alice Walton ambaye ni mrithi wa supermarket kubwa marekani inaitwa WaL-Mart, ni tajiri wapili kwa upande wa wanawake duniani. Lakini gari anayoipenda ni ford ya mwaka 2006 inayoiytwa FORD F-150 King Ranch. Imnauzwa kwa bei za kawaida dola elfu 40.

Ingvard Kamprad ni mwanzilishi wa kampuni ya IKEA yenye thamani ya dola Bilion 28. Gari analoliendesha ni Volvo 240 ya mwaka 1993. Na kama ataliuza gari hilo litakuwa na thamani ya dola $1500Meya wa New York’s bwana Michael Bloomberg anaye endesha gari aina ya Audu R8. Ambayo show window inauzwa dola laki 1 na 20 elfu, nakimbia speed 60mph kwa sekunde 3.2

Bilionea Larry Ellison, mwanzilishi wa Oracle , ni maarufu kwa magari yake mengi. Katika magari yote anayoyafili ni McLaren F1. Mwaka 1998 ni gari lililotajwa kuwa ni gari linalokimbia mno barabarani. Uzalishaji wa magari hayo ulisimamishwa maka huo huo na wakitaka kuya chuku kwa kila moja lina thamani ya dola milioni 4.1

Warren Buffett ni mmoja wa matajiri wakubwa mno duniani, yeye ni muwekezaji na mjasiriamali mkubwa nchini marekani. Anaendesha gari aina ya CADILLAC DTS, ambapo ununuaji waki wagari hilo iliisaidia kujanyua kampuni ya GENERAL MOTOR ambayo ilikuwa inaanguka. Gari hilo kwenye maduka ya magari lina thamani ya dola elfu 45

Mark Zuckerberg ni tajiri kijana duniania ambaye ni mmiliki wa facebook, na mwanzilishi wa facebook anaendesha gari la aina BLACK ACURA TSX. Yenye thamani ya dola elfu 30 tu.

Tajiri mwingine nitajiri mwenye kampuni ya Computer ya Dell, Michael DELL ambaye anaendesha gari aina ya PORSCHE BOXTER ya mwaka 2004. Ambalo model mpya yake inathamani ya dola elfu 80. Naunaweza kununua gari hili likiwa limetumika chini ya dola elfu 20

Steve Ballmer mmoja kati ya matajiri wakubwa mno dunia. Ambaye yupo ndani ya Microsoft. Ambaye anaendesha gari ya kampuni ya ford HYBRID FUSION. Gari lenye thamani ya dola elfu 19 kwenye maduka ya magari

Mwanzilishi wa NIKE Phil Knight anaendesha gari Aina ya AUDI R8 yenye thamani ya dola laki 1 na 20 elfu, aliepata aina ya black model yenye mapanga ya silva pembeni.

Tajiri mwingine ambaye ni mrithi wangu za Pinault Francois Henri Pinaul anayeshea gari lake na mke wake mzuri Salma Hayek ambayo ni Lexus SUV , ambayo ikiwa mpya inathamani ya dola elfu 40 bila kuipimp, au kuiongeze vitu vingine

LAURENE POWELL JOBS ni mjani wa aliyekuwa muwanzilishi wa kampuni ya apple Steve Job. Ambaye anaendesha gari aina ya Audi A5 ambayo ilikuwa imepaki nyumbani kwake Palo Alto. Ambayo thamani ya gari hilo inaanzia dolsa elfu 37,

Google tycoon Eric Scmidt ndio anayeendesha gari la wastani kuliko wote ambalo ni Toyota Prius. Ambayo haiharibu mazingira “environmental friendly” thamani yake inaanzia dola elfu 11

Older Entries

%d bloggers like this: