Home

Mb Dog arudi kwa kishindo, aachia ngoma mpya na kufungua studio

1 CommentBaada ya kupotea kwa muda mrefu kwenye ramani ya muziki, hatimaye Mb Dog amevunja ukimya kwa kuachia wimbo mpya uitwao ‘The Only One’ alioufanya kwenye studio yake mwenyewe aliyoifungua hivi karibuni, Makopa Inc.
Msanii huyo aliyetamba zamani na kibao ‘Latifa’ amesema kwa muda mrefu alikuwa akifanya mambo yake nchini Ujerumani na sasa ameamua kurudi kwenye game.
Katika mazungumzo ya simu aliyofanya na Bongo5, Mb Dog amesema hana wasiwasi kuwa ataishika tena mioyo ya wapenzi wa muziki wa Tannzania kwakuwa haoni kipingamizi na muziki haujabadilika sana.
“Navyoona najua muziki umechangamka katika njia zake, lakini sio kwamba watu wamebadilika kuimba na muziki utafanyika vile vile kama watu walivyozoea kuusikia, sema tu katika kuanzia kuna harakati zitakuwa tofauti muda mfupi wakati nikitulia kwasababu muda mrefu nilikuwa sijajihusisha na haya mazoezi kwasababu ya mambo yangu binafsi,” alisema.
Aliongeza kuwa ujio wake mpya unaweza kuwa zaidi ya Latifa, “hilo ni miongoni mwa mawazo niliyonayo kwasababu sijaona kama kuna vitu tofauti vinavyofanyika labda vya chinichini ambavyo sivifahamu, lakini kimuziki tu naona uko kawaida na ntafanya vizuri zaidi ya hata hivyo.”
Mb Dog amesema hajamsahau P-Funk Majani ambaye ndiye alimtambulisha kwenye muziki wa Tanzania kwa kumtengenezea hit ya Latifa. “Ujue yeye ndo kama father kwenye muziki huu, ni mtu ambaye akinifanyia kazi anatumia nguvu nyingi sana lakini sasa nimerudi, nimefanya hii ngoma mwenyewe sasabu yeye pia ana kazi nyingi, lakini kwasababu muda upo lazima niende pale kupiga ngoma mbili tatu watu waziskie kutoka pale. Katika albam yangu kuna watu muhimu kama yeye hawawezi kukosa kunipigia nyimbo.”

source:bongo5

MSANIFU MAARUFU WA MAGARI YA FERRARI ITALI PININFARINA AFARIKI.

Leave a comment


Msanifu maarufu wa utengenezaji wa magari ikiwemo miundo ya Ferrari na Fiat Sergio Pininfarina (pichani) wa nchini Italia amefariki dunia nyumbani kwake katika mji wa Turin baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Pininfarina alisanifu miundo maarufu ya magari ikiwa ni pamoja na Ferrari, Fiat na Maseratis na pia magari aina ya Peugeot na Mitsubishi.
Sergio Pininfarina pia alikuwa mbunge wa bunge la Ulaya hadi mwaka wa 1988 na baadaye kukiongoza Chama cha Wafanyabiashara wa Italia.
Waziri Mkuu wa Italia Mario Monti amesema kuwa Pininfarina alizaliwa na kipaji cha kuleta pamoja uzuri na ubora katika kazi yake.
Sergio Pininfarina alizaliwa katika mji wa viwanda wa Turin Kaskazini mwa Italia na amefariki akiwa na umri wa miaka 85.

Madaktari 72 wasimamishwa kazi kwa Mgomo

Leave a comment


Mwenyekiti wa Bodi Kaimu [caption id="attachment_3013" align="alignleft" width="500"] Mkurugenzi wa wa hospitali ya rufaa Mbeya Dr E. Sankey akimsikiliza kwa makini kaimu mkuu wa mkoa Mbeya.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Norman Sigara Aikzungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu kusimamishwa kazi kwa madaktari hao.[/caption]BODI ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, imewasimamisha kazi madaktari 72 kwa kosa la kutoingia kazini kwa siku tano jambo ambalo ni kinyume cha makubaliano ya mkataba.

Imeelezwa kuwa madaktari hao ambao 54 ni wale wa mafunzo ambao waliingia mkataba wa miaka miwili na hospitali ya Rufaa na madaktari 18 ni wale walioajiriwa na Wizara ya afya.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Bodi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Norman Sigara, alisema kitendo cha madaktari kutoripoti kazini kwa siku tano ni ukiukwaji wa kanuni za utumisha wa umma toleo la 2009 kifungu namba F.16-F17 na F. 27.

“Hivyo kupitia kanuni hiyo madaktari hao wamesimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa hatua zaidi za kinidhamu,”alisema Sigara.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wa Bodi, imeelezwa kuwa siku ya tarehe 23/6/2012 wafanyakazi 15 waliokuwa zamu(Intern Doctors 12 na Registrars3) hawakufika kazini na tarehe 24/6/2012 wafanyakazi 19(Intern doctors 15 na Registrars 4) hawakufika kazini.

Alisema, kuanzia tarehe 25/6/2012 hadi leo imethibitika kuwa Interns doctor 54 na Registrars 18 hawakufika kazini hadi leo tarehe 28/6/2012 ambapo tarehe 25/6/2012 bodi ya hospitali ilifanya kikao cha dharura kujadili hali ya utendaji kazi na utoaji huduma hospitalini na kutoa uamuzi.

Sigara, aliyataja maamuzi hayo kuwa ni Mwenyekiti wa Bodi akutane na madaktari ambao hawakufika kazini ili awasikilize sababu za kutofika na kujadili namna ya kumaliza matatizo hayo jambo ambalo madaktari hao waligoma.

Alisema, baada ya madaktari hao kukaidi ombi hilo, Bodi ya hospitali ili waandikia barua za kujieleza kwanini wasichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuvunja mkataba walioingia na hospitali na pia kukiuka
kanuni za kudumu za utumishi wa umma nalo walilikaidi

“Iwapo madaktari ambao hawakuripoti au kueleza sababu za kuridhisha ifikapo tarehe 28/6/2012. Kwa kuzingatia kanuni za utumishi wa Umma, madaktari hao watasimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,”alisema.

Aidha, alisema kuwa kwa ujumala madaktari hao waligomea barua zote mbili yaani ya kuitwa kwenye kikao pamoja na ile ya kuwataka kujieleza hivyo Bodi imechukua hatua za kisheria za kuwafukuza kazi.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa bodi, alisema kuwa tayari hospitali ya Rufaa kwa ushirikiano wa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, madaktari watano wamepatikana ili kusaidia huduma kwa hospitali hiyo.

Alpha: kuwa shutumu kampuni ya East Africa Breweries Limited, (EABL),

1 Comment


Wiki hii mshindi wa Tusker Project Fame msimu wa tatu Alpha Rwirangira wa nchini Rwanda ameandika barua ndefu kuishutumu kampuni ya East Africa Breweries Limited, EABL, kuwa imeshindwa kuwaunga mkono washindi waliopita baada ya show.
Barua yenyewe iliandikwa hivi:
“Naandika barua hii nikiwa na uchungu mkubwa moyoni. Mashabiki wangu wapendwa, inauma sana. Kwanza naishukuru EABL kwa kunitambulisha kwenye midani ya muziki. Lakini niruhusuni tena niseme kukatishwa kwangu tamaa.
EABL inaingiza hela nyingi sana kutokana na washiriki hawa lakini bado haitaki kuwaunga mkono na kuwajali baada ya show. Ningependa kuwapa mfano wa Victoria Kimani, kama angekuwa mkweli na kuwaambia yote aliyoyapitia baada ya kushinda TPF1, ni aibu sana, kama EABL ingekuwepo kwaajili yake ninaamini Kimani angekuwa mbali sana na kipaji chake.
Mwangalie Ester, ni aibu jinsi watu wengi wasivyojua kuhusu yeye na bado hawamjui mwimbaji huyu mwenye kipaji, natamani angesimulia story yake kutokana na njia aliyoipitia baada ya TPF2, ni aibu kubwa.
Sasa kuhusu mimi, ni story ile ile naomba radhi kwa kusema hilo, hata hivyo sina cha kupoteza lakini EABL hili ni kubwa mnahitaji kuwasaidia wasanii wenu, msiwaache wakirandaranda kama kondoo waliopotea.
Mnachofikiria ni kuhusu ninyi wenyewe, inauma sana. Nakumbuka niliandaa show nyumbani Rwanda ambako nilileta baadhi ya wahusika wa TPF akiwemo jaji Ian, na niliwaomba EABL wadhamini show yangu wakapuuzia baada ya kuwaonesha ni kiasi gani ninajituma angalau kuwa mbunifu na kufanya nao kazi.
Ni aibu kwamba nilidhaminiwa na makampuni mengine na EABL haikuwepo licha ya kuwa niliwafuata kuwaomba udhamini kama makampuni yote haya mengine. Waliendelea kunipa ahadi mpaka dakika ya mwisho, ni aibu na inauma.
Na sasa mwangalie kaka yangu Davis, mpaka sasa hivi anahangaika na record deal, EABL sijui kinachoendelea kwenye mkataba wake kwakuwa hakuna kilichofanyika hadi sasa na TPF 5 inaendelea, unadhani watu hawa wanawatendea haki wasanii? Ninashangaa kwanini wanaendelea na TPF5 kama watakuja kufanya sawa na walivyotufanyia sisi sote? Sio haki.
Tafadhali watu msinielewe vibaya lakini watu huwapigia kura wasanii wawapendao na wanapenda kuwaona wakikua na wasipoona kile walichotarajia huwalaumu wasanii, tafadhali naomba mniruhusu kuwaonesha akina nani wanaopaswa kulaumiwa.
Inauma sana. Nimeviweka vitu moyoni mwangu lakini umefika muda niviseme, kwakuwa sina cha kupoteza lakini walau wacha niongee na wadogo zangu ili wasije kukutana na tatizo lile lile. Tafadhali mashabiki wetu tunaomba maoni yenu kuhusu suala hili.”
Maoni yetu
Kwanza kabisa tungependa kukubaliana na madai yake hayo dhidi ya waandaji wa Tusker Project Fame kwakuwa wanawajibika kuhakikisha kuwa washindi waliopatikana wanapewa uwezo wa kuja kupambana na wasanii wengine waliotoka kwa njia ya kawaida.
Barua ya Alpha imetukumbusha makala tuliyowahi kuiandika hapa Bongo5 kuhusiana na jinsi mashindano mengine kama hayo ya hapa Tanzania, Bongo Star Search yanavyotoa washindi wasioweza kumudu ushindani wa muziki. Barua hiyo ikatuamsha kuwa kumbe pamoja na mbwembwe zote hizo za TPF, hawachekani na BSS. Wote wale wale. Hutoa washindi ‘vibogoyo’ wasioweza kumudu soko la muziki baada ya kutoka huko.
Aliyoyasema Alpha kuhusiana na ukimya wa washindi wote wa awali wa mashindano hayo ni kweli. Ukianza na Victoria Kamani, leo hii ukiwauliza watanzania mia moja tena wale wapenzi wa muziki, huenda mmoja tu ndo anaweza kuwa anamfahamu.
Kwanini hafahamiki? Well, sababu ya Alpha ni kuwa EABL imeshindwa kumsupport! Swali kwa Alpha ni kuwa, mbona kuna vijana wanafanya muziki katika mazingira magumu kabisa lakini wanafanikiwa. Wapo waliotoka bila msaada wa maana kutoka kwa mtu ama kampuni. Wapo waliotoka mikoani na shilingi laki mbili tu za kurekodia wimbo na kulala kwa washkaji zao Dar es Salaam, lakini leo ni masupasta hata kama hawana kipato kikubwa kivile, kama mtu huyu anavyosema kumjibu Alpha, “Kaka well use the example of your cousin AY. He hustled his way out through the industry and got to make it big. EABL gave you a shortcut to being there in two months and gave you a big fund that most East African artists could hardly make in their early stages of music career! ‘
They prepare you enough for the competition out here I believe. What you got to do now is simply focus ahead and not drain your energy blaming boss wa jana! Instead muonyeshe uwezo wako by opening kampuni yako leo! So wewe kamua huko CA upae zaidi!”
Kwanini hawa akina Alpha ambao kwanza hupewa airtime kila weekend wakati wa mashindano hayo kwa kuonekana live wakiimba kwenye TV, lakini wakipata ushindi na kupewa kitita cha mamilioni ya shilingi hushindwa kufanya lolote.
Alpha alipewa zawadi pamoja na mambo mengine, shilingi milioni tano za Kenya ambazo ni zaidi ya shilingi milioni tisini za Tanzania. Hela zote hizo na bado anataka EABL waendelea kumshika mkono?
“Please Alpha, don’t mislead the people.. They did what they were supposed to do and it is puting you and your colleagues in the limelight, now it’s up to you and no one else.. And for the sponsoring a show part, that’s very different and the have all the rights to accept or decline. Dont mislead us please,”aliandika mtu mmoja chini ya barua hiyo ya Alpha aliyoiandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Mwingine aliongeza, “Tusker project fame is a Launchpad, they promise the winner %5million which they give, they don’t promise to offer any other support like sponsoring events. There are so many people who need that exposure they gave you…. It’s the artist duty to work hard after TPF…. EABL is not a Musician nurturing company…If an artist doesn’t work hard after tpf, they can’t breast feed them.”
Akiwa na milioni tisini alikuwa na uwezo wa kurekodi wimbo sehemu yoyote anayotaka na kufanya video nzuri. Ama hela zimeshaisha na sasa anataka EABL wamwongezee zingine? Huo utakuwa ni mchezo wa pwagu na pwaguzi wa kusindikizana siku nzima.
Labda cha maana sana ambacho EABL na TPF wanapaswa kufanya sasa hivi ni kuwajengea washiriki uwezo wa kujitegemea na kusimama wenyewe watokapo kwenye mashindano hayo. Kamwe hawawezi kufanikiwa kama wasanii wenyewe watakuwa wakitegemea walishwe kila kitu.
Leo hii washindi waliopita wakiwemo Esther na Davis wa Uganda ni kama wanatakiwa waanze tena upya kama underground! Watu wamewasahau. Jambo linalotushangaza ni kuwa mbona wakati wakiimba kwenye mashindano hayo walionesha vipaji vya hali ya juu kuzidi hata wasanii wengi wakubwa waliofanikiwa?
Wanapokuja huku nje, nini hutokea? Ama ni ngumu sana kwa msanii aliyeshiriki mashindano ya vipaji kukubalika kwenye mainstream music? Majibu ya maswali haya ni magumu mno kuyapata.
Ushauri kwa Alpha na washindi wengine wa TPF ni kuwa wakubali sasa hivi wapo wenyewe na wanatakiwa kuhangaika kivyao.Muda wa kulishwa na wao kumeza tu ulishaisha tangu washinde. Wajifunge kibwebwe hasa kupambana na wasanii wengine waliotoka kawaida.
Bila hivyo wataendelea kulalamika maisha yao yote. Endelea kusonga mbele kama ulivyowahi kuimba and be man! The strongest man in the world is the man who stands alone.

source:bongo5

AJALI YA NDEGE KATANGA DRC CONGO

Leave a commentPichani juu ni ajali ya ndege iliyotokea Jumatano Juni 20, 2012 katika jimbo la Katanga nchini DRC Congo. Ndege hiyo ilikuwa imebeba wafanyakazi wa migodi ya Mpweto na Dikulushi. Abiria wote waliokuwemo katika ndege hiyo walinusurika ambapo abiria mmoja alijeruhiwa kutokana na kutofunga mkanda.
Picha na Mdau Gervas ambaye ni mmoja wa Watanzania wanaofanya kazi katika migodi ya Mpweto na Dikulushi.

Picha za Dimond akiwa Ndani ya Mj-Recordz akiumiza kichwa kutengeneza Tangazo la Coca Cola

Leave a comment


Marco Chali na Diamond wakiwa studio wakitengeneza Tangazo hilo

Diamond akiwa anaandika Mistari,

Muziki sio rahisi kama mnavyo dhani, Angali jinsi jamaa anavyojituma kufanya kazi


Muziki sio rahisi kama mnavyo dhani, Angali jinsi jamaa anavyobadilisha mapozi, Lakini anaonekana anaipenda sana kazi yake


Muziki sio rahisi kama mnavyo dhani, Angali jinsi jamaa anavyoumizwa kichwa kutengeneza kazi zake.

JK AAPISHA MAKAMISHNA WAPYA WA TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI.

Leave a comment


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mwenyekiti wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Bw. Cornel Kananila Mtaki katika hafla fupi iliyofanyika Jumatatu Juni 18, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam.

Kamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Bi. Mary Cresent Massay akila kiapo.

Bi. Salma Abdi Chande akila kiapo cha kuwa Kamishna katika Tume hiyo.

Bw. Evod Paul Mushi akila kiapo kuwa Kamishna wa Tume hiyo

Bw. Sauli Herbert Kinemela akila kiapo

Bw. Yahya Kitambazi Msigwa akila kiapo.

Rais Jakaya Kikwete, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dkt Milton Makongoro Mahanga katika picha ya pamoja na Makamishna wapya wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi.

Rais Jakaya Kikwete katika picha na Makamishna wapya wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi.


Rais Jakaya Kikwete katika picha na Makamishna wapya wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo asubuhi amewaapisha wajumbe sita wa Tume ya Usuluhishi na uamuzi

Wajumbe walioapishwa ni Bw. Cornel Kananila Mtaki ambaye anakuwa Mwenyekiti wa tume hiyo ambapo makamisha ni Bibi Mary Cresent Massay, Bibi Salma Abdi Chande na Bw. Evod Paul Mushi.

Makamishna wenginei Bw. Sauli Herbet Kinemela na Bw. Yahya Kitambazi Msigwa.

Wajumbe wa tume hii wanashika nafasi ya tume ya awali ambayo ilimaliza muda wao mapema mwaka 2011, ambapo wajumbe wa tume iliyoapishwa leo waliteuliwa mwishoni mwa mwaka 2011.

Wakati huo huo Rais amekutana na kufanya mazungumzo na Baraza la Michezo Tanzania (BMT) na Viongozi wa Chama cha riadha nchini ambapo amewataka viongozi hao wafufue mchezo wa riadha hapa nchini.

“Kama kuna kitu mnataka serikali isaidie itawasaidia , lakini mchezo wa riadha kama michezo mingine, inahitaji juhudi za vilabu vya michezo yenyewe, na serikali inachangia tu lakini jukumu kubwa ni lenu.”. Rais amesema na kuwapa changamoto ya kuanza juhudi zao hizo katika ngazi za chini, ambapo ndipo wanapoweza kuvitambua vipaji vya watoto, kuvikuza na hatimaye kuviendeleza.

Rais amewakumbusha viongozi hao kuwa ahadi yake ya kusaidia michezo iko palepale, ambapo yuko tayari kugharamia wakufunzi au walimu wa michezo mbalimbali nchini kwa ajili ya kukuza michezo hiyo hapa nchini.

Miaka ya nyuma, Tanzania ilikuwa inavunja rekodi mbalimbali duniani katika riadha kutokana na wanariadha wake ambao walikua mahiri na wenye viwango vikubwa duniani, lakini katika miaka ya hivi karibuni hali ni tofauti na juhudi za kuendeleza pale walipoishia hazijawahi kufanikiwa.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Waziri wa Habari, Vijana na Michezo. Dr. Fenela Mukangara na Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Sethi Kamuhanda.

Rais amewataka viongozi hao wa riadha nchini kuwa wabunifu zaidi, kushirikisha wadau wengine wenye mapenzi na moyo na riadha , ili wapate kufikia malengo yao.

Mwisho.

Imetolewa na

Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,

Premi Kibanga, Ikulu DSM.

18 June 2012.

source:dewjiblog

Older Entries

%d bloggers like this: